Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
mnatuchosha sasa na huyo mtu wenu kila siku kutujazia servers tu hapa jukwaani, kama alikua na umuhimu huo wananchi wa jimbo lake wangeanza kuliona hilo, tafadhalini msituchoshe hii ni thread ya kumi sasa tunahesabu kuhusiana na mtu mmoja. hakuna mengine ya kujadili?
 
Nina wasiwasi na kiwango cha elimu yako itakuwa la7. Nimekuwa nikifatilia post zako hazina mshiko. Vipi afya ya mgombea urais kupitia ukawa?

La saba mbona kubwa sana, unanipa cheo si changu?

Angalau nikupe ahsante kwa kunipaisha namna hiyo.
 
Mimi umeanza vizuri sana. Umenikosha. Unataka pesa utekeleze majukumu yanayokukubili. Wakwepa kidi bandarini wametesa sana. Kumbe unajua. Leo wanasema wamefilisika. Watatumia makampuni mbadala. Vipi mmiliki wa kampuni hiyo ataendelea kuwa balozi mdogo Guanzou, china? Hahahhaha. Mkwepa kodi anakuwa balozi. Raha sana. Kwetu tunasema yeeeeeeeeba mwana wasu.
 
Taifa limedhoofika kwa kuendekeza starehe za magari ya kifahari.chagua viongozi watakao kubali hata kutumia noah.
 
ni ushauri mzuri. pia magari ya serikali yatumike mwisho ijumaa. weekend yabaki tu kama waziri ana matumizi yake binafsi anunue lake....
 
ili kubana zaid matumizi inabidi watumie carina ti na premio
hapo nchi itasonga tujifunze india
 
Mhe.Rais nianze kwa kukupongeza kwa kufuta safari za Nje kwa watumishi wa umma kwa kutumia Fedha za Serikali.. Hakika eneo hili lilikuwa linapoteza Fedha nyingi na kupunguza morali ya kufanya kazi kwani watu walikuwa wanawaza kusafiri tuu.

Pamoja na pongezi zangu naomba nitoe ushauri jinsi ya kuboresha uratibu wa safari za Nje kwa lengo LA kuokoa Fedha za serikali.. Kwani ushauri huu unakuja kwa kutambua kuwa safari za Nje haziepukiki katika baadhi ya ofisi za serikali..

Kwanza: Boresha mishahara ya watumishi hasa watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa kwani watu hupenda sana safari kwa sababu mishahara haitoshi ni midogo kupitiliza... Fanya utafiti mhe.Rais Wage bill ya Ewura + Tanroad yaweza kuwa sawa sawa na wage bill ya wizara zote za serikali kuu... Hakika kunatofauti kubwa sana ya mishahara inayosababisha watu waishi kiujanja ujanja... Pia utakuta kitu cha ajabu kama utafanya utafiti wa kutosha mshahara wa mlinzi was TPA ni sawa na Mshahara wa afisa katika serikali kuu na mitaa..

Pili.. Uratibu wa safari za Nje ubadilike ili MTU asafiri pale tu panapokuwa na ulazima wa kufanya hivyo. Kutengeneza mazingira ya kitokuwa na tofauti kati ya MTU aliyesafiri na asiyesafiri... Tutafanyaje ni rahisi sana na kwa kuwa una wataalam wa kila aina naomba wafanye utafiti na kuangalia uwezekano wa MTU kulipiwa Hotel na usafiri tu (Pale anapokuwa amesafiri) na kufuta posho ya kujikimu hakika utaokoa Fedha nyingi sana na kuzielekeza katika kuboresha maisha na maslahi ya watumishi kwa ujumla wake... Mfano MTU akisafiri kwenda USA.akalipa nauli/tiketi- hii inafanyika sasa; unamlipia hotel ya USD 80 akifika yeye ni kukaa tu; na bocket money USD 50 kwa siku hakika tutaokoa Fedha nyingi mhe.Rais.

Tatu.. Serikali yako najua inapenda usawa kuna taasisi za serikali wanatoa posho kibao.. Posho za nyumba.. Furnicture .. Usafiri - mhe.Rais haya mambo ni adimu kwa baadhi ya taasisi najua First Lady ni mwalimu unaweza muuliza kama alikuwa anapata hizi posho ambazo ni mhimu kwa MTU kuendelea...mulika napo hapa

Nina mengi Ila naomba niishie hapo kwa leo.. siye tupo tayari kutekeleza slogan yako ya hapa kazi tu...
 
Magari haya ya V8 sioni faida yake na hauna tija yoyote zaidi ya gharama kubwa serikalini. Piga marufuku Mara moja tunahitaji fedha ya kununua vitanda, dawa za hospital, madawati na labs shuleni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom