Nawasalimu wote humu
Kwa muda mrefu huwa nawaza itakuwaje Mhe, Raisi wetu mpendwa akiamua kutoa maagizo kuhusu upandaji wa miti nchi nzima kwa utaratibu kama alioutumia kwenye madawati na maabara? Namaanisha yafuatayo:-
1) Awaite wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote nchi nzima na kufanya nao kikao maalumu kwa ajili ya upandaji wa miti nchi nzima.
2) Aweke mikakati isiyotumia gharama za pesa kutoka serikalini, kama alivyofanya katika ujenzi wa maabara na utengenezaji wa madawati; namaanisha kila kata wachague aina ya miti yenye faida maeneo husika, mfano Matunda, mbao, kivuli au hata miti ya asili (ambayo ni dawa kwa ajili ya kuifanya isitoweke).
Wakishaiaisha aina ya miti, waweke mikakati ya kuiotesha katika vitalu katika idadi kubwa sana kutokana na mahitaji ya eneo husika (naamini 100% inawezekana kwa sababu nimeshafanya kazi maeneo kama hayo).
3) Baada ya kuotesha kila kaya ipewe miti ipande maeneo yanayozunguka maeneo yao wanayoishi, mipaka ya mashamba, n.k mwanzoni kabisa mwa msimu wa mvua ili kuiwezesha miti ipate maji ya mvua na kupunguza kazi ya umwagiliaji.
4) Sheria kali kuhusu miti hiyo ziwekwe kwa wananchi kuhakikisha inakua, mf mti ukifa kwa sababu yeyote ile ya kizembe hatua kali za kisheria zichukuliwe vinginevyo kama kuna aliyeharibu aripotiwe katika ofisi au hata polisi kwa ajili ya uwajibikaji.
Nimeandika kwa kifupi ili kutoa picha kidogo jinsi ya kuifanya lakini, naamini inawezekana na inapendeza sana ikitekelezwa.