Wengi wetu tumeguswa na jinsi ulivyoanza kazi, all we can say is KUDO'S.
Kinachofuatia ambacho wengi tungependa kukiona, na ambacho ni rahisi sana kuonekana na kuacha alama ya kumbukumbu, ni hizi Shangingi zilizojaa mjini, kwakweli kwa wengi zinatuumiza kuona matumizi yake yasivyokua na ulazima sana hata kwa watu ambao si lazima sana kuzitumia kwani zinanyonya hazina yetu bila kua na impact yoyote.
Kwakweli gharama za kuzihudumia hata kuzinunua ni juu sana na badala yake, sisi wanyonge tunashauri magari mengine yasiyo ya anasa sana wapewe hawa wakubwa zetu hawa ili watutumike vyema.
Mkuu Magufuli kuna hizi Rav 4 hizi ama hata toyota harrier kwa wale wakuu kabisa zitawatosha kabisa walau tusave pesa watoto waende shule na tupate vitanda mahospitalini.
Wengi wetu, tunahamu kuziona hizi shangingi hizi zikifutika hapa mjini, hakuna haja ya kuishi maisha ya anasa namna hii wakati wengi wetu mlo wa siku ni wa mashaka.
Asante mkuu Magufuli, natanguliza shukrani.