Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Huyu raisi hapangwi,hashauriwi,hajaribiwi,alichukua form mwenyewe,alijichagua yy mwenyewe,lubuva akamtangaza tu ! kuna aliyewahi kutokea chini ya kua kama huyu ?sasa asubiri kifuatacho kwa wanaojulikana kwakua kaenda kwao kwa misifa yake na kujipandekeza,akamdhihaki Mungu na kujiita mpenzi wa Mungu,kisha akatapika nyongo yake kwa jirani hadi alipotosheka.huku nyumbani hakukaliki wananchi roho zimeharibika,sasa amebaki kuigiza na majenerali wanapigwa risasi malangoni mwao ili kupata suluhu ya Lisu.pazuri hapo ! Kila mteule anapangiwa tamko lake na nini chakusema ! Mbona hapo nyumba hayakuwepo Haya? Spika ndo kabisa anamsingizia mpaka mbunge wa ccm kulipia ndege iliyomsafirisha Lisu kumbe baba wa watu alitumia tu Mali kauli ! Kiongozi wabunge huyo aliyedhamiria kuuwa mtu kwa rungu wakati wa kampeni ! Jamani tuachwe na sisi tu toe ya moyoni,hii ipo kikatiba msituletee wasiojulikana kwa kutumia haki yetu ya kujieleza ! Ammmah ! Sasa hivi haruhusu tena watu kumuombea Lisu ili kuthibitisha nia yake yakutaka Lisu afe,na hatapewa tiba za kibunge kama wabunge wengine,kwakua anachotaka yeye ni Lisu kufa ! Wewe masihi wa kuzimu,kama risasi haikugusa kichwa cha Lisu na hajafa mpaka leo kwanini usiamini uweza wa Mungu ktk hili,na ukatubu,na kuiunganisha tena nchi watu wapendane na kusaidiana kama hapo mwanzo ?nchi imesambaratika kiasi kwamba huhitaji hata kuelezwa,unaona tu kwa macho yako.Mungu nakusihi,asiyependezwa na umoja wetu wananchi mkatae Nawe asiwe na umoja nawe kati ya uliowakusanya katika umoja wa upendo /kupendana.kwakua upendo ndiyo amri yako iliyo kuu.mfedheshe dunia yote ubaya wake ukaenee malango yote ya dunia kwa alama ya damu ya Lisu,asikubalike hata ardhini atakaporejea mwisho wa uhai ukimfika,Amen.
 
Kutegemea na ulipo, wanaweza kutumiasheria ya mtandao kupata habari zako kwa Internet Service Provider wako, kutoka hapo wanakufuatilia mpaka kwako.
Hii sheria nafikiri JF walitaka mahakama kutoa tafsiri ya baadhi ya vifungu kwani vinakandamiza uhuru wa kutoa maoni.
ile kesi sijui imefikia hatua gani
 
Mimi nilidhani kauli ya Kikwete kwamba wapinzani si maadui ingemfungua macho huyu na kuamua kubadilika kwa manufaa ya Watanzania wote na vizazi vijavyo.

Siku chache baadaye ndiyo hilo tukio la kutisha la kutaka kuchukua uhai wa Lissu na kauli zilizofuatia baada ya tukio hilo kutoka kwa ndugai na polisi hazitoi matumaini yoyote ya nchi yetu kuwa shwari tena hivi karibuni.

Mtu ambaye anaitakia nchi yake mema hawezi kutoa kauli za hovyo kama hizi ambazo hana haki ya kuzitoa kwa yoyote yule nchini.

Nasikitika kusema laana ya Muumba wetu imeangukia nchi yetu na kama hakukuwa na umakini mkubwa wa kuzikataa chuki na vitisho ili kuurudisha upendo na mshikamano uliokuwepo miaka ya nyuma, basi laana hiyo ya Mungu itaendelea kuiadhibu Tanzania kwa miaka chungu nzima ijayo. Ukipanda bange usitegemee hata siku moja kuvuna mpunga.



 
Afanye maridhiano na nani??? Wakati hakuna aliyemshawishi kuchukua form za kupigania urais na hakuna aliemchangia gharama za kampeni. Maridhiano ruksa atakapostaafu.
Ila Ngosha ana Kibri!!!!
Albadiri itulipie!!!
 
