Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.

Ni kweli media inaweza kutumika vibaya kupotosha. Lakini inaweza pia kutumika kuelimisha na kunyoosha mambo. Huu uwili (dichotomy) upo kwenye mambo mengi na chaguo letu kuendeleza yale mazuri na kuondoa mabaya kwa kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa.
 
Hili ni hitaji muhimu mno! Linaweka mazingira ya usalama wa nchi kwamba hata kama atakuja kiongozi mbovu bado nchi inabaki salama! Paper work ndiyo na kweli inalindwa na mihimili yote iliyo huru. Kama mihimili hiyo siyo imara na huru basi haisaidii kuweka checks and balances zinazotakiwa.
 
Tatizo la kudorora kwa maendeleo ya nchi yetu ni tatizo la kudorora kwa CCM. kudorora kwa CCM kumetokana na kutokuwepo kwa ushindani wa kutosha katika siasa zetu. Kuna haja ya kuweka mazingira ya kuchochea ushindani katika siasa zetu ili ziwe SIASA SAFI.
 
Reli hakuna mtu binafsi mwenye uwezo wa kujenga na kuendesha. Hivyo Serikali lazima ifanye kile ambacho sekta binafsi haiwezi kufanya. Lakini tujiulize, kuhusu ndege: kuna tija gani ambayo tunaipata sasa hivi baada ya kununua ndege ambayo tulikuwa hatuipati kabla? Jibu ni hakuna na hivyo hizo hela ni bora tungezielekeza kwenye SGR. Lakini kwa vile tumeshanunua nashauri hivi:
Dreamliner inahitaji kuwa hewani angalau masaa 4000 kwa mwaka (just to to break even), assuming itakuwa imejaa abiria. Tupate route mbili au tatu za kujaza hayo masaa na zaidi. Dar - Dubai - Guangzhou, Dar - Dubai - Ankara, Dar - Dubai - Bombay. Route zote hizi ni za wafanyabiashara, wanakuwa na mizigo, hivyo provision kwa ajili hiyo sina hakika imewekwa kwenye confuguration ya ndege hiyo. Then tuuze hizo route kwa wafanyabiashara wetu na wengineo. Tuwaondoe kwenye Emirates, KQ, Etihad n.k. tuwarudishe wote nyumbani. Ili kuwavututia wazambia, Malawi, wakongo nk. kupanda ndege yetu ni lazima ijengwe network ya kuwafikisha kwao (connecting flights)
 
Mji kama Dar es Salaam ni sehemu chache sana inafaa kuwekwa miundombinu ya ges . Asilimia karibia 90 haijapangwa. Na sioni juhudi zozote za kulipanga hili jiji. DISASTER!!
Nchi yetu inageuzwa kuwa jangwa kwa sababu ya nishati ya mkaa na DSM ndo haswa mtumiaji mkuu wa mkaa by far. Kwa hiyo faida ya kulipanga jiji ni pamoja na kunusuru nchi yetu kuwa jangwa.
 
Ongeza na Economics, economics!!
 
Msipende tu kubwabwaja vitu "just for the sake of" kubwabwaja, angalieni mifano iliyopo. Ethiopia Airline mbona ina fanya vizuri? Liko chini ya nani?
Hii inasaidia nini kwenye mjadala huu?
Nguvu ya tusi haiwezi kufunika utupu wa hoja!
 
Nguvu ya tusi haiwezi kufunika utupu wa hoja!
 
Tunakuomba ifike wakati tutambue kwamba sisi bado ni tegemezi kwa asilimia kubwa sana kwahiyo hatuwezi kusema kibaya au kufanya kibaya kwa tunaowategemea.

Tunaotaka kushindana nao wana nguvu kubwa wakati sisi ni wanyonge hakika tunajiumiza wenyewe na kusimamisha maendeleo yetu nyuma na kuyarudisha nyuma kabisa.

Mwl.Nyerere kusema hafungamani na upande wowote wakati nchi ni changa kimaendeleo alikosea sana.

Kwako mkuu kiongozi wa nchi,kiongozi wa serikali,Amiri jeshi mkuu,kupingana na kutokua karibu na nchi za magharibi ni kutunyima fursa wananchi na kutuongezea matatizo tunakuomba jumuhika nao ili Tanzania iende mbele.
Tunaaamini wewe ni Raisi bora tunaomba uonyeshe ubora wako.
Wanasema" kama una msitu mkubwa unataka kuchana mbao na huna vifaa na aliyenavyo pekee ni yule jirani uliyekorofishana nae Jana basi yajengeni ili wote mfaidike"
Hili ni Ombi mkuu sio ushauri
 
Hujui thamani ya kura yako!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…