Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Rais magufuli komesha tatizo la watu kukaimu nafasi kwa mida mrefu

Nafahamu Rais JPM anafahamu kuwa serikalini kuna tatizo la baadhi ya watu kukaimu nafasi za madaraka kwa muda mrefu huku wakiwa hawana sifa za kushika madaraka hayo. Wenye sifa wamekuwa wakinyimwa fursa hiyo na hivyo kuwakatisha tamaa na kuzorotesha utendaji kazini.

Watu hao mara nyingi wamekuwa wakisaidiwa na baadhi ya wakubwa walioko wizarani kwa kile kinachoonekana ni ukabila, undugu na urafiki.

Nimetembelea maeneo mengi mfano Singida, Bunda, Shinyanga manispaa na kukuta tatizo hilo hasa kwenye idara za afya, manunuzi na uhasibu.

Naomba serikali hii ishughulikie hili ili wenye sifa wapewe nafasi hizo na hii itaongeza tija ya utendaji serikalini.
 
mambo ya kupigiana debe hayatakiwi hapa, faizafox, umekuwa zitto kumpalilia makamba jr kwenye uongozi.
 
Pongezi JPM. Kwa muda mfupi tu umeonyesha uwezo wa kumudu vyema nafasi yako. Nakuomba tupia macho huu mwenge wa uhuru hasa gharama za uendeshaji.
 
Mimi nataka aje pale halmashauri Ndipo kuna ukiritimba Mwingi,hongo na kujuana ndio vimekithiri.
 
Hahaaaaa kwimba maji yapo Ila huku hungumalwa no maji yan tabu tu umeme wanakata ovyo daah
 
Hahaaaaa kwimba maji yapo Ila huku hungumalwa no maji yan tabu tu umeme wanakata ovyo daah

Dada Eva,kwimba kubwa labda useme Ngudu,,Muamala na baadh ya Maeneo machache ndo kuna maji ya ziwa victoria maeneo Mengi maji ni ya shida sanaa,,Mfano hapo Hungumalwa Maji ni ya kununua kwe matorori tena yenye chumvi
 
Jaman kajanja tena? Ni afisa elimu anayependa haki na kufata utaratibu. Labda Kama unamuongelea mfikwa, colonel au yule mzee wa tsd. Kajanja hapana
 
kaka usibishe Shule ya Msingi Buyogo hawana madawati na kila Mwaka wanaazima Madawati kutoka Nela sekondari Kwa ajiri ya wanafunzi wa Darasa la saba kufanyia mitihani.

kwahiyo yanaagizwa wakati wa mitihani, nitawasiliana na shanif tujue ni kiasi gani kinachohitajika nanyie muache kushabikia ujinga.
 
Wizara ya maji IVUNJWE, idara ya maji iwe chini ya Wizara ya Ujenzi. Sioni kazi yoyote ya wizara ya maji zaidi ya kuendesha semina za maji pasipo maji.

Bajeti yake itumike kutafuta vyanzo vipya vya maji kama mto Rufiji, mto Nile, ziwa Victoria, ziwa Nyasa, visima n.k
 
Huo mfano wa mto Nile haujakaa vizuri,maana mto huo haupo nchini
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…