Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Ninaposema siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa ni wajuzi wa kuteka akili za watu huku wakifukia mambo muhimu, baadhi husema sipendi maendeleo ya viongozi hasa Mh Pombe..

Sasa nawauliza ni juzi tu tumesikia Mh Jk kakomba hazina yote, lakini pia sisi kama wadau tunaowaweka viongozi madarakani tuna haki ya kujua JK na Mkapa walivyopata mali zao,,

sasa je Mh Pombe atatusaidia kuwahoji jinsi walivyozipata ili tujue kua yeye ni kiongozi wetu na hayuko kwa ajili kulinda masilahi ya watu fulani?

Jf hii haifanani na kumteua mama Anna Mngwira kwenye serikali ya raisi Magufuli...acheni kuchomekea

we ni ------ wa nyuma dagaa wewee
 
Ni maufisadi na mauzembe zembe yaliyotishia nchi hii kuangukia mikononi mwa watu wa ovyo Kwa mtizamo wangu

Tayar tunaona rais anafanyia kazi mauzembe zembe kazini. Hili ni suala zuri.

Ufisadi kipind cha magufuli hautakuwa na nafas - naamini hivo. Lakini kuna uliofanyika tayar na ufisadi mwingine utaendelea kutukamua kwa miaka mingi ijayo kwa mfano kupitia mikataba mibovu

Hili litatatuka vipi? Tutatoka lini kwenye hii looping? Hii mikataba ipitiwe upya chini ya magufuli kama rais

Nchi ilikuwa inaenda ndivyo sivyo
 
Kwa jinsi foleni zilivyo mh tunaomba ziara zako za kushtukiza ukaanzie mikoani hapa utatulaumu bure kuhusu kuchelewa kazini na utendaji mbovu kazini maana nimekaa kwenye foleni masaa mawili nimeshachoka morali ya kazi naipata wapi?. Mtangulizi wako kakuachia nchi pabaya. Ukiendelea na ukali wako huu kazi utafanya peke yako.
Ondoa kwanza foleni ndio tulaumiane vizuri
 
Alishasema pale jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni kuwa atawalinda maraisi waliopita
 
Sio Mkapa na Kikwete peke yao wanaosemwa wamepata utajiri mkubwa kifisadi. Wengine wengi wanatajwa. Mfano chenge na lowasa

Sasa hapa tusiwalenge watu binafsi. Itakuwa na changamoto nyingi na ngumu

Kinachotakiwa kufanywa ni kuangalia mikataba na maufisadi yaliyotangazwa na ambayo hayajatangazwa.
 
Siku mbili tuu baada ya Magufuli kuingia madarakani ametembelea Muhimbili na kukuta mashine za CT Scan hazifanyi kazi na wagonjwa wanaambiwa waende hospitali binafsi kwa ajili ya kipimo hicho.

Kipimo hicho ni ghali sana kwa mwananchi wa kawaida hivyo wapo Watanzania wenzetu wengi wamepoteza maisha yao kwa kushindwa kumudu gharama hiyo katika kipindi cha utawala wa JK huku yeye na maofisa wake wakitumbua maisha kwa safari nyingi za nje, tafrija zisizo tija pale Magogoni na mambo mengi ya kifahari.

Tuliloshuhudia ni kuwa amri ya kutengeneza machine hizo ilipotolewa kwa ukali kesho yake mashine zinafanya kazi. Jee Rais mpya kaja na mafundi au fedha za kazi hiyo? Jibu ni hapana, fedha na mafundi wapo ila ni uzembe na udhaifu wa serikali iliyopita ndi chanzo cha raia wengi kupoteza maisha kwa kitu ambacho kinatengenezeka kwa siku moja.

Jee kuna mangapi yataendelea kufichuka kuhusu uzembe uliokuwa umekithiri serikalini? Je bado kuna haja ya kuendelea kumsifia JK kuwa ameendesha nchi vizuri kwa miaka 10 wakati kumbe ndugu zetu wengi wamepoteza maisha yao kwa uzembe mkubwa kiasi hicho?

ImageUploadedByJamiiForums1447306466.321516.jpg

Haya ndio yalikuwa yanapewa kipaumbele na kuambiwa kuwa Rais wetu ni mtu wa watu
 
Ni kweli jamaa alikua dhaifu sana.
But Mr ze "lager"ataturudishia heshima yetu.
 
Waliokuwa wanamsifia JK ni watumbuaji wakuu waliokuwa karibu naye.
 
Tumefika hapa tulipo kwa udhaifu wa Jk pamoja udhaifu wabunge wa ccm kuitetea serikali badala kuikosoa
 
Siamini kwamba ni Uzembe bali ni mpango ulioandaliwa makusudi ili hospitali binafsi ambazo wakubwa wana share or influency waweze kuneemeka. Inawezekana ilikuwa ni mpango wa kuwafanya wakubwa serikalini waweze kupata trip za kwenda nje kupimwa afya zao as if hata hizo hosp. za private hazina vifaa na madaktari.

Tusiseme uzembe tuseme ni uhujumu uchumi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom