Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Katika baraza lake la mawaziri, tashtushwa sana iwapo waziri mkuu hatokuwa MWAKYEMBE na waziri wa nishati hatokuwa Prof. MUHONGO.
Hawa jamaa ni wasaidizi wa rais muhimu sana kwenda na kasi yake.
LUKUVI apewe wizara ya uchukuzi akashughulike na wizi pale.
Mambo ya nje, JANUARI MAKAMBA,
Spika, Zungu
Fedha, MIGULU.
 
Siasa mshaona kama ushabiki wa mpira na viongozi mnaowapigia debe, mnaongea tu kama mnavyopendekeza majina ya wachezaji wa timu mnazozishabikia.
 
watanzania wanajifanya washauri wazuriii kwa serikali kama wanajua kumbe bure kabisa.
hii serikali nyingine mnajaa nafasi ukurasa wa JF
 
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi ametoa ahadi hewa ya kulipa madai ya wastaafu wa ATCL alipokutana na uwongozi wa PPF mapema mwaka 2015.
Uwongozi wa PPF uliushitaki uwongozi wa ATCL mahakamani kwa kutowakilisha makato ya PPF ya wastaafu hao kwa miaka kadhaa wakiwa kazini hali iliyopelekea kulipwa mafao pungufu ya stahiki yao.
PPF ilishinda kesi na kupewa amri ya kukamata mali za ATCL.
Kuona hivyo uwongozi ATCL ulipeleka hukumu hiyo wizara inayo simamia kampuni hiyo, WIZARA YA UCHUKUZI. Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi alikwenda kuonana na uwongozi wa PPF na kuahidi kulipa madai hayo kabla ya mwisho wa mwezi March, 2015. Hadi leo hii hakuna kilicho lipwa. Viongozi hawa PPF na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi wamepuuza amri ta mahakama na kuendelea kuwatesa wastaafu huku wao wakinufaika na nafasi walizo shika.
Tunaomba mheshima raisi uwasaidie wastaafu hawa kwani walioshika madaraka ofisi za umma wajiona miungu watu.
Ewe MOLA MZIDISHIE UJASIRI WA MAAMUZI RAISI MAGUFULI, AMEN
 
rushwa kwa jeshi letu la polisi imegeuka kua utamaduni kiasi kwamba imegeuka kua kero isiyovumilika tena hasa kwa baadhi ya askari wake wanaosimama ktk barabara kuu iendayo zambia kutokea dar polis wanachukua rushwa bila chembe ya aibu. ninani atawaondoleaa watanzania wanyonge uonevu huu? je mamlaka zinazohusika haziyaoni hayo? namuomba mkuu wa jeshi la polisi atwambie ikiwa jeshi la polis limerasimisha rushwa ndani ya chombo hicho mhm kabisa kwa usalama wa wananchi
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kuna haja Jerry Muro afanye tena ile kazi yake ili watakaodakwa waende na Maji.
Tena ukimpa buku anawaambia haitoshi.
Mpaka wana negotiate rushwa
 
kama mishahara haitarekebishwa kufuatana na maisha yalivyo haiwezekani kuzuia rushwa kwani kila mtu atajitahidi kuongeza kipato kupitia kazi anazofanya
 
Hapa chura mbele ya Kiracha mbona ni kawaida hawa traffic police kuchukua bubu hadi buku 2 katika magari ya abiria na mizigo
 
kama mishahara haitarekebishwa kufuatana na maisha yalivyo haiwezekani kuzuia rushwa kwani kila mtu atajitahidi kuongeza kipato kupitia kazi anazofanya

Mkuu unapendekeza polisi walipwe shilingi ngapi? Net salary?
 
Jamani kusimama mbele ya watu na kuanza kuongea ndiyo apewe nafasi serikalini? only in Tanzania.
 
kama mishahara haitarekebishwa kufuatana na maisha yalivyo haiwezekani kuzuia rushwa kwani kila mtu atajitahidi kuongeza kipato kupitia kazi anazofanya[/QUOTE

Wala rushwa sugu hawana cha maboresho ya mishahara, mtumishi anapewa mshahara sh.1,000,000/= kwa mwezi still anaomba rushwa ya sh.3,000/=!
 
Katika baraza lake la mawaziri, tashtushwa sana iwapo waziri mkuu hatokuwa MWAKYEMBE na waziri wa nishati hatokuwa Prof. MUHONGO.
Hawa jamaa ni wasaidizi wa rais muhimu sana kwenda na kasi yake.
LUKUVI apewe wizara ya uchukuzi akashughulike na wizi pale.
Mambo ya nje, JANUARI MAKAMBA,
Spika, Zungu
Fedha, MIGULU.

Nakuunga sqna mkono mkuu sema kwa January anaweza kukaa Dr. Diodorus ambaye amepata uzoefu mkubwa sana ila yote ni mema.
 
Wakati huu ambapo tunasubiri baraza jipya la mawaziri ambalo kama alivyoahiti rais litakuwa dogo lakini lenye utendaji uliotukuka, ni vizuri wananchi na wataalamu mbbali mbali wakapendekeza kufutwa au kuunganishwa kwa baadhi ya wizara. Mimi napendekeza ifuatavyo:

1. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ifutwe badala yake iwe ni idara au kurugenzi chini ya wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa kimataifa,

2. Waziri asiyekuwa na wizara maalumu asiwepo kwani haieleweki anafanya kazi gani labda ni spy

3. Ofisi ya Rais na Makamu wa rais zinakuwa na mawaziri wengi ambao kwa ukweli hawana tija. Mfano waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora mimi sioni haja awepo au waziri wa nchi ofisi ya rais mazingira. Mambo ya mazingira yangeenda huko kwenye kilimo

4. Wizara ya Elimu kwa sasa sijui ina kazi gani kwani masuala ya elimu sasa yanashughulikiwa na ofisi ya waziri mkuu chini ya Tamisemi yaani Tawala za mikoa na serikali za mitaa. Mimi naona hapa kuna haja ya kuangalia haiwezekani jambo moja linashughulikiwa na wizara mbili zikiwa na mawaziri na manaibu mawaziri zaidi ya wawili

5. Kuna wizara bubu ambazo hazina tija yoyote kwa wananchi kama wizara ya kazi na wizara ya habari, utamaduni vijana na michezo. Wizara hizi ingekuwa vema zikaunganishwa kwani kwakweli hazina mshike mshike wowote kwa maisha ya watanzania na mawaziri wake ni kula kulala tu

6. Manaibu mawaziri wapunguzwe baadhi ya wizara zina manaibu wawili kama wizara ya fedha

7. Kama tungekuwa na katiba nzuri mojawapo kati ya waziri mkuu au makamu wa rais ingebidi asiwepo. Kwa Tanzania ukitoka rais anayeonekana kiutendaji ni waziri mkuu tu makamu wa rais ni kama yupo yupo tu ndio maana yule mzee walikuwa wanamwita mzee wa mikasi kutokana na kufanya kazi za kukata tepe kufungua au kuzindua majengo au semina mbali mbali hivyo kazi yake hasa kama makamu wa rais huwa haionekani na ndio maana hana cha kuwajibika nacho.

Mimi naona tunahitaji wizara chache za muhimu kuliko kujaza mawizara ya kupeana vyeo tu. Hayo ni maoni yangu. Maoni yako ni yapi?
 
Hapo ndipo tutakuamini kweli unataka mabadiliko. Utakuwa unamuonea Mama Tibaijuka kwa kutomuinua mkono na kumnadi wakati wa kampeni iwapo itawapa uwaziri wale wengine waliofaidika na hela hizo hizo za escrow kupitia benki ya Stanbic.

Nina hakika ukiitaka hiyo orodha ya wanufaika wa escrow kupitia Stanbic utaipata mara moja.
 
mh pombe nchi ya china ni ya kwanza duniani kwa kuzalisha umeme . zaidi ya 60% ya umeme huo unatoka na makaa ya mawe. tujenge mitambo mingi ya umeme wa makaa huko njombe, mbeya na ruvuma. hatuwezi kuwwa nchi ya viwanda bila umeme. malaysia inawatu 30m na eneo 1/3 ya letu lakini wanazalisha 29,000MW sisi hatufiki hata 2000MW!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom