Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
wengi wao wameweka halmashaur hizi ni makwao. ko wanajidai sana. Halmashauri ya Kilolo watendaji wa juu wanakaa maofisini kama nao wanataka kujiweka miungu watu hawataki kuona na wafanyakaz wa ngazi za chini. kwa hili naona safisha safisha ije. mtu mwenye elimu yako unaambia ongea shida zako na masijala sasa masijala anatoa msaada gani jaman tuende na wakati. tusichukulie hizi ajira ni permanent. ipo siku unae mdharau atakuwa bosi wako. na suala la kukata kata mshahara eti ume chelewa likizo halmashaur ya mafia ina ongoza, maafisa weng wanashirikiana na watendaji wa benk kukata fedha za wafanyakaz bila hata huruma, wakati mazingira ya kaz ni magumu, kwenda huko mpaka uvuke na mitumbwi, jahaz, boti hakuna meli huko. ndege inakula asilimia 50 ya mshahara. ni mateso kwa wafanyakaz wa huko.
 
Nhisi hakuna jipya utendaji wa Rais Magufuli. Huu ni wajibu wake tena hajatimiza ndoto za usawa, haki kudhibiti mauaji ya ovyoovyo, kujilimbikizia mali na mengine mengi. Kinacho tufanya tushangae sikioni. au tunashtushwa na matukio?

Anachokifanya ni kuuanika uozo uliomo serikalini. Hamna jipya bali yote haya yalipigiwa kelele na Slaa 2010. Tena mengine mengi bado hajayagusa. najaribu kuamini msemo wa Roma kwamba UCHAFU WA MRISHO UNAMFANYA MSAFI AONEKANE BENJA.

KUNA sehemu nyingi sana tunaporwa. kodi zinapotea, misamaha mikubwa ya kodi kwa makampuni, ukimbizwaji wa mbio za mwenge, mishahara minono kwa baadhi ya watumishi, katiba mbovu, madai ya walimu, mishahara hewa, undugu makazini.baadhi ya vyeo visivyo muhimu serikalini tena vya juu(mikoa na wilaya). Tanzania ni kichaka chenye kira mnyama, ukirusha jiwe utasikia ushamtungua mmoja.

Anaiacha uchi serikali iliyoongozwa na watangulizi wake, mda naye tutayasikia yake.

Eti unahisi; my foot!!!! Usitumie hisia (emotions) dogo! Tumia akili (brains); chambua, chekecha, nyumbulisha! Usikubali kukaririshwa! Eti dr Slaa! Ganda la muwa la jana chungu kala nini?! Anyway; Asiyejua maana haambiwi maana! Baki ulivyo! Ni kichanga tu wewe; ukikua utaelewa. Bs
 
mpe ushauri nae ni binadamu. mbona wanapita humu JF. toa solution usi attack moja kwa moja. sawa mkuu.
 
Nhisi hakuna jipya utendaji wa Rais Magufuli. Huu ni wajibu wake tena hajatimiza ndoto za usawa, haki kudhibiti mauaji ya ovyoovyo, kujilimbikizia mali na mengine mengi. Kinacho tufanya tushangae sikioni. au tunashtushwa na matukio?

Anachokifanya ni kuuanika uozo uliomo serikalini. Hamna jipya bali yote haya yalipigiwa kelele na Slaa 2010. Tena mengine mengi bado hajayagusa. najaribu kuamini msemo wa Roma kwamba UCHAFU WA MRISHO UNAMFANYA MSAFI AONEKANE BENJA.

KUNA sehemu nyingi sana tunaporwa. kodi zinapotea, misamaha mikubwa ya kodi kwa makampuni, ukimbizwaji wa mbio za mwenge, mishahara minono kwa baadhi ya watumishi, katiba mbovu, madai ya walimu, mishahara hewa, undugu makazini.baadhi ya vyeo visivyo muhimu serikalini tena vya juu(mikoa na wilaya). Tanzania ni kichaka chenye kira mnyama, ukirusha jiwe utasikia ushamtungua mmoja.

Anaiacha uchi serikali iliyoongozwa na watangulizi wake, mda naye tutayasikia yake.

we mwanazuoni hapo saut au unaishi jirani na chuo?
kama mwanazuoni unawaza namna hii unatofauti gani na bodaboda aliyekuwa anasubiri benki yao.
 
Tunataka atoe ufafanuzi mapema, maana 50000 ya necta kidato cha nne haina tofauti na ada kama itaachwa
 
Kuiongoza Tanzania ni rahisi kama kumsukuma mlevi, watanzania ni watu wa ajabu sana, watu wamekaa vyuoni lakini walichofaidi ni kutoka na makalatasi tu na kakingereza ka uongo na ukweli lakini vichwani hamna kitu, tanzania umeme unakatika mwezi mzima ukiwaka wiki moja wanachangilia na kumpongeza meneja huku wakilipa bil hata ile umeme ulikuwa hauwaki, hiyo unaikuta tanzania tu, watu wanachangishwa michango ya kujenga shule, wanafyatua tofali wenyewe, lakini ileta mabati tu wanashangilia na kusema selikali inawajali hiyo unaikuta tanzania tu, watanzania hawajui haki zao, watanzania tumeitwa majina mengi ya aibu na marais wa mataifa mbalimbali, sasa hivi magufuli kafanya katukio kidogo tu, tumesahau shida zote mpaka watu wanamkufulu Mungu wakimwita masihi, magufuli kazi kwako lakini mimi bado nalia na tanzania yangu.
 
Elimu ya msingi mpaka kidato cha nne ulisema ni bure, hii bure mbona haiko wazi kuhusu malipo ya mitihani ya kitaifa hasa wa kidato cha nne??

Ebu toleeni ufafanuzi ili maana january ndiyo hiyo vijana wanaenda kufanya usajili wa mtihani huo

Umeambiwa inaanza kutumika Januari 2016 sasa kiherehere cha nini? Si usubiri ianze rasmi halafu ukilipishwa ndiyo uje kulalama hapa?
 
La umeme usiseme watu wanashangilia kama wanapewa bureeeeeeeeeeeeeeeeee, kumbe ulishalipia kitambo bali hujapewa ulicholipia!!!!!!!!!!!!!, je huu ni uungwana kweli?
 
Hili tatizo la umeme ni janga la kitaifa, na ukiligusia hapa kuna watu wanamtetea Magufuli utawaona watakuja mbio kusema ana siku 20 ikulu haraka za nini. Kama ana siku ishirini tu ndio kisingizio kwamba hajui tatizo la umeme?

CC: Hammy-D
 
Kwanza nianze kumpongeza kwa kusimamia utumbuaji wa majipu ya nchi hii, iko hivii ni vema Safari ya nje ya nchi ya kwanza ya Mheshimiwa Magufuli aanzie kwanza nchini Kuwait kuwaomba Radhi Sadam hakuwahi kuwa Rais wa Kuwait.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom