Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Wadau amani iwe kwenu.

Kama kuna kosa kubwa ambalo Kikwete analijutia ni la kumteua James Mbatia kuwa Mbunge. Wapinzani wa Tanzania wanabaki kuwa wapinzani. Hawana hoja za ushindani bali ni za upinzani. Ndivyo alivyofanya James Mbatia. Baada ya kuteuliwa kuwa mbunge, siku zote alikuwa anamuandama Kikwete na kumzulia chungu ya mambo ambayo kimsingi hayakuwa sahihi. Bahati mbaya sana Katiba haitoi fursa kwa Rais kumfuta mtu ubunge baada ya kumteua.

Kikwete alikuwa na matarajio kuwa James Mbatia angejenga hoja zenye mustakabali mwema kwa taifa. hata hivyo, Mbatia akawa ndiye kinara wa kuishambulia serikali na CCM na akawa anaporomosha kejeli kwa aliyemteua. Shukrani ya Punda.

Kwa somo tulilopata kwa James Mbatia, nakushauri Rais wangu Magufuli, achana kabisa na hawa wanaojiita wapinzani hasa wale wanaotoka kule Kaskazini. Si watu kabisa. Watakuvunjia heshima bure. Bora ukawafuta machozi wabunge wengi wa CCM ambao wamekumbwa na jinamizi la Ukaskazini kama Ole Sendeka, Namelock Sokoine na Anne Kilango ambao naamini ni watu makini na wana uchungu na chama chao na nchi yao.
 
Mh umekuwa ukisisitiza kwenye kampeni "hapa ni kazitu#" na kupambana na ufisadi. Ushauri wangu ni huu hapa:

1) Huduma za jamii ziboreshwe ili wenye huduma hizo binafsi ama wafuunge au washushe gharama zao ili watanzania wengi waweze kumudu. Huduma hizo ni kama vile madawa hospitali, vitabu mashuleni, nk.

2) Ufanyike utafiti kuhusu njia kuu za ufisadi ili mianya, mirija na bomba zake zifungwe. Wahusika, baada ya muda mfupi, watajifunga wenyewe badala ya kupitia njia ya mahakama ambayo ni ndefu yenye upotevu wa muda na pesa.

3) Ajira za vijana: Mikakati na juhudi zichukuliwe kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali (km kilimo, mifugo, uvuvi), kutoa huduma (km gereji, saloon, migahawa) na sanaa. Makumpuni yahamasishwe kuvisaidia hivi vikundi kwa mitaji au mashindano. Matokeo yake yatakuwa ni zaidi ya ajira kwani jamii itapata bidhaa na huduma zilizo bora na nyingi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA na UONGOZI WAKE MPYA

Ndoto za Alinacha...
 
Kupinga Ufisadi gani "Unafiki tu".Unapinga Ufisadi halafu unaungana na FISADI LOWASSA.

Nadhani unazungumziwa ufisadi ambao unaonekana kwenye nyaraka ambazo kafulila alikuwa nazo kuhakikisha mf.dili la ESCROW,na si Ufisadi unaopatikana kwa mtu kuandikwa Fisadi magazetini au kwa kuwa tu mtu ni Tajiri kama Lowassa,Bakhresa.
 
Wadau amani iwe kwenu.

Kama kuna kosa kubwa ambalo Kikwete analijutia ni la kumteua James Mbatia kuwa Mbunge. Wapinzani wa Tanzania wanabaki kuwa wapinzani. Hawana hoja za ushindani bali ni za upinzani. Ndivyo alivyofanya James Mbatia. Baada ya kuteuliwa kuwa mbunge, siku zote alikuwa anamuandama Kikwete na kumzulia chungu ya mambo ambayo kimsingi hayakuwa sahihi. Bahati mbaya sana Katiba haitoi fursa kwa Rais kumfuta mtu ubunge baada ya kumteua.

Kikwete alikuwa na matarajio kuwa James Mbatia angejenga hoja zenye mustakabali mwema kwa taifa. hata hivyo, Mbatia akawa ndiye kinara wa kuishambulia serikali na CCM na akawa anaporomosha kejeli kwa aliyemteua. Shukrani ya Punda.

Kwa somo tulilopata kwa James Mbatia, nakushauri Rais wangu Magufuli, achana kabisa na hawa wanaojiita wapinzani hasa wale wanaotoka kule Kaskazini. Si watu kabisa. Watakuvunjia heshima bure. Bora ukawafuta machozi wabunge wengi wa CCM ambao wamekumbwa na jinamizi la Ukaskazini kama Ole Sendeka, Namelock Sokoine na Anne Kilango ambao naamini ni watu makini na wana uchungu na chama chao na nchi yao.
baada ya bunge la kumi kuisha tumeshuhudia wabunge wengi hasa wa ccm wakikiri waziwazi wameshindwa kufanya kazi iliyowapeleka ya kuisimamia serikali na matokeo yake wakawa watetezi wa chama, kazi ya mbunge bungeni ni kuisimamia serikali.
 
Kupinga Ufisadi gani "Unafiki tu".Unapinga Ufisadi halafu unaungana na FISADI LOWASSA.

Hakuna ushahidi kamili kuwa Lowassa ni fisadi.Halafu Lowasa ni adui wa ccm hivo ni rafiki kwetu kwa ule wakati(The enemy of your enemy is your Friend)
 
Achague wabunge wapya walete mambo mapya hao kama hawakutendea mengi ya kufurahisha wanajimbo wao wakapumzike.
 
Wadau amani iwe kwenu.

Kama kuna kosa kubwa ambalo Kikwete analijutia ni la kumteua James Mbatia kuwa Mbunge. Wapinzani wa Tanzania wanabaki kuwa wapinzani. Hawana hoja za ushindani bali ni za upinzani. Ndivyo alivyofanya James Mbatia. Baada ya kuteuliwa kuwa mbunge, siku zote alikuwa anamuandama Kikwete na kumzulia chungu ya mambo ambayo kimsingi hayakuwa sahihi. Bahati mbaya sana Katiba haitoi fursa kwa Rais kumfuta mtu ubunge baada ya kumteua.

Kikwete alikuwa na matarajio kuwa James Mbatia angejenga hoja zenye mustakabali mwema kwa taifa. hata hivyo, Mbatia akawa ndiye kinara wa kuishambulia serikali na CCM na akawa anaporomosha kejeli kwa aliyemteua. Shukrani ya Punda.

Kwa somo tulilopata kwa James Mbatia, nakushauri Rais wangu Magufuli, achana kabisa na hawa wanaojiita wapinzani hasa wale wanaotoka kule Kaskazini. Si watu kabisa. Watakuvunjia heshima bure. Bora ukawafuta machozi wabunge wengi wa CCM ambao wamekumbwa na jinamizi la Ukaskazini kama Ole Sendeka, Namelock Sokoine na Anne Kilango ambao naamini ni watu makini na wana uchungu na chama chao na nchi yao.

Unafikiri atakuteua wewe....lazma amtafute kijana mmoja wa CHATO
 
Kafulika ESCROW imemponza!! ukiwa msema kweli na mpenda haki nchi hii lazima yakukute tu.
 
Akuna huruma namshanga kwa kwa ziara za kushtukiza leo kaelekea njia ya morogoro kupitia mbezi wakati karuka hapo tanesco na dawasco palipo na uchafu wote nchii hiii
 
Wadau amani iwe kwenu.

Kama kuna kosa kubwa ambalo Kikwete analijutia ni la kumteua James Mbatia kuwa Mbunge. Wapinzani wa Tanzania wanabaki kuwa wapinzani. Hawana hoja za ushindani bali ni za upinzani. Ndivyo alivyofanya James Mbatia. Baada ya kuteuliwa kuwa mbunge, siku zote alikuwa anamuandama Kikwete na kumzulia chungu ya mambo ambayo kimsingi hayakuwa sahihi. Bahati mbaya sana Katiba haitoi fursa kwa Rais kumfuta mtu ubunge baada ya kumteua.

Kikwete alikuwa na matarajio kuwa James Mbatia angejenga hoja zenye mustakabali mwema kwa taifa. hata hivyo, Mbatia akawa ndiye kinara wa kuishambulia serikali na CCM na akawa anaporomosha kejeli kwa aliyemteua. Shukrani ya Punda.

Kwa somo tulilopata kwa James Mbatia, nakushauri Rais wangu Magufuli, achana kabisa na hawa wanaojiita wapinzani hasa wale wanaotoka kule Kaskazini. Si watu kabisa. Watakuvunjia heshima bure. Bora ukawafuta machozi wabunge wengi wa CCM ambao wamekumbwa na jinamizi la Ukaskazini kama Ole Sendeka, Namelock Sokoine na Anne Kilango ambao naamini ni watu makini na wana uchungu na chama chao na nchi yao.
duh! unamshauri rais huku jf! au unawafanyia kampeni ya ubunge waliokataliwa na wananchi majimboni,au wewe ni mmoja wao? rais atumie busara yake na kama unataka kumshauri lifanye faragha, humu ni mjadala,kusifu au kukosoa,tuma ujumbe au ushauri kwa faragha kwa rais
 
Kwa muda mrefu katika nchi yetu kumekuwa na utengenezwaji wa pombe kiholela,kuanzia za kienyeji mpaka hizi nyingine,zinauzwa kiholela,stand ya mabasi,madukani,barabarani na kwenye vioski,pombe hizi zimesababisha madhara makubwa sana kwa jamii yetu,pombe hizi zinanyweka wakati wa mchana ambao ni mahsusi kwa shughuli za uzalishaji mali,familia nyingi zimeathirika sana,namshauri Rais wangu JPM aanza na hili,funga bar zote mchana,fungua saa kumi funga nne usiku wakalale.Waambie watafute vyanzo vingine vya mapato sio kutegemea walevi,vijana wamekwisha,hata kuzaa hawawezi.
 
Jambo la kushangaza ni kuona mtu mwenye cheo na madaraka kama ya DC,RC,Daktari Bingwa, Profesa,Mwanasayansi mashuhuri na wengine wenye majukumu muhimu katika jamii, kitaifa na kimataifa, wanaacha kazi zao na kuimbilia kwenye ubunge. Hiki ni kitendawili.
 
Baba koku kwani ubunge sio jukumu muhimu katika jamii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom