Tukiacha unafiki na tukasema ukweli kama mh Raisi anavyosisitiza, kweli ameanzisha Mambo mengi yenye kuwasha masikio na kusisimua miili yetu lakini karibia yote yanafeli kutokana na ukurupukaji na kutokua na mipaka na miongozo inayompa mwelekeo.
Tujikumbushe haya aliyoanzisha na kufeli:
SAMAKI WA KAGUFULI,
NYUMBA 70, MASAMAKI NA WENZAKE,
MANJI NA MAJEZI YA JESHI,
ACACIA NA MAKINIKIA,
TANZANIA KUA DONA COUNTRY,
MILLION 50 KILA KIJIJI,
Haya Ni baadhi tu ya yale aliyoanzisha na kushindwa Kwa Muda mfupi sana alioingia MAHALA patakatifu.
Namuomba Mh Raisi, wimbo wa msemakweli Ni mpenzi wa Mungu sasa auimbe kwa vitendo kama anavyojua IMANI bila MATENDO imekufa, Ni wakati sasa wakujitengenezea heshima ya kweli. Mtauliza afanyaje sasa atengeneze hiyo heshima? Jibu;
ARUDISHE MCHAKATO WA KATIBA MPYA.
Katiba yenye kipengere kinachosema;
HATA KAMA NI RAISI HURUHUSIWI KUAMUA KWA UTASHI WAKO JAMBO LOLOTE, LENYE MASILAHI KWA TAIFA BILA KULISHIRIKISHA BUNGE, WATAALAMU WENYE UELEWA WA JAMBO HILO PAMOJA NA WANASHERIA.
karibu msaidie raisi kujitengenezea heshima.
moods wenye mitazamo ya kina Jerry Muro hawachelewi kufuta uzi kama juu.