Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
kauli yatu ya hapa kazi Bila mishahara mizuri, tena kwa walimu, mh. anajisumbua, ukizingatia michango imefutwa! like shule za msingi kutakufa vibaya sana
 
Iwekwe Sheria Kabsa Itakayokuwa Wazi Kwa Makampuni Yote, Kuonyesha Ulazima Wa Kuonyesha Free Kwa Chaneli Zote Za Ndani Ya Nchi, Yaani Tbc1, Itv, Startv, Chanel Ten, Eatv, Clouds Tu. Ambazo Ndo Zinatangaza Habari Za Hapa Nchini
 
Nikupongeze rMCBll Magufuli kwa mwanzo mzuri. umeonyesha dhamira ya dhati kwa kuwa mkweli na mpenda haki umeyasema waziwazi matatizo ya serikali ya CCM pasipo unafiki mengi ya hayo wapinzani waliyapigia kelele sana baadhi ya mambo hayo ni sheria ya manuzi ya umma, safari za rais na viongozi waandamizi serikalini nje yanchi, matumizi makubwa ya serikali,ukwepaji Jodi nk.

Wakati wanasema walibezwa sana na wabunge was CCM. Leo hoi wanakushangilia hivyo naomba jihadhali na unafiki huo.pili kama wapinzani waliwaliyaibua haya ambayo pia wewe unayapigia kelele wafanye wapinzani kuwa msaada kwako usikubali kuwaona ni mmadui bungeni walitoka kuogopa unafiki ambao pia umesema msema kweli ni mpenzi was mungu ni sahihi she in so rais was Zanzibar.

Tatu maendeleo yoyote katika nchi yanategemea sana haki na amani ya kweli na kukwepa laana toka kwa mungu,hakuna dhambi mbaya kama kumwaga damu isiyo na hatia damu hiyo hugeuka na kuwa laana, umesema tukuombee ni sawa ila naomba kemea polisi wasiue hivyo na kuwapiga raia. acha demokrasia ichukue mkondo wake nchi hii imegeuka kuwa adui wa wasema kweli na wanaharakati.

Vipo vifo vimeanza kutokea wakati wa utawla wako vyenye utata hivi vinaashiria giza katika uongzi na utawala wako kifo cha mwanasiasa mawazo kimezua utata baada ya kuuawa bado mazishi yanazuiwa na polisi hebu toa tamko angalau kulaani mauaji hayo, angalia kifo cha katibu wa madereva ili ufanikiwe tafadhari kemea kumwaga damu katika ardhi ya Tanzania isiyo na hatia.
 
kuna halimashauri ambazo zinakera na zinatia kichefuchefu kiutendaji,maendeleo duni,wapo wapo tu wanakula bata.

~Kishapu

~Sengerema

~Meatu

~Bunda

Ongezea na wewe ili magufuli alale nao mbele
 
kuna halimashauri ambazo zinakera na zinatia kichefuchefu kiutendaji,maendeleo duni,wapo wapo tu wanakula bata.

~Kishapu

~Sengerema

~Meatu

~Bunda

Ongezea na wewe ili magufuli alale nao mbele

Kishapu kudadekiiii zao na mbunge yule rofa hata hana tym na wapga kura wake.kudadekizo walikula hela bilion 80
 
NINA HAKI YA KUTOA MAONI KWA DR.JOHN POMBE MAGUFULI RAIS WA JMT AWAMU YA TANO.

Ninaomba kutoa angalizo kwa Mh.Dr.John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka 5 atakachokuwa akiongoza JMT.
1. Ni vyema akaepuka watu wachonganishi watakaomchonganisha na Watendaji wake kwa manufaa ya watu hao.Kwa kutumia vyombo vya dola na utashi wake kama Rais ni vyema akachuja kila taarifa atakayopewa kabla ya kuchukua maamuzi stahiki.Kama ilivyokuwa wakati wa Kampeni,watu wengi watajisogeza kwake kwa njia ya kumpa ushauri katika mambo mbalimbali.
2. Ni vyema akatafakari sana katika uteuzi wa Watendaji atakao ufanya maana hao ndio watakuwa wafuatiliaji wa shughuli zake za kila siku.Kama kuna mahalia mbapo JPM anapaswa kuwa makini ni katika teuzi mbalimbali atakazozifanya.Asifanye uteuzi wenye nia ya kulipa fadhila.Bali weledi na uchapakazi pamoja na uaminifu katika utendaji wa kazi.
3. Ni vyema JPM akashughulikia kwa moyo wake wote suala la Zanzibar kabla hali ya amani haijavurugika ZAIDI.Mshindi halali atangazwe na kazi iendelee.Imani kwamba CUF watavunja Muungano si ya kujenga na Imani kwamba CCM pekee ndiyo yenye kuleta amani na utulivu si hoja makini na jadidi.
4. Ni vyema akaweka mikakati thabiti ya kushughulikia ahadi lukuki alizoziahidi ili imani ya Wananchi kwake na kwa Chama chake irudi na Maisha ya Wananchi yawe bora zaidi.Watangilizi wake hawakutimiza ahadi zao lukuki walizotoa kwa mbwembwe majukwaani.
5. Ni vyema akaepuka kuongozwa na watangulizi wake ambao kwa nguvu kubwa walimbeba na kumweka madarakani.Akumbuke yeye ndiye rais wa JMT na watangulizi wake walikwisha maliza vipindi vyao.
6. Ni vyema akafanya kazi na makundi yote hususani vyama pinzani na wanaharakati wapenda maendeleo.Kushinda uchaguzi sio kushinda kila kitu.Hata walioshindwa wanaweza kupewa ushirikiano kwa ajli ya kuleta maendeleo yanayohitajika.
7. Ni vyema harakati za kufufua Viwanda vilivyokuwa vimebinafsishwa na kutelekezwa ama kubadilishwa kuwa magodauni ziendane na kuboresha upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme pamoja na kuondoa Michango lukuki inayoitwa ya kisheria katika Viwanda hivyo kama OSHA,FIRE RESCUE,NEMC,VIPIMO,MAJI,TBS,LESENI,CESS ZA VIJIJI,MITAA NA WILAYA,NK.Hizi zote huwa ni kero kwa Wenye viwanda.Pia ni vyema soko la ndani la bidhaa husika lilindwe kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa hizo zinauzwa na tija kupatikana.
8. Ni vyema akaondoa kabisa kodi katika pembejeo za kilimo kama matrekta, mbolea, powertiller, mbegu bora n.k.Jitihada za kuboresha sekta ya Kilimo ziwe za dhati na zenye tija na wala sio blah blah.
9. Ni vyema suala la Bunge kuwa la mipasho badala ya chombo cha kutunga sheria na kujadili matatizo ya wananchi likemewe kwa sauti kuu na yeye awe mfano bora wa kulisimamia hilo.Jambo baya katika hotuba yake alisisitiza hilo na papo hapo yeye mwenyewe akatoa mipasho kwa kuwaita wapinzani ?watoto?
10. Ajira kwa vijana ni bomu hatari.Ni lazima tatizo hili litatuliwe kwa jitihada kubwa kwa kufufua viwanda na kuimarisha kilimo sambamba na kukomesha ajira za upendeleo.
Haya ni maoni yangu binafsi, hata hivyo michango kwa wengine ni muhimu kwa nia ya kutupeleka katika maisha bora zaidi.Aidha kutofautiana mitizamo ni chanzo cha Maarifa mengine.
 
We ni nani mpaka umpokelee maoni rais?
Mleta hoja anatoa maoni yake kwa rais wake,wewe unayapokea kama mkewe au sekretari wake?
Mawazo ya kujenga kama hya yanakaribishwa kwa mikono miwili
 
Kwa kuongezea:
Pamoja na nia yake ya kuunda Baraza dogo la Mawaziri wachapa kazi kama alivyoliita, ila kihalisia Makatibu Wakuu wa Wizara ndio watendaji wakuu wa majukumu ya Wizara husika. Baada au hata kabla ya kuteua Mawaziri atangaze "Nafasi za kazi" ya "Ukatibu Mkuu & Naibu K/MKuu" ya Wizara alizokusudia kuziunda ili wa-Tanzania mbali mbali wenye sifa za kutosha waweze kuomba na kupitishwa kwenye "mchujo" ambao utamwezesha kupata watendaji wa kuendana na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tu"!!
 
