Mheshimiwa Raisi, nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya. Umewadhihirishia Watanzania kwamba penye nia hakuna linaloshindikana. Umethibitisha kutembea katika maneno yako "HAPA KAZI TU".
Ninaimani na baraza ulilolichagua, na ninaelewa kwa umakini ulioouonyesha kwa Muda mfupi tangu ushike madaraka, bila shaka umezingatia sana ufanisi wa kazi, sifa na malengo ya taifa kwa awamu yako hii.
Kwa kuzingatia hili, ninakushauri WIZARA YA UJENZI NA MIUNDOMBINU AMBAYO WEWE UMEKUWA KINARA WAKE KWA MIAKA MINGI, umteua Engineer Mashiku M. P. aliyeko umwagiliaji.
Huyu mtu ni mchapa kazi wa kiwango cha juu na ambaye anaweza kuwa miongoni mwa Watanzania wachache wanaopashwa kuigwa.
Ni mtulivu na kiongozi makini asiye na makundi, majungu wala makuu. Yeye ni 'HAPA KAZI TU".
Ni mwadilifu na hajawahi kuhusishwa katika kashfa yoyote. Ni mtu asiyekubali hazi iharibike na ni mtu ambaye ni results oriented, mjenga team ya kazi, anasimamia uwajibikaji na results oriented.
Hana mbwembwe wala haonei mtu. Ni kiongozi na Mhandisi mzuri sana.
Bila shaka Mheshimiwa raisi, kwa kumteua Engineer Mashiku M.P, kuwa waziri wa Ujenzi, hutakuja kujuta, watanznia hawatajuta na zaidi sana uteuzi huu utaimarisha kazi na viwango vya ufanisi wa kauli mbiu yako ya "HAPA KAZI TU".
Engineer huyu ni miongoni mwa wahandisi wachache sana wa kuigwa duniani.