Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mughwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.

Thread ndo nini? Andika kiswahili
 
Thread ndo nini? Andika kiswahili

Hiyo imeongezewa na moderator alipoamua kuifanya hivyo usomavyo. Mimi maandiko yangu yanaanzia para ya pili.

Wacha kiherehere. JF yenyewe haipo kwa Kiswahili.
 
Hiyo imeongezewa na moderator alipoamua kuifanya hivyo usomavyo. Mimi maandiko yangu yanaanzia para ya pili.

Wacha kiherehere. JF yenyewe haipo kwa Kiswahili.

Mi naomba mh.waziri amulike.wizara ya ardhi imekubuhu kwa rushwa yaani unalipia hati zaidi ya mil2 na bado inachukua years kuipata...aanze nayo
 
Pole na majukumu.

Mheshimiwa rais, binafsi nimefarijika na utendaji wako kwa muda huu mchache ukiwa madarakani. Ushauri wangu kwako naona itakuwa ni vyema kwako ukaanzisha account kwenye mitandao ya kijamii na iwe wazi kwa wananchi ili upate yanayojiri na ushauri pia kutoka kwa wananchi wako. Binafsi naona hili litakusaidia kujua watendaji wako walivyo na nini wananchi wanahitaji au nini kifanyike ili kutatua watatizo yao.

Asante.
 
>Kwa: Rais J.Magufuli

>Kutoka: Mungu Aliye Hai

>Kupitia: Mch.Emmanuel

>Yah: Chanels Zote Za Ndani Kuonyeshwa Bure Kwny Ving'amuzi.

Kutokana Na Teknolojia Kwenda Mbele Zaidi Kuliko Hali Ya Mwananchi Kwa Siku, Hii Imepelekea Wananchi Wengi Kukosa Uhuru Wa Kupata Habari Kutokana Na Mfumo Mpya Wa Ving'amuzi. Ambao Umefanya Watanzania Wanunue Kuwa Fedha Ili Kupata Hotuba Ya Rais, Kufuatilia Mikutano Ya Bunge nk.

Hivyo Ninakupa Ushauri Niliopewa Na Mungu, Kuwa Unaweza Kuamuru Makampuni Ya Ving'amuzi Kuonyesha Bure Chaneli Zote Za Ndani, Ili Watanzania Waweze Kupata Taarifa Ya Nchi Yao Kama Katiba Inavyosema.

Nimewasilisha Kwa Jina La Yesu Kristo.Amen
 
Ujinga wapi hii nchi inaendeshwa na kodi so msitake kujifanya wehu
 
Unahisi wao watapata wapi fedha za kuendesha hizo tv?
Unadhani matangazo pekee yanatosha kuendesha tv?
Unajua kwa mwaka wanalipia shilingi ngapi matangazo yao kwenda hewani?
Kama kupeleka matangazo hewani tu, star times wanachukua over million 400. Bila kuwa na subscription fee tv itarudishake hiyo fedha?
 
>Kwa: Rais J.Magufuli

>Kutoka: Mungu Aliye Hai

>Kupitia: Mch.Emmanuel

>Yah: Chanels Zote Za Ndani Kuonyeshwa Bure Kwny Ving'amuzi.

Kutokana Na Teknolojia Kwenda Mbele Zaidi Kuliko Hali Ya Mwananchi Kwa Siku, Hii Imepelekea Wananchi Wengi Kukosa Uhuru Wa Kupata Habari Kutokana Na Mfumo Mpya Wa Ving'amuzi. Ambao Umefanya Watanzania Wanunue Kuwa Fedha Ili Kupata Hotuba Ya Rais, Kufuatilia Mikutano Ya Bunge nk.

Hivyo Ninakupa Ushauri Niliopewa Na Mungu, Kuwa Unaweza Kuamuru Makampuni Ya Ving'amuzi Kuonyesha Bure Chaneli Zote Za Ndani, Ili Watanzania Waweze Kupata Taarifa Ya Nchi Yao Kama Katiba Inavyosema.

Nimewasilisha Kwa Jina La Yesu Kristo.Amen

ni sawa na linawezekana mbona ila nafisadi hayatakubali
 
Unahisi wao watapata wapi fedha za kuendesha hizo tv?
Unadhani matangazo pekee yanatosha kuendesha tv?
Unajua kwa mwaka wanalipia shilingi ngapi matangazo yao kwenda hewani?
Kama kupeleka matangazo hewani tu, star times wanachukua over million 400. Bila kuwa na subscription fee tv itarudishake hiyo fedha?

Chanel za ndani ni lazima zioneshwe bure..huo ndo mkataba ulofikiwa na serikali baina yake na watoa huduma ya ving'amuzi kipindi wanahamia digitali..tatizo ni usimamizi tu
 
Unahisi wao watapata wapi fedha za kuendesha hizo tv?
Unadhani matangazo pekee yanatosha kuendesha tv?
Unajua kwa mwaka wanalipia shilingi ngapi matangazo yao kwenda hewani?
Kama kupeleka matangazo hewani tu, star times wanachukua over million 400. Bila kuwa na subscription fee tv itarudishake hiyo fedha?

Kabisa,wabongo tunapenda sana kubwabwaja,magufuli ajikite kwenye mambo ya msingi kuliko haya anayoleta mtoa mada,azam,ting,*times zote zina free local channel.Tunataka magufuli aboreshe sector ya afya,elimu,miundombinu,uwajibikaji wafanyakazi sector ya umma etc.
 
Hiyo imeongezewa na moderator alipoamua kuifanya hivyo usomavyo. Mimi maandiko yangu yanaanzia para ya pili.

Wacha kiherehere. JF yenyewe haipo kwa Kiswahili.

Kweli kile kidude kinakuwasha, achana na mabishano usiku mhudumie mume. Au unpm tuchat kwenye whatsp nikusaidie dear enhee??
 
Nampongeza Rais Magufuli kwa uchapakazi wake alioonesha hata watumishi wa umma wameacha business as usual na kuchapa kazi kwa kwenda mbele.Kwa hili hata wafuasi wa ukawa nao wameanza kumuunga mkono kimyakimya.
 
Sasa hivi kilo ya nyama kwa baadhi ya maeneo nni sh 10,000, hiyo Muhimbili ambayo mkurugenzi anasimamishwa kazi tumeshuhudia Mara nyingi sana Madactari wakigoma kwasababu ya mishahara duni, je amefanyaje kuboresha mishahara ili kuwapa moyo wa kufanya kazi?

Tunashudia wanafunzi wa elimu ya juu wakihangaika bodi ya mikopo je anawahakikishiaje kupata hiyo mikopo?

Wafanya biashara wadogo wadogo bado hawana maeneo rafiki ya kufanyia kazi zao hili nalo anasemaje?

Madeni ya waalimu na mishahara yao vipi? mwaka wa masomo ndo unakaribia kuanza hivyo

Wafanyakazi wa serikalini kwa ujumla hasa wale wa ngazi za chini vipi maboresho ya mishahara yao ili wafanye kazi kwa ari?

Mi ninachokiona ni watu kukimbilia maofisini asubuhi asubuhi kwa sababu ya hofu alafu watakaa maofisini na kuchezea laptops wakifanya kazi kidogo ilimradi yupo na muda unaenda...

Ushauri kwa Mr Raisi naomba aboreshe kwanza mazingira ya kazi yawe rafiki kwa watendaji wake, wawe na morally ya kufanya kazi hapo hata usimamizi utakua rahisi

"Punda mwenye njaa ukimpiga sana ili aongeze mwendo na mzigo, mwisho wake atakaa chini" mpe majani na maji ashibe hutamchapa bali utafanya kazi ya kumzuia asikimbie sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom