Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Sijui kama unajua moja ya masharti ya kuuziwa kiwanda au shamba kutoka serikalini ni kuliendeleza bila kubadilisha matumizi.

Kweli wabaya wa hii nchi ni watanzania wenyewe.

Mkuu unataka serikali iache kuvifuatilia hivi viwanda na mashamba wajenge vingine?

Hana analojua achana nae
 
Wewe unashangaa leo?
hio ndio kazi ya upinzani ni kupinga tu kila jambo,hapana kufikiri,liwe jema ama si jema ila kama anaetaka kulifanya ni CCM ni kupinga tu
 
Chanzo cha viwanda vingi kufa ni biashara huria, na kuingiza bidhaa nyingi toka njee ambazo nyingi zinapatikana hapa, kwa mfano nguo za mitumba, vitenge, viatu, juice, tairi za magari, karatasi za rim.

viongozi wetu walianza kufanya biashara zao binafsi za kuimport bidhaa zao na kuuwa viwanda vya nyumbani makusudi ili wapate mapato makubwa.

Tukiweza kudhibiti bidhaa toka nje hasa zile ambazo sisi tunaweza zalisha tutafufua viwanda vyetuu!!!
 
Watu watamuingiza Magufuli bonge la mkenge
Why awanyan'ganye bila kuuliza nini kimewafanya washindwe?
je kina nani hao watakao pewa baada ya kunyang'anywa?

wata qualify vipi kupewa?

serikali ikiamua iviendeshe itaweza?
kwa miaka mingapi vitaweza leta faida?

huu mkenge ni mkubwa sana...time will tell....

There is nothing to lose hata akishindwa kwani mpaka sasa waliopewa wameshindwa pia kwahiyo hapo ni win win situation , cha msingi apige kwanza hatua ya kwanza kuvichukua sio kumkatisha tamaa
 
Kuna wananchi wawili ambao kama Magufuli atawateua kuwa wabunge atajijengea heshima sana mbele ya jamii nao ni huyo mama mwenyekiti wa ACT Anna Mughwira na Kafulila. They will add value to the bunge proceedings na hilo ndio la muhimu!!

Umeearibu baada ya kusema neno kafulila ,huyu ameshaabadilika kitambo ,sio mpingaji wa ufisadi tena ,huyu ni anawanadi mafisadi papaa
 
Shirika la nyumba la taifa (NHC) kwa data za December 2014 lilikuwa linaingiza Bilioni 9.763 kama wastani kila mwezi kama faida. Na ni shirika la umma hili 100%. Kabla hajaingia Mchechu...shirika hili hili lilikuwa likiendeshwa kwa hasara. Nafikiri unaelewa nini maana ya shirika kuendeshwa kwa hasara. Things have changed. Serikali inaweza kumiliki viwanda kwa kuajiri wataalamu kutoka sekta binafsi. Tatizo la hapa Tanzania....wale watu waliozoea sekta za umma ufanya kazi kwa mazoea sana...hivyo sio watu wa kuwatumia kwenye hivyo viwanda vitakavyoanzishwa. Ufumbuzi hapa ni kuchukua smart people kutoka sekta binafsi na kuwa absorb huku kwenye public sector...tutaona mabadiliko.

Katika siku zote leo umeogea kitu, watendaji serikalini akili zao zimedodaa, zimelala, ni muda wa kuwabadilisha na kuweka wapya ambao ni creative kwa gharama yoyote, wanafunzi kufundishwa fani husika ya kiwanda hicho, hata course ya miaka miwili
 
Mimi namshauri Raisi ajiuzulu Kwani atapata Maadui wengi wa Hatari.... labda ajipe Moyo kama ule wa Mwakyembe maana yeye alisema alishaonja kifo... so haogopi mtu
 
Shirika la nyumba la taifa (NHC) kwa data za December 2014 lilikuwa linaingiza Bilioni 9.763 kama wastani kila mwezi kama faida. Na ni shirika la umma hili 100%. Kabla hajaingia Mchechu...shirika hili hili lilikuwa likiendeshwa kwa hasara. Nafikiri unaelewa nini maana ya shirika kuendeshwa kwa hasara. Things have changed. Serikali inaweza kumiliki viwanda kwa kuajiri wataalamu kutoka sekta binafsi. Tatizo la hapa Tanzania....wale watu waliozoea sekta za umma ufanya kazi kwa mazoea sana...hivyo sio watu wa kuwatumia kwenye hivyo viwanda vitakavyoanzishwa. Ufumbuzi hapa ni kuchukua smart people kutoka sekta binafsi na kuwa absorb huku kwenye public sector...tutaona mabadiliko.

Mkuu mfano wako ungekuwa wa viwanda ningekuelewa vizuri sana, tatizo umetoa mfano wa shirika la umma kama NHC, mi wasiwasi wangu hauko ktk mashirika, wasiwasi wangu ni kwenye viwanda mkuu.
 
Naam, serikali isijiingize moja kwa moja kwenye biashara, nakubaliana na wewe 100%,kwa sasa duniani nadhani ni China pekee(yenye ujamaa wa kweli),ambapo serikali inafanya biashara. Kwa kuwa sisi Ujamaa wa kweli umetushinda basi viwanda viwe vya umma kupitia PPP au Kiundwe chombo chenye meno ambacho kitaratibu kwa ukaribu Viwanda vyote kwa niaba ya Serikali. Kazi kuu ya Serikali iwe kutoa huduma.

Seconded mkuu
 
Watu watamuingiza Magufuli bonge la mkenge
Why awanyan'ganye bila kuuliza nini kimewafanya washindwe?
je kina nani hao watakao pewa baada ya kunyang'anywa?

wata qualify vipi kupewa?

serikali ikiamua iviendeshe itaweza?
kwa miaka mingapi vitaweza leta faida?

huu mkenge ni mkubwa sana...time will tell....

You are right The Boss
Ila kuwanyang'anya acha tu wanyang'anywe coz wako baadhi ni kweli wamevikalia tu, wamefanya magodauni na wengine ni kweli wanafugia mbuzi

Acha tu viwe mikononi mwa serikali kama hatua ya kwanza, then hatua ya pili vitangazwe upya kwa wawekezaji, huwezi jua wanaweza kutokeza wawekezaji serious wakavichukua na kuvifufua.

Jambo la kuepuka ni kwa serikali kujiingiza kuendesha hivyo viwanda, itakuwa ni bonge la mistake
 
Pamoja na hayo mengi yaliyosemwa; Dr. Magufuli afute permanent employment, kuwa na ajira za mikataba tu hii itaongeza sana ufanisi wa wafanyakazi.
 
suala la elimu ya sec na advance walikosea sana kushusha viwango vya ufaulu na inatakiwa virudi kama awali.
 
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mghwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.

Ulishindwa nini kumwambia haya JK. Tuliwaambia miaka 10 sio mingi sasa umeanza kulialia. Wacha JPM afanye kazi yake kama ulivyomwacha JK kutanua kwa pesa za walipa kodi, zamu yenu imekwisha.
 
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mghwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.

Pamoja sana.
 
Sio siri kuwa CCM ni chama kilicholea na kuhifadhi ufisadi nchini.

Kupata mtu mwadilifu ndani ya CCM ni sawa na kocha kutafuta wachezaji wa kusajili MOI.

Chama kilihangaika kumpata mgombea urais mwadilifu kikakosa kikabidi kumpata mwenye nafuu kidogo,na kumnadi kwa pesa nyingi za kukufuru, na kufanikuwa kumchagulusha.

Sasa tujiulize huyo waziri mkuu na mawaziri wasio na kashfa ndani ya chama chetu watapatikanaje?

Nimesikia majina yanatajwatajwa lakini yote yana madoa ya ufisadi. Subiri wateuliwe uone jinsi watu watakavyoanza kuweka hadharani madudu yao.

si bora ccm hatakama wamehangaika kumtafuta lakini walau wamechaguana wenyewe kama taasis imara .
sasa nyie mliosubiria makapi mkaaza kuyasafisha kwa nguvu zote
 
Ni bora mtu kama wewe uwe kaburini huenda kuoza kwa mwili wako kutarutubisha ardhi yetu ya Tanzania kuliko kuwa na mtu mwenye mawazo kama yako humu JF.
Hili ni dua au nini? Haya ni maoni yangu ambayo hayastahili kunihukumia kifo! Uungwana unatakiwa na uangalie kauli zako zisikurejelee. Ni lini hivyo viwanda vilitaifishwa mpaka lro tuwaze kuwa vinaweza kufufuliwa vikarejea katika hali yake iliyotakiwa? Bado nafikiri baadhi yake ni rahisi kujenga kiwanda kipya kuliko hata kugikiria kuvifufua.
 
Umemwelewa lakini au unahara tu,

Teknolojia tuliyonayo ni tofauti na wakati viwanda vinabinafsishwa ni bora kujenga vipya kwa teknolojia ya kisasa.

Ulichotakiwa wewe ni kutoa maoni yako kuanzia alipoishia badala ya kutoa matusi.
Wanaendeshwa na mihemuko, wakati mwingine unafikiria kuna chemechembe za chuki kuliko hekima!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom