Raisi JPM kwa mujibu wa tume amepata kura kama milioni 8 na zaidi. Hizi kura ni za watanzania.
Tungependekeza Raisi akaunda Serikali ya watanzania kwa maana siyo serikali ya CCM. hayo ndiyo mabadiliko ya kweli.
Kuanzaia Bunge spika CCM naibu upinzani na wajivue uwanachama wa vyama vyawo
Taasisi zote za vyombo vyadola wasiwe wanachama wachama chochote
Vyombo vya dola ni Mahkama , Takakuru, Usalama wataifa, Jeshi la ulinzi, Polisi , vyombo vya sharia, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu wa wizara na wote wengine.
Wakurugenzi asichague yeye wacha bodi ya utumishi iwa chague kwa mujibu wa CV zao.
Mheshimiwa wacha mihimili ya taifa viwe huru .
Kumuingiza Dk Tulia na kumpa unaibu spika ni kulidhibiti bunge.
Inavytakikana hawa wote wawe hawana chama na wafanye kazi bila ya utashi wa siasa.
Mheshimiwa Magufuli lete mageuzi ya kweli.
Ukiwa na wana CCM kila pahala mambo yale yale. kama nyumba inavuja utahama kila chumba na utahamisha kila kitu nyumba itabaki kuvuja. Chakufanya weka paa jingine jipya.