Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Je atausoma huu uzi ama kushaurika kukataza mikutato ya kisiasa inatosha kujua kwamba hataki kushauruka (usiwe una twanga maji kwenye kinu)
 
Siku tutakayoamua kama watanzania kuongelea vipaumbele vyetu na namna ya kuvifikia itakuwa mwanzo wa hatua za uhakika!HAKUNA shaka kwamba tunahitaji.

1. Maji ya uhakika-hii itasaidia jamii yote yaani wakulima (umwagiliaji), ufugaji,viwanda na maisha kwa ujumla

2. Usafiri/miundombinu- hii itasaidia mtawanyiko wa bidhaa kwa bei nafuu na kwa urahisi hivyo kupunguza makali ya maisha kwa raia

3. Umeme wa uhakika- huu utasaidia viwanda,elimu,afya na sekta nyingine
Lazima tuzungumzie haya na tuyafanye kwa nguvu zetu na Mali zetu zote!Otherwise tutaendelea kuimba wimbo wa Bashite,TLS,usaliti na kila aina yake unaopigwa mbele yetu.
 
Bila kupoteza mda, Mheshimiwa Rais Magufuli usiamini watu wako kupita maelezo na pia sikiliza ushauri wa watu.

Kusikiliza ushauri haina maana lazima uwe ule unaopewa na washauri wako bali maoni ya watu mbalimbali na wengine hatuko huko serikalini.

Tukio la video mpya kutoka radio ya mawinguni linakuchafua wewe moja kwa moja na nikutokana na kutosikiliza sauti za watu, wengine wakiwa mawaziri wako.
Wapo walioamua kukaa kimya, pia ukimya wao ulikuwa ni ushauri kwako lakini uliwapuuza kutokana na imani yako kwa 'dogo' au sababu zingine unazojuwa wewe (inawezekana ni ungumi jiwe).

Natambua pia tukio hili linaweza kuwa ni kijisababu cha kumtema 'dogo' ili kuuwa soo la makaratasi tunayopewa baada ya kumaliza shule halafu wale watu wa mawinguni akamalizane nao pembeni.
 
Enzi hizo kulikuwa na chuo cha kufunza makada wa chama ambao baadae walipatikana viongozi wenye busara na heshima kuongoza serikali na mashirika ya umma,kwani bwana wewe huyu mtoto wa jicho ulimfukua dampo gani!
 


Hiyo video haitoshi, wekeni maongezi yote aliyoyanena. Hakuna ukweli wa maneno yanayoandikwa.

Ni kiongozi na lazima alindwe na polisi.

Makonda oyeeeeeee
 
Mheshimiwa rais Magufuli, huu ni waraka wangu kwako:

Sasa hivi upo katika kuinyoosha nchi, ilikuwa inajiendea tu, watumishi walifanya kazi kwa mazoea, viongozi nao vivyo hivyo, wanaccm alkadhalika.
Mheshimiwa umejitoa mhanga, ni lazima upambane kweli kweli, hasa na watu wa kutoka kwenye chama chako ambao wanajitahidi kukukwamisha kwa kuwa unagusa maslahi yao au ya wafadhili wao au jamaa zao.

"Hapo kwenye kamati kuu, mpaka halmashauri kuu tengeneza vichwa vyako, vyenye maslahi ya chama na nchi kwa ujumla wake, na pale bungeni yule katibu wa wabunge wa ccm akufai, alitakiwa yeye ndiye angemwajibisha mapema kabisa yule mbunge wa CCM aliegawa muda kwa wapinzani, wewe ungepata taarifa tu, hao ndio wachawi wenyewe.

Katika nafasi zako za kuteua wasaidizi, usisikilize mpinzani kasema nini au kataka nn, we angalia utaemteua atakusaidia vipi maadam hauvunji sheria za nchi, watasema mchana usiku watalala.

Mwisho baba angalia wachapa kazi, usiangalie elimu zao, au vyeti vyao, "Mwalimu Nyerere alipomchagua mheshimiwa Kawawa kuwa waziri mkuu, sio kama akuwaona wasomi akina Oscar Kambona, Sir Kahama n.k bali alimchagua kutokana na imani yake, uadilifu, utiifu na kuyasimamia vyema maagizo ya rais wake"

Kwahiyo baba unaowateua, au kuwapitisha katika nyanja mbalimbali za uongozi, akikisha unapitisha watu watakaosimamia na kutekeleza maagizo yako na ilani ya chama chako.
 
Mkabila, mbaguzi, chuki, visasi, roho mbaya hawezi fanikiwa kwa chochote sababu ya hila zake
 
Huu sio ushauri bali ni kujipendekeza kwako, hakuna ushauri wa hovyo kama huu unao tekelezeka na mwenye akili
 
Ateue watu wake kwasababu nchi na chama ni mali yake....
Asiangalie vyeti wala elimu ya mtu yeye ateue tu....
Mwalimu Nyerere alipomteua Kawawa alikuwa ana degree ngapi kwa majina tofauti?
Nani anapinga Rais kumteua mtu asiye na vyeti?
 
Mshauri afukuze makonda
 
Ukibeba gunia la kimba lazima majimaji yakuchuruzikie mwilini

La bashite tayari,magunia bado yako mengi
 


Matumaini yangu pia lazima akaze buti Rais wetu.

JPM oyeeeeeeee
 
Makada wanavamia ofisi za watu na SMG halafu unamwambia mwenyekiti afanyeje? CCM mna matatizo makubwa sana ya akili
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…