Hiyo level mtoa mada ya majirani kunyimana hao bado wananafuu kubwa.Mimi nimeshuhudia katika level ya familiya.Kijana alikuwa anakaa na baba take mdogo akisomeshwa then dogo akashangilia Siku fulani taarifa ya Mbowe kuharibiwa shamba baba mdogo kamtimua na amehapa hatolipa ada tena,wazazi wake hawana uwezo anesema yuko radhi asomeshe mwingine yeyote kutoka familiya ya kaka yake lakini huyo mjadala umefungwa.
 
lini rais aliwakataza kunywa supu lini rais alisema meisaidiane ccm haiwez kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na vibaraka wa mafisadi kila mtu apambane na hali yake kama umetumwa imekula kwako
 
Hii sheria nafikiri JF walitaka mahakama kutoa tafsiri ya baadhi ya vifungu kwani vinakandamiza uhuru wa kutoa maoni.
ile kesi sijui imefikia hatua gani
Wazori wa sheria Tanzania kashakwambia Tanzania ya leo haina rais wala sheria. Bungeni.

Rais akathibitisha hilo alivyoropoka kwamba wanakamata mawasilianobya makampuni.

Sasa unakuwaje na uhakika wakikutaka wataheshimu sana sheria wakati waziri wa sheria kasema Tanzania leo hakuna sheria, bungeni. Unakuwaje na hakika hivyo?
 
Kikwete alishasema mzigo mzito mpe Mnyamwezi.

Makamba alishasema Kikwete aliwabatiza kwa maji, hiyu atawabatiza kwa moto.

Mtu kashasema kuna wastaafu wanawashwawashwa, hata Kikwete mwenyewe inabidi ajifikirie mara mbili kabla ya kusema.

Maana anaweza kuunganishwa kwenye wastaafu wanaowashwa washwa kirahisi sana.

Huyu rais kasema hapangiwi.
 
Waliokimbia umande hawawezi kuelewa kilichoandikwa pamoja na kuwa kipo wazi
kabisa. Magufuli anajenga chuki za kutisha katika jamii ya Watanzania na athari za hizi chuki zimeshaanza kulisambaratisha Taifa na sasa watu wanawindana kwa mitutu ya bunduki na mapanga. Lissu katika jaribio la kutaka kumuua alimiminiwa risasi chungu nzima na watu ambao DAB anawafahamu siku chache baadaye dreva wa Mbunge Heche anashambuliwa na mapanga katika jaribio la kutaka kutoa roho yake.

Tanzania si salama tena na wa kulaumiwa ni Magufuli tu hakuna mwingine.


lini rais aliwakataza kunywa supu lini rais alisema meisaidiane ccm haiwez kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na vibaraka wa mafisadi kila mtu apambane na hali yake kama umetumwa imekula kwako
 
Watu ambao hawastahili kukabidhiwa madaraka na inapotokea kupewa madaraka hayo basi huwalevya na kuwa kama wametumia madawa ya kulevya kwa kauli zao zilizojaa dharau vitisho na chuki. Hebu fikiria leo hii Wastaafu wanaambiwa wanawashwa washwa! Kosa lao ni kuongea ukweli kuhusu kutoridhishwa kwao na hali inavyoendelea nchini. Watanzania wote wasimkosoe huyu huku kukiwa na kila dalili upendo kutoweka kwa kasi kubwa sana.

Akusikilize .... wewe? labda kama huwashwi
 
mhh! hii chuki ni kubwa sana rais asipokuwa makini ataliangamiza taifa letu.
Unafikiri kwenye hali ya vurugu na machafuko nani atabaki salama?
 
Ni lini waziri alitamka hayo maneno huko bungeni?

Bila sheria ni kutengeneza kitu ambacho kitataka kuziba lile gape liloachwa kwa kutoheshimu utawala wa sheria hii ni hatari kubwa.
 
Alisema kuna Wastaafu wana washwawashwa wa ule upande Mwingine. Akapongeza upende wa Mahakama wastaafu wake wametilia.
Upande mwingine ni Serikali na Bunge.

Sasa kwa kuangalia rekodi za karibuni, Wastaafu wa serikali na bunge, ni Mstaafu mmoja tu ndiye aliyetoa kauli tata huko kwa Zuma.

Nafikiri lile ni Onyo, ila Na yeye nasikia Kifua anacho
 
 
Ulishawahi kuishi vijiji vyote hadi upinge hoja yake,kwa taarifa yako ata mimi ninapoishi kuna mgawanyiko mkubwa sana, kwa taarifa zisizo rasmi huenda kuna zahanati moja ya kata fulani ikashindwa kukamilika mpaka diwani ambaye ni wa chama X amalize mda wake ili achaguliwe wa chama Y, Michango kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati inachangwa na wanachama wa chama X.
 
Watumishi wanalia na kusaga meno, Vijana hawana ajira, sekta binafsi inatetereka, kuna makundi yanahitaji milioni 50 yashaunda vikundi. Elimu haieleweki. Wanafunzi 31,000 wamekosa mikopo, wakulima mbaazi wanauza kwa kg 150

- Wanakusubiri wewe
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…