Mheshimiwa rais Magufuli, huu ni waraka wangu kwako:
Sasa hivi upo katika kuinyoosha nchi, ilikuwa inajiendea tu, watumishi walifanya kazi kwa mazoea, viongozi nao vivyo hivyo, wanaccm alkadhalika.
Mheshimiwa umejitoa mhanga, ni lazima upambane kweli kweli, hasa na watu wa kutoka kwenye chama chako ambao wanajitahidi kukukwamisha kwa kuwa unagusa maslahi yao au ya wafadhili wao au jamaa zao.
"Hapo kwenye kamati kuu, mpaka halmashauri kuu tengeneza vichwa vyako, vyenye maslahi ya chama na nchi kwa ujumla wake, na pale bungeni yule katibu wa wabunge wa ccm akufai, alitakiwa yeye ndiye angemwajibisha mapema kabisa yule mbunge wa CCM aliegawa muda kwa wapinzani, wewe ungepata taarifa tu, hao ndio wachawi wenyewe.
Katika nafasi zako za kuteua wasaidizi, usisikilize mpinzani kasema nini au kataka nn, we angalia utaemteua atakusaidia vipi maadam hauvunji sheria za nchi, watasema mchana usiku watalala.
Mwisho baba angalia wachapa kazi, usiangalie elimu zao, au vyeti vyao, "Mwalimu Nyerere alipomchagua mheshimiwa Kawawa kuwa waziri mkuu, sio kama akuwaona wasomi akina Oscar Kambona, Sir Kahama n.k bali alimchagua kutokana na imani yake, uadilifu, utiifu na kuyasimamia vyema maagizo ya rais wake"
Kwahiyo baba unaowateua, au kuwapitisha katika nyanja mbalimbali za uongozi, akikisha unapitisha watu watakaosimamia na kutekeleza maagizo yako na ilani ya chama chako.