Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.

Hana analojua achana nae
 

Wewe unashangaa leo?
hio ndio kazi ya upinzani ni kupinga tu kila jambo,hapana kufikiri,liwe jema ama si jema ila kama anaetaka kulifanya ni CCM ni kupinga tu
 
Chanzo cha viwanda vingi kufa ni biashara huria, na kuingiza bidhaa nyingi toka njee ambazo nyingi zinapatikana hapa, kwa mfano nguo za mitumba, vitenge, viatu, juice, tairi za magari, karatasi za rim.

viongozi wetu walianza kufanya biashara zao binafsi za kuimport bidhaa zao na kuuwa viwanda vya nyumbani makusudi ili wapate mapato makubwa.

Tukiweza kudhibiti bidhaa toka nje hasa zile ambazo sisi tunaweza zalisha tutafufua viwanda vyetuu!!!
 

There is nothing to lose hata akishindwa kwani mpaka sasa waliopewa wameshindwa pia kwahiyo hapo ni win win situation , cha msingi apige kwanza hatua ya kwanza kuvichukua sio kumkatisha tamaa
 
Kuna wananchi wawili ambao kama Magufuli atawateua kuwa wabunge atajijengea heshima sana mbele ya jamii nao ni huyo mama mwenyekiti wa ACT Anna Mughwira na Kafulila. They will add value to the bunge proceedings na hilo ndio la muhimu!!

Umeearibu baada ya kusema neno kafulila ,huyu ameshaabadilika kitambo ,sio mpingaji wa ufisadi tena ,huyu ni anawanadi mafisadi papaa
 

Katika siku zote leo umeogea kitu, watendaji serikalini akili zao zimedodaa, zimelala, ni muda wa kuwabadilisha na kuweka wapya ambao ni creative kwa gharama yoyote, wanafunzi kufundishwa fani husika ya kiwanda hicho, hata course ya miaka miwili
 
Mimi namshauri Raisi ajiuzulu Kwani atapata Maadui wengi wa Hatari.... labda ajipe Moyo kama ule wa Mwakyembe maana yeye alisema alishaonja kifo... so haogopi mtu
 

Mkuu mfano wako ungekuwa wa viwanda ningekuelewa vizuri sana, tatizo umetoa mfano wa shirika la umma kama NHC, mi wasiwasi wangu hauko ktk mashirika, wasiwasi wangu ni kwenye viwanda mkuu.
 

Seconded mkuu
 


You are right The Boss
Ila kuwanyang'anya acha tu wanyang'anywe coz wako baadhi ni kweli wamevikalia tu, wamefanya magodauni na wengine ni kweli wanafugia mbuzi

Acha tu viwe mikononi mwa serikali kama hatua ya kwanza, then hatua ya pili vitangazwe upya kwa wawekezaji, huwezi jua wanaweza kutokeza wawekezaji serious wakavichukua na kuvifufua.

Jambo la kuepuka ni kwa serikali kujiingiza kuendesha hivyo viwanda, itakuwa ni bonge la mistake
 
Pamoja na hayo mengi yaliyosemwa; Dr. Magufuli afute permanent employment, kuwa na ajira za mikataba tu hii itaongeza sana ufanisi wa wafanyakazi.
 
suala la elimu ya sec na advance walikosea sana kushusha viwango vya ufaulu na inatakiwa virudi kama awali.
 

Ulishindwa nini kumwambia haya JK. Tuliwaambia miaka 10 sio mingi sasa umeanza kulialia. Wacha JPM afanye kazi yake kama ulivyomwacha JK kutanua kwa pesa za walipa kodi, zamu yenu imekwisha.
 

Pamoja sana.
 

si bora ccm hatakama wamehangaika kumtafuta lakini walau wamechaguana wenyewe kama taasis imara .
sasa nyie mliosubiria makapi mkaaza kuyasafisha kwa nguvu zote
 
Ni bora mtu kama wewe uwe kaburini huenda kuoza kwa mwili wako kutarutubisha ardhi yetu ya Tanzania kuliko kuwa na mtu mwenye mawazo kama yako humu JF.
Hili ni dua au nini? Haya ni maoni yangu ambayo hayastahili kunihukumia kifo! Uungwana unatakiwa na uangalie kauli zako zisikurejelee. Ni lini hivyo viwanda vilitaifishwa mpaka lro tuwaze kuwa vinaweza kufufuliwa vikarejea katika hali yake iliyotakiwa? Bado nafikiri baadhi yake ni rahisi kujenga kiwanda kipya kuliko hata kugikiria kuvifufua.
 
Umemwelewa lakini au unahara tu,

Teknolojia tuliyonayo ni tofauti na wakati viwanda vinabinafsishwa ni bora kujenga vipya kwa teknolojia ya kisasa.

Ulichotakiwa wewe ni kutoa maoni yako kuanzia alipoishia badala ya kutoa matusi.
Wanaendeshwa na mihemuko, wakati mwingine unafikiria kuna chemechembe za chuki kuliko hekima!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…