Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Chonde chonde kwa jinsi navyojua watu wema wanashughulikiwa na mfumo ambao by and large umeota mizizi kwa mwendo huu ulinzi wa rais na whistle blowers uongezwe maradufu.Madudu ni mengi
 
Chonde chonde kwa jinsi navyojua watu wema wanashughulikiwa na mfumo ambao by and large umeota mizizi kwa mwendo huu ulinzi wa rais na whistle blowers uongezwe maradufu.Madudu ni mengi.Mungu amlinde Rais wetu na wafichua maovu
 
Katibu mkuu wizara ya Uchukuzi ametoa ahadi hewa kwa uwongozi wa PPF kuhusu malipo ya madai ya wastaafu wa ATCL. PPF ilishitaki uwongozi wa ATCL mahakamani kwa kutopeleka makato ya michango ya wastaafu hao wakati wakiwa kazini. PPF walishinda kesi na kuamriwa kukamata mali za ATCL na kuziuza ili kuwalipa wastaafu hao. ATCL walipeleka amri hiyo wizara mama ya Uchukuzi ambako Katibu mkuu wake alikwenda kuonana na uwongozi wa PPF na kuahidi kuwa angelipa madai hayo kabla mwisho wa mwezi March,2015. Had sasa hakuna alicholipa na PPF wanasema wanasubiri pesa japo amri ya kukamata mali wanayo. Hivi ndivyo watendaji wakuu wanavyo dharau amri za mahakama kwa kulindana na kuacha wanyonge wakitabika.Wastaafu hawa wengine walistaafu toka 2010 na wengine wamefariki na waliopo hawajui watalipwa lini na kama kutakuwa na arrears
Tunamuomba raisi awasaidie wazee hawa kwani watendaji wakuu wanalinda maslahi yao tuu.
 
Naunga mkono hoja.

- Tena ikiwezekana awe anapata taarifa kutoka kwenye social media zote hasa kwa mambo yanayoligusa Taifa moja kwa moja Kama haya maufisadi na mauwizi, matumizi mabaya ya madaraka, huduma mbovu kwa wananchi nk

- Awe na simu maalum yenye whatsup ili wananchi wamtumie mambo wanayoyaona ni kero za muda mrefu, pia itumike Kama whistle blower.

- Afungue account kwenye social media zote kwa jina la ikulu

Mwisho vijana wake wawe wanaandika ripoti kila siku na kumkabidhi. Yale wanayoona ni more serious yapewe kipaumbele na kushughulikia haraka kwa kufanya uchunguzi zaidi.

Confidentiality kwa watoa habari iwe guaranteed.

Queen Esther

 
Furaha yangu sio ushindi wa CCM ... Ni ushindi wa Mgalatia .... Katika vipindi vinne ya taasisi ya uraisi watz tumeshuhudia Wavaa njiwa na wapiga soga mkiharibu nchi yetu, safari hii kaingia tena mwenye UCHUNGU na Tanganyika...... Mtaisoma namba.

By FaizaFoxy

Hongera sana.

Huko hunipeleki kwa sasa. Nnaiheshimu sheria ya mtandao ya kutoeneza chuki za kidini kama ufanyavyo.

Hatum-judge mtu kwa dini yake tunam-judge mtu kwa vitendo vyake.
 
Haaaa umeanza lini kuwakubali wagalatia?

Safari hii lazima mnyooke wavaaa kininja  Mlizoe vibaya sana na Kichwa Maji wa Msoga

By FaizaFoxy

Hongera sana.

Huko hunipeleki kwa sasa. Nnaiheshimu sheria ya mtandao ya kutoeneza chuki za kidini kama ufanyavyo.

Hatum-judge mtu kwa dini yake tunam-judge mtu kwa vitendo vyake.
 
By FaizaFoxy

Hongera sana.

Huko hunipeleki kwa sasa. Nnaiheshimu sheria ya mtandao ya kutoeneza chuki za kidini kama ufanyavyo.

Hatum-judge mtu kwa dini yake tunam-judge mtu kwa vitendo vyake.

Umeanza lini hiyo tabia ya kujaj mtu kwa matendo na siyo Dini yake ...ajuza usiye na haya
 
Umeanza lini hiyo tabia ya kujaj mtu kwa matendo na siyo Dini yake ...ajuza usiye na haya

By FaizaFoxy

Hongera sana.

Huko hunipeleki kwa sasa. Nnaiheshimu sheria ya mtandao ya kutoeneza chuki za kidini kama ufanyavyo.

Hatum-judge mtu kwa dini yake tunam-judge mtu kwa vitendo vyake.
 
Hatupokei ushauri wa chadema.asante
Mjinga mkubwa wewe!CCM kwa ushabiki wenu wa kijinga ndio mmeifikisha nchi hapa kwani nyie hata angepitishwa Assumpter mmengempa kura tu.

Hizi jitihada za Magufuli zimechangiwa na wana-UKAWA kuikataa CCM kwa kiasi kikubwa na pia kitendo cha yeye kuzomewa kwenye kampeni nacho kimemuuma sana.

Ukweli ni kwamba hamkustahiri kurudi madarakani na ushahidi mzuri ni pamoja na hali mbaya pale Muhimbili kama picha jinsi zile picha zilivyoonyesha.

Nyie mliokuwa mnashabikia CCM pamoja na madudu haya ndio mmepelekea wanachi kuteseka kwani mliwafanya viongozi wa CCM kutotambua makosa yao.

Kwa kifupi Magufuli anawaumbua nyinyi mliokuwa mnashabikia CCM kwani hata kama angepitishwa mtu tofauti na Magufuli bado mmengemchagua tu na mmengeendelea kuimba CCM ili hali huduma za kijamii ni mbovu kiasi hichi.Ingekuwa ni nchi za wenzetu hata huyu Magufuli asingepata nafasi hiyo kwani CCM kwa ujumla wake ilishastahili kutoka madarakani siku nyingi ila mnapeta kwasababu ya ujinga wa watanzania tu.

Ovyo kabisa nyie watu msiojua thamani na umuhimu wa opposition licha ya uozo wote huu.
 

Thank you, for recognizing the President!
 
Sioni vibaya hata mtu akichelewa kuzinduka; karibu Salary...
Unadhani wote tungekuwa na akili za kuipigia makofi CCM kama nyinyi huyo Magufui angeakuwa na hii kasi?

Unadhani bila Magufuli kuzomewa kwenye kampeni angeshutuka?

Jiulize mbona alipokuwa waziri hii kasi ya leo haikuwepo?

Jiuluze kama upinzani ungekuwa na nguvu uliyonayo leo hii Magufuli na wenzake serikalini wangejimilikisha nyumba za serikali?

Unadhani Magufuli angebadilika kama wote tungeimba CCM?

Kwa akili zenu hata kama CCM ingempitisha mtu tofauti na Magufuli mmengacha kuipa kura?

Hata kama Ukawa ingemsimsmisha mtu tofauti na Lowassa wewe ungeipa kura ukawa?

Acheni ujinga wenu na hata huyu Magufuli bado tunaendelea kumuangali na akibadilika na sisi tunambadilikia ingawa nyinyi naamini hata akija kuzembea mtaendelea tu kumpigia makofi kisa katoka CCM.

We unashangaza sana!
 
Mheshimiwa rais nimewasiliana na wewe kupitia Jamiiforums kwa vile sina njia nyingine ambayo ningeweza kufanya hivyo.Hata hivyo kama utaipata taarifa hii,naomba uichukulie kama kilio halali cha wazee waliostahafu waliokuwa katika mashirika mawili dada na kaka ya TARO(Tanzania Agriculture Research Organization) na TALIRO(Tanzania Livestock Research Organization)

Mashirika haya mawili yaliundwa kwa pamoja mnamo tarehe 01/07/1982 kwa nia ya kuongeza ufanisi kwa kuwahamisha wafanyakazi wa kitengo cha utafiti wa iliyokuwa Wizara ya Kilimo na Mifugo wakati huo na kuwapeleka kwenye mashirika hayo mawili.Hata hivyo mnamo tarehe 26/06/1991 mashirika hayo yalivunjwa na wafanyakazi wote wakarudishwa Wizarani.

Kwa bahati mbaya makato ya wafanyakazi hao kwa ajili ya malipo ya pension zao hayakupelekwa mahali stahiki katika kipindi chote walichokuwa katika mashirika hayo.Tendo hili ambalo ni kosa la jinai,lilisababisha wafanyakazi waliokuwa katika mashirika hayo kukosa haki za malipo ya uzeeni ya kipindi tajwa mara walipostahafu.

Kwa vile haikuwa kosa lao kutopeleka michango,naiomba serikali kupitia wewe ndugu rais ifikirie sasa kuwalipa haki yao ambayo wamenyimwa kwa muda mrefu.

Nimefanya hivi ndugu rais kwa kuwa wafanyakazi hawa wamekuwa wakipewa ahadi zisizotekelezeka kwa muda mrefu sana.Naamini pia kwamba taifa linalodhulumu watu wake hususan watoto na wazee linaingia kwenye laana.Kwa vile wastahafu walionyimwa haki hizi sio nyingi,naomba tusilifikishe taifa letu huko Ndg.Rais.


Ndugu Rais nakutakia kila la heri katika kuijenga Tanzania mpya ambayo naamini kila Mtanzania ana hamu ya kuishuhudia.
 
Nitamdhalau Mh Magufuli nikwaon hao makada wakiteuliwa kuwa mawaziri. Dhamana uliyopewa na chama chako hoi ni kubwa, 2020 sio mbali
 
Nitamdhalau Mh Magufuli nikwaon hao makada wakiteuliwa kuwa mawaziri. Dhamana uliyopewa na chama chako hoi ni kubwa, 2020 sio mbali

Ndani ya Chama, Makamba ni senior kwa Mh Magufuli fahamu hilo
 
Nitamdhalau Mh Magufuli nikwaon hao makada wakiteuliwa kuwa mawaziri. Dhamana uliyopewa na chama chako hoi ni kubwa, 2020 sio mbali

wewe ni miongoni mwa kura zilizoharibika, 2020 huna impact yoyote!
 
Nitamdhalau Mh Magufuli nikwaon hao makada wakiteuliwa kuwa mawaziri. Dhamana uliyopewa na chama chako hoi ni kubwa, 2020 sio mbali

Makamba likey kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.Ila Ghasia sijui.hata Ubunge huwa anapitaje,ila waweza shangaa ana kuwa waziri,yule mama sijui ana kadude gani ka mvuto maana utawala wa Kikwete hajacheza nje ya uwaziri japo alikuwa anapingwa sana
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…