Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kwani kuna lugha nyingine mbadala ambayo angeweza kuitumia zaidi ya kiswahili?
Kiingereza mkuu ambacho amekitumia hadi kufikia ngazi ya udaktari kwa kusoma na kufanya utafiti sio wa kupewa. Nyingine ni kisukuma. Anakifahamu vizuri lakini sio lugha rasmi kitaifa na kimataifa
 
Sawa kabisa. Nyongeza katika swala la elimu.

Afumue kabisa wizara ya elimu.. watu waliopo pale hawana jipya. Hawana mbinu wala mifano ya namna gani utoaji wa elimu katika karne ya 21 inatakiwa iwe.

Katika elimu tuanze kufuta ubabaishaji kwa kuwapa ajira watu walio competent kuanzia walimu na maafisa wengine. Pili walipwe mshahara unaolingana kabisa na kiwango cha elim lakini pia mshahara linganifu na katika sekta zingine. Mazingira ya kazi yaboreshwe, kuwepo uwiano mzuri kati ya mwalimu na wanafunzi. Ikiwa na maana kuwa angalau uwiano uwe 1:50 kwa shule za msingi, 1:45 shule za upili na 1:30 kwa vyuo vikuu. Hili linaweza tekelezwa hatua kwa hatua ndani ya miaka mitano.

Miundombinu katika elimu.. serikali iwekeze katika ujenzi wa miundo mbinu ya elimu badala ya kuliacha jukumu hilo kwa wananchi maskini au halmashauri za wilaya zilizojaa wababaishaji na wezi. Hii itawezesha Tanzania kuwa na miundo mbinu ya kisasa na ya viwango.

Asanteni
 
Kila chama kilikuwa na ilani yake, sasa kusema ampe ubunge then cheo anachostahili Serikalini una maana gani? Je akiwa serikalini atakuwa anatekeleza ilani ipi kati ya ile ya ACT ya kwake na hii yenu ya CCM?

Wote ni CCM so Atatekeleza ilani ileile ya mafisiem
 
Wakitutembelea hapa atumie kiswahili. Akitembea kwa wenzetu waarabu, wachina, warusi Nk atumie kiswahili

Akitembea ktk nchi za kiingereza kama uingereza, baadhi ya nchi za ulaya na marekani hana budi kutumia kiingereza

inasemekana jamaa ni mtupu kwenye hiyo lugha ya kufundishia. Huoni wazo hili ni kujihami na kuficha huo udhaifu? Hiyo siku atakayoongea kizungu nadhani hapa jukwaani ndio itakuwa sehemu ya kumdhihakia. Japo ni wazo zuri kutumia kiswahili hasa kama jamaa ni mzito kwenye hiyo lugha.

Wanaccm jiandaeni kukoseshwa raha hiyo siku kizungu kitatumika na kama andaeni matusi kabisa maana itakuwa shida
 
Wakitutembelea hapa atumie kiswahili. Akitembea kwa wenzetu waarabu, wachina, warusi Nk atumie kiswahili

Akitembea ktk nchi za kiingereza kama uingereza, baadhi ya nchi za ulaya na marekani hana budi kutumia kiingereza.


Akihutubia mikutano ya kimataifa kama ya afrika mashariki, sadc, AU na UN atumie kiswahili
Hata huko Uingereza, Ulaya na Marekani anatumia tu kiswahili akina Obama na Cameroun watatafsiriwa. Mbona viongozi wa china wanakwenda huko na wanatumia kichina na kuelewana bila shida.
 
Bila kumsahau mzee wa tanzania ni muungano wa visiwa vya zimbabwe na tanganyika..huyu ahata uraia anyanganywe
 
Huyu kwakweli taifa linamuhutaji sana bila shaka jpm kesha uona uwezo wake..mimi nilimsikiliza siku ile ya jpm anapewa hati ya urais nilimkubali sana huyu mama..smart n beauty..!
 
Wote hao walionekana wabovu kutokana na kuwa na RAISI mbovuuu. Magufuli anaweza chukua baraza hilohilo ila yeye akawa hachekicheki na kukesha angani.
 
Ukiwa rais hata kilugha chako kinaeleweka.Sembuse ushauri wako?
 
Jamani tuweke akiba ya maneno hapo.
Mimi ninachokiona kila mtu ni mtendaji mzuri akisimaniwa vizuri.
Kwa kuwa tumempata msimamizi mzuri basi atakayeteuliwa kuwa waziri ajue sio zama zile za kujisimamia ila atasimamiwa na kupimwa kazi zake na bosi wake ambae ndie rais wa JMT.
Kubwa zaid rais kasema wazi km mtu anajiona hawez kuendana na kasi basi aseme mapema.
Tusipuge kampeni humu fulani hafai fulani anafaa huu ni unafiki ambao rais hataki kuusikia
 
We kamwambie tu uache porojo, hapa jf RAIS ana watu wake wanaokusanya maoni na mitazamo ya watu. ndio maana ukiwachokonoa wakubwa hapa jf watakujia juu.Nashauri Akisharudisha hizo pesa achunguzwe ili serikali ikjiridhisha 2020 ndo apewe huo uwaziri

Hahaha sawa nimekusoma, siwezi kubishana kwa kitu kama hicho, kama unadhani baraza la mawaziri linapatikana kutokana na michango ya jf basi baki na mawazo yako.
 
Kwani kiingereza ni nini mbona wachina hawakijui na ni tishio duniani? Tunadumaza akili zetu kwa kuziongezea mizigo bure. Sawa tusome tukifahamu lakini siyo lazima kukitumia kila mara unapotaka kuwakilisha mawazo yako ya kina. Vikwazo vya lugha visimaanishe eti hatuna watu vichwa kuliko wazungu.
Mkuu fikiri kabla ya ku type bwana unafanisha china na Tanzania kwa kigezo cha lugha are u serious??? Unamatatizo na bila shaka utakuwa ccm
 
Rais anajua kazi yake, siyo mpaka mumpangie nani wa kuteua na nini cha kufanya. tulieni. Kwani mna ubia na urais wake?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom