Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau amani iwe kwenu.
Kama kuna kosa kubwa ambalo Kikwete analijutia ni la kumteua James Mbatia kuwa Mbunge. Wapinzani wa Tanzania wanabaki kuwa wapinzani. Hawana hoja za ushindani bali ni za upinzani. Ndivyo alivyofanya James Mbatia. Baada ya kuteuliwa kuwa mbunge, siku zote alikuwa anamuandama Kikwete na kumzulia chungu ya mambo ambayo kimsingi hayakuwa sahihi. Bahati mbaya sana Katiba haitoi fursa kwa Rais kumfuta mtu ubunge baada ya kumteua.
Kikwete alikuwa na matarajio kuwa James Mbatia angejenga hoja zenye mustakabali mwema kwa taifa. hata hivyo, Mbatia akawa ndiye kinara wa kuishambulia serikali na CCM na akawa anaporomosha kejeli kwa aliyemteua. Shukrani ya Punda.
Kwa somo tulilopata kwa James Mbatia, nakushauri Rais wangu Magufuli, achana kabisa na hawa wanaojiita wapinzani hasa wale wanaotoka kule Kaskazini. Si watu kabisa. Watakuvunjia heshima bure. Bora ukawafuta machozi wabunge wengi wa CCM ambao wamekumbwa na jinamizi la Ukaskazini kama Ole Sendeka, Namelock Sokoine na Anne Kilango ambao naamini ni watu makini na wana uchungu na chama chao na nchi yao.