Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Anauliza zina tija gani kwa bibi yake kule kijijini??

Mwambie hata tungechonga barabara,bibi yake hana gari maana ndio uwezo wake wa kufikiri umefikia.
Cha muhimu kwake ni kuwasomesha wale ndugu zake wanaomzunguka bibi yake siku nzima wakiwa vifua wazi ili waje wamjenge nyumba ya kisasa yenye kila kitu ndani.

Uwezo ni mdogo sana kwa watanzania wengi katika kufikiri mambo ya kawaida sana ya kimaendeleo.

Kuna mtu anaitwa Malisa GJ yeye kazi yake huwa ni kurusha humu jukwaani picha za watu wakinywa maji machafu vijijini halafu anauliza hizo ndege zinawasaidia vipi watu wa aina hiyo!.
 
Akifa Leo nafanya sherehe kubwa nitamchinja kambako wangu ninywe mchuzi kwa laha zangu eee Mungu sikia kuomba kwangu
 
Acha kufitinisha makabila. Tumchukie sababu?
Maisha yetu hayamtegemei mtu au mtawala bali MUNGU ambayebanabariki kazi za mikono yetu.
Dec kwa kwanza kwenda homee....
Kielimu mkoa wa kwanzaa...
Tumchukie kwa lipi?
Ninyi mnaomchukia huku kinafiki mnajifanya mnampenda mtapata tabu sana.
Hahah umeita Wachaga kijanja, ngoja tufanye sensa JM!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namshauri afanye haya yafuatayo;
1. Ningemuomba ile nguvu anayoitumia kujenga mji wa Dar es salaam aihamishie katika majiji mengine.
2. Ajikite kuboresha sekta ya afya kuliko kununua ndege nyingi. kumbuka Kila mtu anahitaji huduma ya afya iliyo bora lakini siyo lazima kupanda ndege.
3. Suala la maji na umeme nchini ni tatizo kubwa sana.
 
Nawasalimu wote humu

Kwa muda mrefu huwa nawaza itakuwaje Mhe, Raisi wetu mpendwa akiamua kutoa maagizo kuhusu upandaji wa miti nchi nzima kwa utaratibu kama alioutumia kwenye madawati na maabara? Namaanisha yafuatayo:-

1) Awaite wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote nchi nzima na kufanya nao kikao maalumu kwa ajili ya upandaji wa miti nchi nzima.

2) Aweke mikakati isiyotumia gharama za pesa kutoka serikalini, kama alivyofanya katika ujenzi wa maabara na utengenezaji wa madawati; namaanisha kila kata wachague aina ya miti yenye faida maeneo husika, mfano Matunda, mbao, kivuli au hata miti ya asili (ambayo ni dawa kwa ajili ya kuifanya isitoweke).

Wakishaiaisha aina ya miti, waweke mikakati ya kuiotesha katika vitalu katika idadi kubwa sana kutokana na mahitaji ya eneo husika (naamini 100% inawezekana kwa sababu nimeshafanya kazi maeneo kama hayo).

3) Baada ya kuotesha kila kaya ipewe miti ipande maeneo yanayozunguka maeneo yao wanayoishi, mipaka ya mashamba, n.k mwanzoni kabisa mwa msimu wa mvua ili kuiwezesha miti ipate maji ya mvua na kupunguza kazi ya umwagiliaji.

4) Sheria kali kuhusu miti hiyo ziwekwe kwa wananchi kuhakikisha inakua, mf mti ukifa kwa sababu yeyote ile ya kizembe hatua kali za kisheria zichukuliwe vinginevyo kama kuna aliyeharibu aripotiwe katika ofisi au hata polisi kwa ajili ya uwajibikaji.

Nimeandika kwa kifupi ili kutoa picha kidogo jinsi ya kuifanya lakini, naamini inawezekana na inapendeza sana ikitekelezwa.
 
NAUNGA MKONO HOJA KWA 100%,Nchi yetu baada ya miaka 50 mpaka 100 ijayo kuna hatari kubwa sana ya kugeuka jangwa..Maeneo mengi ya Nchi yetu yana uhaba wa miti..Sehem kama Morogoro ambapo zamani ilikuwa ikisifika kwa mito mingi inayotiririsha maji misimu yote iwe kiangazi,masika,vuli,kipupwe nk leo hii imekuwa hadithi za kusimuliwa kwenye vitabu..Watu wanakata miti sanaa na hovyo kwa ajili ya Mkaa na Mbao lakini hawajishughulishi ktk upandaji..January Makamba alianzisha kampeni nzuri ya upandaji miti kuanzia shuleni,kila mwanafunzi anakabidhiwa miche kadhaa ya miti na kuhakikisha anaisimamia hadi inakuwa sijui sasa imeishia wapi maana siiskii tena..Pamoja na kwamba kipaumbele kikuu cha serikali yetu kiko kwenye SGR lakini naamini kwa hili halihitaji pesa nyingi ili kuweza kulifanikisha..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwe na mpango wa kukopesha Maliki ya gesi na mitungi yake ili kuongeza watumiaji. Hili litapunguza matumizi ya kuni na mkaa.
Sio kukopesha tu pia serikali iondoe kodi zote zinazohusiana na gesi ya kupikia ikiwezekana pia itoe ruzuku kwa gesi ya majumbani ili iweze kumfikia mwananchi wa chini kwa bei ya chini zaidi kuliko hata gharama ya kuni.

Maendeleo hayana chama
 
Sio kukopesha tu pia serikali iondoe kodi zote zinazohusiana na gesi ya kupikia ikiwezekana pia itoe ruzuku kwa gesi ya majumbani ili iweze kumfikia mwananchi wa chini kwa bei ya chini zaidi kuliko hata gharama ya kuni.

Maendeleo hayana chama
Kama wataweza hili utakuja kukuta hata mti ukatike utaoza uwe mbolea hakuna atakae kata miti hovyo.

Tunakata miti out of desperation. Nishati mbadala ni kwa wenye uwezo tu.
 
Kama wataweza hili utakuja kukuta hata mti ukatike utaoza uwe mbolea hakuna atakae kata miti hovyo.

Tunakata miti our of desperation. Nishati mbadala ni kwa wenye uwezo tu.
Hahahaaaa ila mkuu jinsi anavyo kumaindi akisoma tu huu mchango wako ataongeza kodi makusudi ili akukomoe,
Maana anadai yeye hua hapangiwi

Maendeleo hayana chama
 
Hahahaaaa ila mkuu jinsi anavyo kumaindi akisoma tu huu mchango wako ataongeza kodi makusudi ili akukomoe,
Maana anadai yeye hua hapangiwi

Maendeleo hayana chama
Na sisi hatumpangii kuwa rais next term tunafunga na kuomba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom