Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Yas Wakuu Jimbo Letu Liko Kwenye Mkoa Wa Kilimanjaro Unaosifika Kwa Uchumi Wa Juu Lakini Wilaya Hii Ya Mwanga Inaweza Kuwa Chini Kiuchumi Ukilinganisha Na Wilaya Ya Tangahimba Newala Na Hata Singida Vijijini Kwenye Matembe Mengi Tu

Wakuu Wilaya Ya Mwanga Haina Chanzo Chochote Cha Ajira Na Hata Ardhi Yake Ni Ya Milima Hivyo Haifai Hata Kwa Kilimo
Ukiacha Kiwanda Cha Kutengeneza Pombe Kali Cha Bepari La Kihindi Kisichotoa Ajira Kwa Wakazi Wa Mwanga Hakuna Fursa Yeyote Vijana Wamwanga Wamejazana Stendi Wakiuza Maji Kwa Wasafiri Na Wengine Wamesepa

Wito Kwa Rais Usimpe Cheo Cha Uwaziri Mbunge Wangu Prf. Maghembe Ili Akishirikiana Na Dc Shwaibu Ndemanga Watengeneze Fursa Za Ajira Wilayani Humu Chonde Sana Rais Wangu
Mkoa wa Kilimanjaro ni moja ya mikoa very strategic, kwa vile mkoa wote umeshikwa na upinzani, mbunge huyu lazima apewe uwaziri ili tuu kuonyesha Kaskazini nayo imetoa waziri!. Mawaziri sio uwezo tuu lakini pia lazima wasambazwe!.

Pasco
 
Wacha tu ampe uwaziri amalizie mradi wa maji kwenda Dar, Magufuli kishabomoa ile nyumba ya mwana Ukawa kama alivyoahidi kwenye Kampeni.

#Hapakazitu

Hah hah hah Dar yenyewe ipo chini ya UKAWA sasa uitaka zungumzia vyama ama mutu binafsi hatutafika mbali. cha msingi ni kushirikiana kunyesha na kufundishana kutumia fursa zilizopo katika kusukuma Gurudumu la maendeleo kwa mmoja mmoja hatimae Taifa kwa ujumla.

Tunapenda Taarabu mno tatizo letu.
 
Wadau, nmekuwa nikifuatilia sana mchakato wa rais mpya wa tanganyika... Maana Zenji bado kuna mgogoro lkn naona kama kwenye donda ndugu anapakwepa kiaina flani. Namuomba atie maguu Tanzania Electric Company.

usiwashtue tunataka kuwashtukiza.
 
The open secret is that the TZS was overvalued...what happened is that the TZS returned to its true value and that is why we have relative stability at the moment.

Well it was an open secret. But so is the kenyan shilling and the imf did categorically state that. But it also stated that the term disorderly depreciation!

There is no doubt that the local unit was overvalued! But it is how you get it to equilibrium! Disorderly depreciation has caused a loss in confidence ; financial instability; and inflationary pressures!
 
Wadau, nmekuwa nikifuatilia sana mchakato wa rais mpya wa tanganyika... Maana Zenji bado kuna mgogoro lkn naona kama kwenye donda ndugu anapakwepa kiaina flani. Namuomba atie maguu Tanzania Electric Company. Kuwadadavua kama kweli kapania kuirekebisha hii nchi na pia namuomba ahakikishe gharama za umeme, mafuta, vyakula na vifaa vya ujenzi vinashuka ili kuwakomboa watz wa kipato cha chini.
Nawakilisha.....

Hebu mwache rais wetu......kama wamedhan wanaogopwa..hao tanesendelee na usanii wao..then siku isiyo na jina.....!!
 
Huyu bwana maghembe asipewe uwazir jimbo peke yake limemshinda ...kumpa uwazir nikutaka Wana Mwanga waendelee kuwa maskin hohehahe....
 
Naunga Mkono Hoja,Hayo Mashirika uliyoyataja Anza nayo fastaaaa,heshima lazima irudi Kitaa,ni ujuha kumlipa mchechu mil 36.5 kwa kazi ipi? kukaa vikao ambavyo analipwa 1.5m per session? Tangaza kazi hii weka mishahara mil 5 anayetaka aapply huku akijua mishahara ni huo na anapewa job description akishindwa piga chini na Kama akifuja Mali au akifanya fraud weka ndani tu.
 
Sidhani kama wewe ni mchumi (na kama ni mchumi basi utanisamehe..no disrespect intended). Ila bidhaa na huduma ndani ya nchi zikiuzwa kwa dollar...inaathiri sarafu yetu (TZS). Fikiria kwa mfano unataka kukodisha nyumba..mwenye nyumba aseme anataka $500 kwa mwezi...na wewe mshahara wako ni shillingi. Itakupasa uchukue shillingi zako uende bureau ukanunue dola..ili ulipe kodi. Au ulipe kwa shillingi lakini kwa exchange rate ya mwenye nyumba ambaye na yeye ataenda kununua dola. Hiyo inamaana kwenye huo muamala shillingi zimetumika kununua dola. Na kadri shillingi zimavyonunua dollar ndio dollar inaongezeka thamani na shillingi kushuka thamani (supply and demand).

Sasa fikiria kinyume chake...imagine kama hoteli ya serena ingekua inacharge shillingi kwa vyumba vyake. Hiyo inamaana mtalii anayetoka nje ya nchi ingebidi achukue dola zake anunue shillingi ili kulala serena. Hiyo inamaana shillingi yetu ingeongezeka thamani maana "inafukuzwa" na dola nyingi (supply and demand).
nimesafiri nchi ambazo uchumi wao uko juu sana kupita Bongo, na matumizi ya dola ni kawaida mpaka shopping,
sasa kwa nn iwe Bongo tu matumizi ya dola yasifae..:shock::shock::shock:
 
Mnasema kama anawasikia anafanya vitu kwa ajili ya sifa na kzkomoa ili kuongeza fedha za kzhudumia afya na elimu
 
Nianze kwa kukupongeza kwa uzalendo unaouonesha kwa kututumikia Watanzania bila woga wowote.

Enzi za mwalimu wanafunzi Wa UDSM waliwahi fanya mgomo na kuharibu mali. Mwalimu akawatia ndani. Kisha akawaeleza kuwa "The objectives you had are genuine but the methods you used to achieve those objectives were improper". Kwa nini hamkunitaarifu matatizo yenu kabla ya kugoma? Matatizo yenu ni sahihi kabisa ila njia mliyoitumia siyo sahihi.

Kuna rafiki yangu alinipigia simu jana usiku na kuniuliza "mbona waislamu Tu!? Mkurugenzi Wa muhimbili alieondolewa muislamu. Leo tena Wa TRA muislamu. Kulikoni!?". Nilimjibu kuwa Nina imani na magufuli. Ni coincidence tu lakini halengi waislamu.

Nikirejelea kauli ya mwalimu nyerere kwa wanachuo, muh magufuli upo sahihi kabisa lakini tafadhali fuata ushauri wangu ufuatao;

Endelea na oparesheni tumbua majibu. Amini kuwa sisi watanzania tupo nyuma yako. Ninachokuomba, unapoamua wizara au shirika lipi litumbuliwe, angalia dini ya mhusika. Changanya uwajibishaji kwa mujibu Wa dini. Leo muislamu kesho mkristu kwa sababu waliokosea ni mchanganyiko Wa dini mbalimbali. Ikitokea kigogo mwengine atakaeguswa ni muislamu, kazi yako iliyotukuka itaingiwa nchanga. Waislamu wataanza kulalamika.

Uongozi unahitaji kucheza na akili za watu. Kumbuka kuwa imani INA nguvu sana.

Usimbakishe fisadi yeyote serikalini. Fagia wote ila cheza karata zako vizuri kwa kufanya mkasi utue kwenye dini zote kwa sababu nina hakika wanaokosea si Wa dini moja Tu. Marejeo (reference) ya escrow, maliasili Nk... Ni kielelezo kuwa dini siyo kigezo cha ufisadi.

TANBIHI
Nimesukumwa na uzalendo kuandika makala hii na siyo udini!
 
Naunga Mkono Hoja,Hayo Mashirika uliyoyataja Anza nayo fastaaaa,heshima lazima irudi Kitaa,ni ujuha kumlipa mchechu mil 36.5 kwa kazi ipi? kukaa vikao ambavyo analipwa 1.5m per session? Tangaza kazi hii weka mishahara mil 5 anayetaka aapply huku akijua mishahara ni huo na anapewa job description akishindwa piga chini na Kama akifuja Mali au akifanya fraud weka ndani tu.

Kabisa, heshima lazima irudi serikalini na kwa wananchi.

Haya mashirika, JPM lazima ayafumue kama TRA.. maana wanaifisidi serikali..
 
Nimepitia sijaelewa vizuri, ngoja nikanywe chai nitarudi tena kuisoma.
 
Sidhani kama wewe ni mchumi (na kama ni mchumi basi utanisamehe..no disrespect intended). Ila bidhaa na huduma ndani ya nchi zikiuzwa kwa dollar...inaathiri sarafu yetu (TZS). Fikiria kwa mfano unataka kukodisha nyumba..mwenye nyumba aseme anataka $500 kwa mwezi...na wewe mshahara wako ni shillingi. Itakupasa uchukue shillingi zako uende bureau ukanunue dola..ili ulipe kodi. Au ulipe kwa shillingi lakini kwa exchange rate ya mwenye nyumba ambaye na yeye ataenda kununua dola. Hiyo inamaana kwenye huo muamala shillingi zimetumika kununua dola. Na kadri shillingi zimavyonunua dollar ndio dollar inaongezeka thamani na shillingi kushuka thamani (supply and demand).

Sasa fikiria kinyume chake...imagine kama hoteli ya serena ingekua inacharge shillingi kwa vyumba vyake. Hiyo inamaana mtalii anayetoka nje ya nchi ingebidi achukue dola zake anunue shillingi ili kulala serena. Hiyo inamaana shillingi yetu ingeongezeka thamani maana "inafukuzwa" na dola nyingi (supply and demand).

Cha msingi ni kufuta sheria zinazoruhusu matumizi ya dollar nchini Tanzania. Sheria hizi ni zile za madini na utalii. Zikifuatwa hoteli zote zitatoza kwa shilingi. Pia malipo ya leseni za madini na shughuri zingine zinazoendana navyo zitalipwa kwa shilingi yetu.

Tukianza na hizo wageni watakuja kuona wanyama na kutafuta madini kwa kutoa dollar (supply) na kutafuta (demand) shilingi. Kama sheria ya uchumi ilivyo shilingi ikitafutwa sana inapanda bei (yaani inakuwa imara dhifi ya sarafu zingine) na dollar inayotolewa itashuka bei kutoka iliko sasa hivi ya Tzs2,150 kwa shilingi hadi tuseme Tzs800 kwa dollar!
Kama hatuwezi tupitishe sheria inayoruhusu sarafu moja tuseme dollar. Hatuwezi kuweka ulingo mmoja kijana anaanza kukimbia (shilingi) na mwana riadha maarufu (dollar) halafu tutarajie ushindi (yaani shilingi kuwa imara); itakuwa madafu tu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom