Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Yeye ametoa tip na ameeleza maeneo husika , kwa nini Iwe ngumu? Kuna ugumu gani kwa maofisa husika kujifanya wanunuzi kwenda kununua bidhaa hapo Kariakoo na hatimaye baada ya kujiridhisha kuwakamata?
 
Twitter naona ndio sehem sahihi ya kupeleka hii issue. Muheshimiwa anatumia twitter
 
Wew vip. Hapa kama seeikali ipo serious si wanaenda watu kujifanya wananunua vitu na kama ni kweli wanakamatwa. Mbona simple sana
 
Mkuu, ni rahisi sana kuongea hoja hizo nzuri. But trust me hizo ni nadharia tu, kiuhalisia hakuna mpinzani wa kushinda mwaka 2020. Si udiwani wala si Ubunge.
Wapinzani wenyewe ndiyo hawa ambao wameshindwa kabisa kuwapatia wananchi ownership ya usalama wa kura zao. Wameshindwa kuwafanya wafuasi wao waji feel responsible.
kuna andiko nimeliandika lakini bado najifikiria sana kuhusu kuliachia mitandaoni. Hilo lina mbunu na hila zote dhidi ya upinzani. Kwa kukumegea tu, wapinzani wajiandae kupikea watu kama akina Msukuma, Lusinde, Mkamia na wengineo wasio pendwa na wananchi. Kufikia hapo upinzani utakua umesha jifia rasmi.
Lengo ni kuufuta kabisa upinzani nchini kwa mbinu hizo
 

..pandisha andiko lako ili sote tujifunze.

..ukikaa nalo inaweza ikafika siku ukajilaumu kwa kutolipandisha hapa.

..nakubaliana na wewe kwamba wapinzani wanahitaji watu wengine zaidi ambao wana nia ya dhati ya kuleta MABADILIKO.

..zaidi wapinzani wanahitaji watu very effective ktk kampeni kwasababu CCM watajaribu kila mbinu kuwalaghai wananchi.
 
Ndugu, nikiweka risiti ama jina la duka hapa huoni hata kama maana nzima ya uchunguzi itakuwa imepotea? Hivi kweli ingekuwa duka moja tu kulikuwa na sabbu ya kuanzisha uzi hapa?
Je huyo mmoja tu angekuwa na uwezo wa kuisumbua taasisi nzima?
Ninapata mashaka sana na maelezo yako.
.
Ama wewe ni miongoni mwa wenye maduka hapo Kariakoo na huwa una hiyo michezo hivyo unataka kupata uhakika kama ntakutaja.

Au ni mtumishi ambaye upo serikalini lakini katika utumishi wako una elementi fulani za uzembe, hivyo unataka uletewe kila kitu kisha wewe ufanye maamuzi tu.

Mwisho huenda unajitahidi kupindisha hoja kistaarabu ili hiki kikombe kiepukwe usije ukakinywea.!

Michezo hii ya kutoa risiti isiyo fanana na mauzo halisi ipo maduka mengi kama siyo yote kariakoo hasa ya jumla, hasa kwa wateja ambao ama hutoka Nje ya Nchi au wale ambao wamenunua bidhaa kwenye duka hilo zaidi ya mara moja..

Ushauri wangu.
Watumishi waliopo TRA hasa kitengo cha ukusanyaji mapato eneo la kariakoo masoko ama waondoshwe wote wakianzia na uongozi wao wote.!
Ama wawajibushwe kisha wabadirishwe. Eneo la kazi.
 
Tatizo la siasa za nchi zetu hizi ni kwamba zinazunguka watu, badala ya kuzunguka itikadi.

Ndiyo maana wanasiasa wanahamahama vyama sana.
 
Kwa hali iliyopo, kwa Tume iliyopo, kwa utawala uliopo, wenye imani kubwa kwa matumizi ya nguvu (ingawa kwenye maeneo mengine wanafanya vizuri); bado natafakari kama nitaenda kupiga kura 2020 ama la. Siamini kama kura yangu inaheshimiwa, sioni kama Tume na polisi wanao uwezo wa kufuata matakwa ya wapiga kura.

Vv
 
Hivyo akirudi kutoka kwenye matibabu harafu shughuli za kisiasa zikaruhusiwa kwa mujibu wa katiba, ndani ya muda mfupi upinzani utaimarika mara dufu.
Mbona kuna tetesi kuwa,kaomba hifadhi katika nchi ya Canada.
 
That's why they wanted to kill him.
 
Tatizo la Tanzania sio wapinzani..ni wananchi ...watanzania bado hawako tayari kutetea haki zao..popote pale..ni watu wa porojo nyingi..its our nature..asili yetu inafanana sana na wenzetu wa SADC...ndivyo tulivyo....

Tatizo lingine...Wanasiasa wa nchi hii hawana misimamo ya kiitikadi...mtu mwenye msimamo wa kiitikadi ni vigumu sana kuhamahama vyama...wanasiasa wetu ambao ni reflection ya sote tulivyo ..wanajali matumbo yao zaidi..watanzania wengi ndivyo tulivyo ..mkono kinywani tu.

Tatizo lingine...ni mwaka 1992..watanzania hawakuwa tayari na mfumo wa vyama vingi..walipiga kura na maoni ya zaidi ya asilimia 80 wakavikataa vyama vingi...Kipindi hicho CCM kwa influence ya Mwalimu Nyerere ikaamua KUVIANZISHA vyama vingi...vyama vikaanzishwa vingi kweli..lakini wengi hapa hata hamjui pia CHADEMA nayo ilianzishwa na CCM.Mnijibu hapa ,Je mtoto anaweza kumzaa baba au kumpindua baba kwenye nyumba?

Cha kufanyika;
Kuna wanasiasa ambao wako very legite wamejikuta kwenye hivi vyama watoto wa CCM na wakadhani wana fight same battle...wanasiasa kama kina Lissu..heche..mnyika..mdee....hawakujua kuwa wako kwenye same umbrella ya CCM.

Kwa hali iliyofika CHADEMA imeamuliwa kumaliza muda wake..wa miaka 20..mzazi.ameshaamua...hawa watu legite waunde chama chao ambacho kitakuwa the real opposition....

Its true Lissu ni karata pekee..but Lissu peke yake hawezi...na CHADEMA sio chama sahihi kwake...

TIME is now...

Wajijenge na wala wasilenge 2020..walenge 2025...hapa katikati zifanyike juhudi za makusudi za kuendelea kuwaamsha watanzania...Imani yangu ni kuwa CCM is a dying horse....haya yanayofanyika ni artificial
 
LISU SIYO UPINZANI NA UPINZANI SIYO LISU.

UPINZANI ULIKUWEPO KABLA YA LISU, UMEKUWEPO KIPINDI CHA LISU NA UTAKUWAPO BAADA YA LISU.

KWA HIYO JARIBUNI KUTENGANISHA KATI YA MTU NA MIFUMO YA KITAASISI.

CC: stigajemwa
 
Upinzani waache kuchagua wagombea ubunge wanaotaka wao viongozi...waachie wananchi wa eneo husika watapata wabunge wengi 2020
Kupata 40% kwa awamu ni ngumu mkuu..tena kuna uwezekano ata wabunge wa 5 wasifike labda katiba ibadilishwe lakn kama ni hii, upinzani mwisho wake 2020[emoji51][emoji51]
 
Hivyo akirudi kutoka kwenye matibabu harafu shughuli za kisiasa zikaruhusiwa kwa mujibu wa katiba, ndani ya muda mfupi upinzani utaimarika mara dufu.
Nawasilisha.
Kwani kwa sasa katiba hairuhusu shughuli za kisiasa,au kauli za jiwe zimegeuzwa kuwa katiba?
 
Okay, tumeshaanza kuizoea hiyo singo!
Aiseee......Maskini Lissu wangu anakufa bila tumaini kabisa...anyway fight to the last stand
 
Nyakati za kila mtu kutoka ofisini na kwenda kusimamia kazi kwenye miradi mikubwa na midogo ndio hizi za sasa.

Hizi sio nyakati za kuuza sura kupitia runinga, kwa mtu kuonyesha ufundi wa kuongea ilmradi tu kesho awe ndio kichwa cha habari.

Yeyote yule anaweza kuwa kiongozi mfano wa upinzani, lakini atambue kuwa hizi sio nyakati za kutegemea tu uwezo wa kuongea mbele ya kamera, ni kwenda hatua moja zaidi katika kuchapa kazi.

Watu wanahitaji tija inayoyagusa maisha yao ya kila siku, sio uhasama na ufundi wa ukosoaji halafu tija ni zero.
 
Ndugu zangu wana JF napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Rais wetu mpendwa John P. Magufuli kwa kazi nzuri na kubwa anazozifanya za kuiletea maendeleo nchi yetu ya Tanzania. Sambamba na pongezi hizo nawakaribisha katika jukwaa hili kwa mtu yeyote kutoa maoni na ushauri kwa Rais wetu mpendwa JPM juu ya mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi yetu. Rais wetu ni msikivu na huwa anafuatulia sana mambo nina imani atasoma maoni yako na kuyafanyia Kazi. Naomba kuwasilisha na karibuni kwa maoni,kero na ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…