Wanakwimba tuna malalamiko yaguatayo:-
a. Madawati kwa shule za msingi na sekondari hayatoshi.

b. Mgawanyo wa walimu ni upendeleo. Shule za mjini zina walimu wengi kuliko za vijijini

c. Barbara ya hungumalwa kwenda Maswa haipitiki na mvua zinazoendelea zitatuzuia kuchapa kazi.

D. Nyumba za walimu. Ukifanya ambush utatawahurumia hao walimu.

E. Afisa elimu wa sekondari bw kajanja amejaa ujanja ujanja

F. Tunaomba Maji baba na umeme. Vituo vya afya na ile m50!

Mh. Magufuli twaomba ututatulie hizo kero
 
Napenda kumpa heko mheshimiwa JPM kwa kuionyesha jamii hadi sasa ya kwamba matatizo ya watanzania yalitokana/yanatokana na watawala badala ya wananchi wenyewe kama tulivyojaribu kuaminishwa kabla. Kihulka,tuliambiwa watz ni wavivu na wanategemea maendeleo yawafuate bila kufanya kazi. Lakini mheshimiwa wa sasa ndani ya kipindi kifupi tu, kaonyesha ya kwamba matatizo ya kiuchumi ya wananchi yanauhusiano wa moja kwa moja na ulafi,choyo,na umimi wa watawala wetu.
Kutokana na kuanza vizuri na kukubalika kwa falsafa za magufuli tunaimani mambo mengi yatakwenda mbele kwa kasi ya kuvutia. Hivyo basi,ili aishi mioyoni mwa watz miaka nenda rudi, atuwekee sheria zitakazowabana viongozi wanaokuja nyuma yake ambao lengo lao la kuingia madarakani litakua kutafuta ukwasi na wala si maendeleo ya wananchi. Hasahasa kuondoa kinga ya kushitakiwa rais baada ya kutoka madarakani. Mfano mzuri ni huyu wa sasa na aliyepita wanaonekana kabisa wameharibu lakini hatuna la kuwafanya kwa mujibu wa sheria.
Nawakilisha wanajamvi..
 
Wanakwimba tuna malalamiko yaguatayo:-
a. Madawati kwa shule za msingi na sekondari hayatoshi.

b. Mgawanyo wa walimu ni upendeleo. Shule za mjini zina walimu wengi kuliko za vijijini

c. Barbara ya hungumalwa kwenda Maswa haipitiki na mvua zinazoendelea zitatuzuia kuchapa kazi.

D. Nyumba za walimu. Ukifanya ambush utatawahurumia hao walimu.

E. Afisa elimu wa sekondari bw kajanja amejaa ujanja ujanja

F. Tunaomba Maji baba na umeme. Vituo vya afya na ile m50!

Mh. Magufuli twaomba ututatulie hizo kero

wacha mambo ya kijinga, wewe hukai kwimba, maji kwimba yameshaletwa na moil, madawati hebu sena shule gani ambayo haina madawati? ulashakaririshwa madawati madawati mpumbavu mkubwa wewe.
 
wacha mambo ya kijinga, wewe hukai kwimba, maji kwimba yameshaletwa na moil, madawati hebu sena shule gani ambayo haina madawati? ulashakaririshwa madawati madawati mpumbavu mkubwa wewe.

acha jazba mkuu....yeye kajenga hoja na wewe jenga ya kwako kumpriempty....siyo matusi....its just a simple wisdom!
 
acha jazba mkuu....yeye kajenga hoja na wewe jenga ya kwako kumpriempty....siyo matusi....its just a simple wisdom!

nimemuuliza anitajie shule moja tu ambayo haina madawati nayanapungua mangapi ijumaa nipeleke. Moil yuko vizuri jimboni kwake asilete porojo.
 
nimemuuliza anitajie shule moja tu ambayo haina madawati nayanapungua mangapi ijumaa nipeleke. Moil yuko vizuri jimboni kwake asilete porojo.

kaka usibishe Shule ya Msingi Buyogo hawana madawati na kila Mwaka wanaazima Madawati kutoka Nela sekondari Kwa ajiri ya wanafunzi wa Darasa la saba kufanyia mitihani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom