Naunga mkono wazo la mtoa mada. Utakuta baadhi ya wakuu wa mkoa/wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri wa mikoa ya pembezoni hawataki kutumia usafiri wa ndege wakati wanaitwa kwenye majukumu aidha Dodoma au Dar! Utakuta shangingi linaburuzwa mfano toka Kigoma hadi huko kwa pesa nyingi sana. Kuna pesa za mafuta, posho ya dreva,posho ya RC,DC,RAS,DED na pesa zingine za dharura! Ukipiga hesabu ni bora kutumia usafiri wa ndege! Kama hiyo haitoshi, magari hayo kila mwezi lazima yaende service utake, usitake! Matokeo yake, mashangingi mengi yameharibika kwa kipindi kifupi mno na hivyo kusababisha hasara kwa Taifa!