Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Na hii imekuwa ikiwafanya watu wengi kutaka kuhamia huko huko hata kama anamiaka 5 alipo kweli inakatisha tamaa sana unasoma na kozi moja darasa nchi moja mnaajiriwa na serikali moja kwa nafasi ile ile halafu wewe kwako panakuwa pakavu kwake kuna mchuzi lazima stress na kama mtu huyu hatakubali gap lililotengenezwa na serikali yenyewe atatafuta mpango wa kando ambao unaweza kuwa halali au haramu ili kufidia mipango yote hii itakuwa na athari ktk utumishi kubwa ikiwa kupoteza concentration kwenye kazi na rushwa
 

Duuh hivi unajua nazungumzia viongozi gani?Hakuna Mtumishi wa kawaida anayeendelea kulipwa asilimia 75 ya mshahara akiwa amestaafu!Ina maana uboreshaji umeanzia kwao?Ni miaka mingi tokea utararibu huo uanze,vp mbona haujafika kwa watumishi wa kawaida?Usikurupuke
 

Hahaaaaaaa,Pasco umeunganisha verse zangu vibaya,nina?homaanisha malipo ni makubwa na wako wengi wanaonufaika kwa wakati mmoja!Nilichopendekeza ni walipwe 10% ili hata wakiishi muda mrefu tuwe tumepunguza gharama!
Watu hawa wanainyonya serikali sana,ni wakati muafaka wa kuwadhibiti!
 
Wanaomtaka kafulila poleni sana. Kale kajamaa ni ka fisadi kakubwa.Hao wafadhili wake mabilionea waliomsaidia kumuondoa Muhongo wangemsaidia pia kumpa ubunge.
 
kwa kutekeleza dhana yako ya kupunguza gharama zisizo na tija,ningependekeza uwafutilie mbali wakuu wa wilaya wote na badala yake wilaya ziwe chini ya wakurugenzi tu...pia naomba utubadilishie mkuu wa mkoa wa dsm kwani jiji hili linahitaji mtu mwenye kaliba kama yako ili lisonge mbele kimaendeleo..
 
Hakupigwa chini kwa kura bali Zito na ccm ndiyo wamemhujumu kwa kupenyeza Goli la mkono.

Kafulila ni jembe, nina imani kwa msaada wa Mwenyezi Mungu atarudi mjengoni, siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga.
 
Tumeshaona majipu madogomadogo yakitumbuliwa sasa tunataka majipu makubwa kama ESCROW,RICHMOND,EPA,UUZAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI,KAGODA N.K yatumbuliwe haraka ili kuleta maisha bora kwa watanzania.Mungu akupe nguvu ya kuyatumbua hayo majipu,hongera sana umeanza vizuri kutumbua majibu
 
 
haya ya kuambiwa changanya na yako kwani nadhani mengine kubenea atatuongoza bungeni na hata baada ya ubatizo wa mch. dj
 
Ni lini wadanganyika wa nchi hii watafungua maabara ya kuwang'oa meno viongozi watafunao mali za umma.Inatosha msiba kuwa mawaidha,tumechoka na dhuluma,tumechoka na matatizo lukuki.Ni lini Tanzagiza itaondoka na kuturudishia Tanzania yetu.kama ikishindikana ni bora tuliasisi taifa letu lililokuwa na waadilifu wenye uchungu na rasilimali na wazalendo kwa taifa lao.Taifa hili si jingine ni Tanganyika,huenda tukiliasisi watawala wataiogopa Tanganyika,kwani historia ya taifa hili itawahukumu.
 
Jpm hii nchi haihitaji huruma uiendeshe kidiktete ili watu tubadilike tulizewea kusukumwasukumwa na kuchekeana .tunabitaji tutoke hapa tulipo sasa na sio kesho
 
USHAURI KWA RAIS JPM JUU YA VIONGOZI WA POLISI:

Mh.Rais JPM we are kindly advise you 2change all of Polisi leaders.Weka Viongozi wako hao wa mwenzio sasa basi. Ili kuendeleza ufanisi Na kuacha kufanya Kazi Kwa mazoea.Unaweza kuona wengine wanakuabisha Kwa Kuwa Na personal decision.

Mh.IGP,we know your capacity.wewe pia ni msomi.we know you since changombe.msaidie Rais Kwa haya majanga asichukiwe Na wananchi Kwa Haraka. Ameanza vizuri.Hawa viongozi wachache wasiokuwa Na weledi waondoe.wengine wamesoma sawa lakini hawajui leadership Na ideologically hawana strategic management plan.

Mh Rais.Hali hii inakuharibia Na kufanya wananchi wachukie uongozi wako.wakidhani wewe ndiye unawa-instruct police kufanya hivyo.Fanya surprise visit huko police post kama ulivyofanya muh.2 Na bandari.

Hao ma RPC,Hawashauriki OCD/OC-CID anaweza Kuwa Na Wazo Zuri.Lakini hawezi kusikilizwa na bosi wake kwakuwa yeye ni RPC ndiye anayeweza kuwasiliana Na IGP.

Aidha pia unaweza kubadilisha kabisa uongozi.na PGO.Ubadilishwaji huu wa uongozi uhusishwe na kupokea ushauri kwanza Kwa wale wa Chini.

Mfano ukienda Kwa Siri Na ghafla kwenye vyuo huko uonane Na wakuu wa vyuo Na ma lecturer wengi ni wasomi Na wanaweledi.Hasa pale Kurasini DPA wale walimu wanao fundisha maofisa ni kama wapo Chini ya Dk.Semboja.lakini Na kidato pia.

Maafisa almost all huwa wanapiia mikononi mwao.Kwakuwafahamu & by using professional zao wanaweza kusaidia Ku-fanya replacement au reshuffle nzuri ya jeshi leftu la Polisi. Ukienda police HQ pale huwa kwa kujuana wanapigiana chapuo. Hawana leadership,Strategic management wala academic reason.

MFANO:
Wanafunzi wa UDSM/UDOM wanaandamana wanaenda kwa mkuu wa Chuo kumueleza madai Yao Juu ya pesa ya Chakula wamepewa elfu 7000perday ziwekwe kwenye Ac zao wanunue Chakula wenyewe maana ni grown-up.

Mkuu wa Chuo amemuagiza "basa" pesa zichukuliwe Na Chuo wanafunz wale cafeteria wali maharage Na asbuhi chai rangi Andazi mbili.Wanafunzi walilalamika wakivumilia kwa miezi 3 bila kusikilizwa Na kupuuzwa.Change inayobaki ya wanafunz vigogo Hao wa Chuo wanamalizia ujenz wa baa zao huko Sinza.

Wanafunzi wakiwa njiani kwenda office ya mkuu wa Chuo.mkuu wa Chuo anampigia RPC "Jamanii naomba msaada wako wanafunz wanaandamana wanakuja Kuniua kwa madai ambayo mimi si husiki ni serikali.Pia Inaonekana Hawa wameagizwa Na Chadema" Huku yeye akijua wazi kosa lake.

Hapo polisi ni kama wamenusa unga wa pili pili kichaa puani,wameona Jina la Chadema...!
RPC Anaomba msaada wa kuongezewa nguvu kwa OC-Field Force Unit HQ.anaagiza OCD Na OC-CID waandae vikosi vya magari washa.mabomu Na risasi Na wala sio Brancoo ni Za "Fire" Wakifika wanasema "ilani ilani..........."mara moja ili mradi wakamilishe procedure.Wanafunzi wanapigwa vibaya,wanavunjwa miguu,mbavu,wanapasuliwa mishipa ya KICHWA.wengeni hospital.wengine Wanakuwa-arrested Na kuwekwa mahabusi kwa Muda usiojulikana.zaidi ya 100 "off registered"masomo.Wanafunz hawakuwa Na Silaha kabisa Zaidi ya Simu zao Na laptop mgongoni.

MFANO wa aliyekuwa RPC mmoja yeye was called kwa issue kama hiyo hiyo alipokwa magomeni kama OCD alichofanya.Japo alipigiwa Simu Na mkuu wa Chuo lakini alipofika hakwenda Officn Kwake.

Alikwenda mpaka kwa wanafunz akawasikiliza wanamadai gani ili kujua Shida Na source of problem.Wanafunz walikusanyika kwa wingi Chini ya mwembe chuoni wakamwambia madai Yao kwa jazba sana lakini yeye akawaondoa jazba Kwa weledi wa hali ya Juu.

Akawasikiliza akaagiza miongoni mwa wanafunz viongozi Na Askari wake mmoja wamwie makamo mkuu wa Chuo Na basa,Wakaja akawauliza mbele ya wanafunz kama madai ya wanafunz ni genuine wakakubali.

Akawauliza wapewe Siku ngapi ili wanafunz waweze kula Kama wanavyopaswa Kwa pesa waliyopangiwa.mkuu wa Chuo Na basa wakasema 14days. Akawapa namba viongozi wawili wa wanafunz after 14days wampigie Na endapo madai Yao yasipokamilishwa yeye OCD will escort wanafunz kufanya maandamano ya Amani kudai haki zao.

Lakini alisema Najua Basa Na mkuu wa Chuo hawawezi kuniangusha. Wanafunz walishangilia Sana Na walipenda wasukume Gari la OCD mpaka Officn Kwake.Yeye aliwasihi warudi darasani kwenye vipindi Kwani walikuwa wameshapoeza Muda mwingi wakamuelewa. Huyo si mwingine ni SAIMON NYAKORO SIRO sijui yuko wapi Kwa sasa huyu Kamanda Mweledi.

Leo hiii mhalifu akisikia a call afike Kwa Afande SIRO anakwenda mara moja anajua mahojiano ya haki ndiyo msingi wa uongozi wake sina hakika lakini pia kunamkoa alipewa nadhani pia akifanyakazi Kwa weledi.kwake Raia ama wananch ama watanzania ni msingi wa mafanikio Na Maendeleo yake.wengine sijui wanachukuliaje wanadamu. Kama ni kiongozi jiulize hili swali WHO IS PEOPLE 2 U? As a resul waki-retire Kurudi uraiani wanajifungia ndani.

MY ADVISE:1
(a) Polisi Wasifanye Kazi Kwa kukurupuka Na Kwa jazba,Ukisikia wananchi wana mgomo chuoni.kiwandani .maoficn.au mahali ama wanaandamana au wanalengo la kuandamana kupinga jambo Fulani ni Vema mkawasilikilize wale wanaogoma ama kuandamana kwanza.halafu upande wapili.wawekeni mezan msolve problem sio Kwenda kuchochea Fujo Kwa kupiga wananch mabomu.

(b) Au awe anajulishwa Kamanda SIRO aende kwanza kabla ya magari ya maji Na risasi.Hapo hamuwezi kumuangusha Mh.Rais na pia wananchi hawawezi Kuwa Na chuki Kwa uongozi wake.

ADVISE:2
Polisi wajengewe nyumba makazi BINAFSI ya kuishi Na familia zao.Halafu repayment ifanyike pole pole kwenye salary akishindwa akiba ya mfuko imlinde.Sio wanaishi kwenye Makambi ya Polisi Na magorofa,akimaliza Kazi anakabidhi nyumba Kwa meja wa kambi anaenda kupanga uraiani hii imepiwa Na wakati.

ADVISE:3
(a) Waboreshewe mishahara Yao. Kuwe Na malipo ya Elimu zao Na pia rank.Sio Askari Ana masrs-degree analipwa laki 600.Na mwingine darasa la Saba au form four failure ama Ana cer.in law-ni asp au super.analipwa mil 1.3 ndiyo Hao wanaofanyakazi bila weledi wengi ni wazamani hivyo wanavyeo vikubwa hufanyakazi Kwa uzoefu

(b) Askari anapandishwa cheo mwaka 2010 mpaka Leo hawalipwi mshahara wa cheo chake.anaambiwa mako makuu wanashughulikia hazina. Hazina wanasema bado hawajapewa fungu la wizara. Lakini fungu la magari ya maji washa ya billions of Shs lilipaikana Kwa hali ya dharula.

(c) Only happened Kwa uongozi uliomaliza Muda wake mwezi wa kumi mwaka huu.Hasira zinaishia Kwa Raia wema.Askari wasipopewa maji ya kunywa ni faini au mahabusu.Kesho asbuhi Kesi nyingine kabisa.hapo anajua lazima uje udhaminiwe. Na Askari akibainika anafukuzwa Kwa Rushwa.Lakini mazingira yameandaliwa Na viongozi wa Juu ambao ndiyo wanaokwenda kumuhukumu huyo Askari.

NB: Mh.Rais Kama haya ninayoandika niyauongo nenda pale DPA au kwenye police post yoyote Kwa Siri mchukue Askari wa Chini you will understand. Ama mchukue Yule Askari Polisi aliyewahi kukulinda ukiwa waziri wa ujenz miaka ya 2002-04 ulipokuwa ukifanya majukumu yako ya ujenz wa Barabara ambazo Leo wanazisifia wakati walichukia Na kufikiria kuondoka Na roho yako Washindwe kabisa Na wala usilipize.Yule Askari will explain black & white.

(d) Deliverance of report:
Wanapo-repot jambo Fulani kwenye media wanaonyesha hasira Na chuki ya nini? Jambo lenyewe linaweza Kuwa lakawaida. Kwa hili wajifunze Kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa ANGA.

Make follow-up ya report Zake kwenye media.mfano ya Askari wa kabuku Na speed barabarani-Rushwa.na nyingine.Anafanya Kwa weledi Na uadiliifu mkubwa Huku aki-smile,bila mihemko yoyote.Na wananchi ama Raia wanamuelewa.Lakini Habari hiyo hiyo inge-reportiwa Na wa pale DSM mmmh....!!!!! Mungu jalia hekima Na weledi Kwa jeshi la Polisi.
Naamin M4C-2 Magufuli 4Change ilikuwa ni Kweli endapo everyone of us will be responsible and accountable in our respectable offices. "SASA KAZI......"

Kikurajembe
 
Tunamshukuru sana rais wetu kwa kuzuia safari za nje ya na kufuta sherehe za uhuru . Ila conde chonde rais sisi tunaomba usifute sikukuu ya X-mass maana hii ndiyo njia pekee sisi wachaga tunasafiri baada ya kukaa nje ya moshi kwa mwaka mzima huku tukiwa tumewaacha wake zetu na baba mkwe wakikatia ng'ombe wa kisasa majani na pia ndio njia pekee ya kuonyeshana utajiri wetu na ubabe wa hela tulizotafuta mwaka mzima, pia ndio muda wa kujua nani ana pick up au stout mpya.
Aka magufuli.
 
Siku hizi jf kila anayejisikia kuandika utumbo anapost tu.hadhi hapa jf imeshuka sana.
 

Hiyo ndiyo maana ya demokrasia.
 
Atutangazie mshahara wake na ule wa makamu wake pamoja na wa waziri mkuu.

Ni haki yetu kujua tunawalipa kiasi gani.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…