Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Bado mapema sana kijana. Unakumbuka 1985 wakati wa serikali ya awamu ya pili?. Au ulikuwa mdogo?... alianza na "fagio la chuma baadae ikawa rukhsa"
 
Bado mapema sana kijana. Unakumbuka 1985 wakati wa serikali ya awamu ya pili?. Au ulikuwa mdogo?... alianza na "fagio la chuma baadae ikawa rukhsa"

Wewe unachofanya hapa ni kufuru.

Humpendi mtukufu rais wetu mpendwa chaguo la mungu na allah mheshimiwa Joni Pombe Josefu Magufuli.

Utakufa na kijiba cha roho.
 
Wewe unachofanya hapa ni kufuru.

Humpendi mtukufu rais wetu mpenda chaguo la mungu na allah mheshimiwa Joni Pombe Josefu Magufuli.

Utakufa na kijiba cha roho.

Hahahaaa
kweli kabisa hiki 'kijiba cha roho' kitaua wengi sana
 
Bado mapema sana kijana. Unakumbuka 1985 wakati wa serikali ya awamu ya pili?. Au ulikuwa mdogo?... alianza na "fagio la chuma baadae ikawa rukhsa"

Historia inatuonyesha kuwa marais wote walioingia madarakani baada ya Mwl Nyerere, mwanzoni wote walijifanya ni viongozi na watetezi wa walalahoi, kila mtu akiingia na kauli mbiu yake kuanzia "fagio la chuma", "Ukweli na uwazi" na "maisha bora kwa kila mtanzania" kwa kibwagizo cha "ari mpya", kasi mpya" na "nguvu mpya" Lakini vyote viligeuka kuwa kinyume, fagio la chuma likawa "ruksa," Ukweli na uwazi ukawa "kuvidhibiti vyombo vya habari na kusaini mikataba ya siri na wawekezaji", maisha bora kwa kila mtanzania yamekuwa "maisha machungu kwa kila mtanzania". Hicho kibwagizo cha ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya, "ndio kimeondoa kabisa ari, kikapunguza kasi na kunyong'onyesha watu badala ya kuwatia nguvu" Na kibaya na kutia aibu zaidi "Wote watatu wameondoka madarakani wakiwa ni mafisadi wakubwa'' Ni mapema mno kumjaji Mr JPM kwa vile bado hajaijua sukari ya Ikulu. Hajakutana na smart guys wanaojua kumsomesha mtu akasomesheka. Hakuna binadamu chini ya jua aliyetegemea Mr Ben Mkapa "Mr Clean" angeondoka madarakani akiwa kajilimbikizia mali na kutumia madaraka yake vibaya pamoja na kuaminiwa kuwa alikuwa mfuasi mzuri wa Mwalimu JK. Chezea Ikulu wewe!!!
 
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge mteule wa Kigoma Mjini ametumia msemo wa kiongozi wa zamani wa Burkina Faso Hayati Thomas Sankara kuwa huwezi kufanya mabadiliko makubwa bila kuchukua maamuzi magumu (?You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness?).
Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Zitto ameoredhesha mambo kumi ambayo anadhani kama yatafanyiwa kazi basi mabadiliko halisi yatapatikana.
I. Mikataba yote ya rasilimali za nchi iwekwe wazi.
II. Posho za vikao(Sitting allowance) katika mfumo mzima wa Serikali zifutwe kama Mpango wa maendeleo unavyotaka.
III. Tiketi za ndege za daraja la juu(Business Class) Kwa watendaji wa Serikali na wanasiasa zifutwe isipokuwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
IV. Kufuta Serikalini matumizi ya magari ya bei ghali(mashangingi) akitolea mfano wa Benki Kuu kutotumia magari ya aina hiyo.
V. Uingizaji wa Sukari kutoka nje ufutwe badala yake kuanzishwe miradi ya miwa ili kuweza kuzalisha sukari ya kutosha hapa nchini na kuiuza nje.
VI. Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha nje ya nchi iwekwe wazi na kufunguliwe mashtaka Kwa wahusika mara moja.
VII. TAKUKURU ipewe mamlaka ya kukamata na kushtaki na kila mwenye mali athibitishe ameipataje.
VIII. Mali na madeni ya viongozi yawe wazi Kwa UMMA na wananchi waruhusiwe kuhoji.
IX. Mshindi wa uchaguzi Zanzibar atangazwe na Serikali iliyoko madarakani iwe tayari kufanya nae kazi.
X. Mchakato wa Katiba ufanyike upya kwa kuanzia ilipoishia Tume ya Jaji Warioba.
Haya ni maoni ya Mh Zitto Kabwe kiongozi wa ACT-Wazalendo ambayo anadhani kama yatatekelezwa basi mabadiliko yatatokea.

 

Attachments

  • zittooo.jpg
    24.2 KB · Views: 415
Ninakubaliana na Zitto kwa 100% kuhusu hili,naamini Dr Magufuli atayafanya hayo.
 
Asimfundishe rais kazi, anatafuta KICK, ili aje kutamba kwamba yeye ndo kamwambia au?
 
Why call this madness?? Kwa nchi maskini kama zetu, hicho ndicho kitu sahihi cha kufanya...!!!
 
Well, mawazo mazuri haya. Kama alikuwa hana kwenye list yake basi atapata zuri nakuona uwezekano wake. Kuna baadhi ya wabunge wao ni kutetea maslahi yao binafsi lakin wengne wanakuwa katikati, thafi thana!
 
Ninakubaliana na Zitto kwa 100% kuhusu hili,naamini Dr Magufuli atayafanya hayo.
Yapo na mengine mengi tu, mimi nitataja moja. Pesa wanayochukua wabunge kama mikopo ya magari na pesa ya mafuta ifutwe mara moja. Watumie magari ya serikali, wakimaliza ubunge wao magari yatatumika kwenye idara zenye uhitaji.
 
Zitto huijui Ccm vizuri !!!!

Kwenye Kampeni
Magufuli huyu alimponda Lowassa huyu akisema

Maamuzi Magumu hata jambazi anafanya!!!

Mtasubiri sana Ccm Ni ile ile
 
Nafikiri uzi wa Ushauri wa zitto usingeunganishwa Hapa ungeachwa uendelee watu wajadili mawazo ya zitto kama ni valid. UshaurI tu KWA MODS Cookie, Mhariri, Active, Moderator.
 
Binafsi namshauri angeanza na Bodi ya TRC na DG wake.

Kisha nahamia TRA, Bodi na Management yake pamoja na maswahiba wote wa HOME SHOPPING CENTRE

Kisha ahamie kwa huyo jamaa wa TPDC ambaye anaitia harasa serikali kwa kila mwezi si chini ya dola 70,000 na misafara ya kwenda kwa familia yake USA.

Feel free kuongeza list mpaka ijae
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…