Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
January. Hamisi kigwangala, Mwigulu...list ya wanaojpendekeza ni ndefu sana
Ianze kwanza Ikulu ihamishiwe Dodoma,,,aanze kuonesha mfano kwa kuhamia rasmi dodoma
Sio siri kuwa CCM ni chama kilicholea na kuhifadhi ufisadi nchini.
Kupata mtu mwadilifu ndani ya CCM ni sawa na kocha kutafuta wachezaji wa kusajili MOI.
Chama kilihangaika kumpata mgombea urais mwadilifu kikakosa kikabidi kumpata mwenye nafuu kidogo,na kumnadi kwa pesa nyingi za kukufuru, na kufanikuwa kumchagulusha.
Sasa tujiulize huyo waziri mkuu na mawaziri wasio na kashfa ndani ya chama chetu watapatikanaje?
Nimesikia majina yanatajwatajwa lakini yote yana madoa ya ufisadi. Subiri wateuliwe uone jinsi watu watakavyoanza kuweka hadharani madudu yao.
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.
Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mughwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.
Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.
Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.
Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.