Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Engineer Mashiku P. M.

Yuko wizara ya kilimo ni mkimya sana, lakini mchapa kazi kuliko kawaida, hana makuu ni mweledi na mwadilifu hujawahi ambiwa.

Kama anahitaji watu wa kufanya nao kazi kwa kauli mbiu ya "hapa kazi tu", naam huyo ndiye saizi yake na hatajuta na wala Watanzania hawatajuta. Jamaa ni balaa wa kazi na utawala.
 
CPC Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi 2012 ni mchapa kazi mzuri sana na siku zote kwenye utendaji wake ni mwenye kusimamia sheria, kanuni na taratibu. Ushahidi ni mafanikio ya sensa ya watu na makazi 2012.
 
Rosemary Mwakitwange, ni mchapa kazi Na MTU ambaye hupenda kuona matokeo ya kazi yake, Result Oriented, ni hayo tu wakuu
 
Ludovick Mwananzila ambae ni mkuu wa moa wa Tabora kwa sasa nae jembe huwa hana maslahi binafsi yeye kaaazi tu...alitolewa unaibu waziri kwa mizengwe ya kina pinda
 
Kumekua na tabia ya kuongezeana mda wa utumishi mara baada ya maafisa wa vyombo vya ulinzi muda wao wa utumishi unapomalizika. Hii hupelekea vijana wengi ambao ni wasomi kutopata nafasi za kuongoza vitengo mbalimbali katika kada hiyo.
Wana Jf, nyie mnalionaje swala hili.
 
Mi mwenyewe ni mchapakazi niliondolewa tu kwa mizengwe gate no 5 yaani nikirudishwa pale hayapiti makontena bila ushuru hata vile vikontena vya chakula vidogo lazima vilipiwe ushuru tunapoteza sana mapato eneo lile aisee
 
Ili kukwepa gharama kubwa za kuwalipa wakurugenzi wengi na gharama nyingine kwa hizi hospitali yaani MOI, MUHIMBILI, OCEAN ROAD HOSPITAL, TAASISI YA MOYO NA HOSPITALI YA BENJAMIN WILIAM MKAPA napenda kutoa ushauri wangu kwa Muheshimiwa JPM kuwa aziunganishe hizi hospitali 5 ziwe chini ya muhimbili national hospital na zilizobaki ziwe ni IDARA.

kama utakumbuka miaka ya nyuma hizo zilikuwa ni idara chini ya muhimbili lakini kuna baadhi ya watu waliamua kuandaa miswaada ambayo ilipitshwa bungeni na kuwa sheria na hivyo kujitenga. Wengi wa wanaoandaaa miswaada hiyo wanakuwa na lengo kuwa kama hii itakuwa taasisi basi fulani atakuwa Mkurugenzi hivyo mambo yatakwenda vizuri. Hii ilisababishwa na ile kasumba kama mtu akiwa mkurugenzi basi anaweza kuendelea kula katika nafasi hiyo mpaka anastaafu kama network yake ni nzuri.

ijulikane kuwa katika kila hospitali ina bodi, mkurugenzi mkuu mmoja na wakurugenzi wasaidizi zaidi ya 4 katika kila hospitali ambao wanatumia gharama nyingi.

Nashauri turudishe kama zamani Hospitali iwe moja yaani Muhimbili na wengine wawe wakuu wa Idara chini ya muhimbili.
 
Ni mwezi mmoja na siku tano tangia uapishwe kuwa kiongozi mkuu wa taifa letu sina budi kukupongeza kwa jinsi unavyofanya kazi kwa bidii wananchi tumeamasika na kuona kweli tunakiongozi shupavu na mwenye uchu wa kubadilisha nchi yetu ili tufike uchumi wa kati inapofika mwaka 2025.

Baada ya pongezi naomba nitoe maoni yangu kwenye swala hili coco beach . Mimi naona kuna ulazima liangaliwe kwa uangalifu na siyo kukurupuka. Ufukwe wa coco beach unaanzia masaki light house mpaka hotel ya sea cliff hotel. Hili ni eneo zuri sana la ufukwe, kumekuwa na mgogoro wa uliodumu kwa muda mrefu na sasa umeamuliwa na mahakama kuwa kampuni Q Consult iliyoshinda kandarasi wanaweza kuanza kuendeleza ufukwe huo. Mimi kama mwananchi wa kawaida sioni ubaya wa ufukwe kuendeleza na kuendeshwa kisasa ili utengeneze ajira kwa watanzania na watu wawe na sehemu safi na salama ya kupumzikia. Kama sheria zilifuatwa katika zabuni na kutoa kandarasi sioni kuna ubaya gani aliyeshinda kuanza kufanya kazi . kwasababu nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya sheria. kama palikua na uvunjifu wa kanuni na sheria basi watu waliousika wakamatwe na kufikisha katika vyombo vya sheria.

Napata hofu na hoja unayoijenga kuwa uwekezaji wa aina hii utafanya watu masikini washindwe kufaidia rasilimali za nchi yao. Hii ni hoja nyepesi kwasababu ni rahisi kwa serikali kuangalia ni vip mradi uweze ku accomodate watu wote kwa kusababu ya ukubwa wa ufukwe. mfano Jagwani beach (Mbezi Africana) kuna hoteli zimejipanga na pia public beach kubwa isiyo na kiingilio. Uwekezaji uliopo sasa hivi coco beach ni mdogo mno, unaajiri watu wachache kwa ajira zisizo endelevu, ufukwe hauna ata vivuli vya kutosha, hamna life gurd, hamna restaurant zakutosha zinazolipa kodi kwa ujumla ufukwe wa coco kwa hauna manufaa makubwa kwa uchumi na ustawi wa nchi.

Nashauri Mh Rais angalia maswala kama haya kwa umakini utengeneze uchumi imara kwa wawekezaji wakubwa wazawa na wadogo, lazima to co-exist hii ni nchi yetu sote. Pili tuanze kuangalia jinsi ya kuwa na njia ya nyingi ya kukuza uchumi , angalia visiwa vya Bahamas uwekezaji kwenye fukwe zao, ibiza (spain) uwekezaji katika leisure and recreation facilities katika kamji kadogo unaovuta ma milioni ya watu kila mwaka, Monaco (France) mifano ipo mingi . Tutumie vizuri fukwe zetu na tugawe vizuri vibali vya fukwe vigawiwe kwa umakini ili pawe na public beach na private beach kwa ajili ya uwekezaji. Hawa watalii wakifika Tanzania wakati wanasubiri kwenda kwenye buga za wanyama na kupanda milima wapate sehemu nzuri za kupumzika na za kutumia fedha zao , tusitegemee mbuga za wanyama tu .

Naamini unania ya dhati katika kukuza uchumi wa nchi hii . tukitumia fukwe vizuri tukaacha kugawa vibali vya fukwe hovyo hovyo kwa matumizi binafsi (matumizi ya ardhi) tukafanya sehemu kubwa ya bahari iwe sehemu ya uwekezaji makini basi tutainua uchumi wa nchi kwa watalii wa ndani na nje ya nchi. baadhi ya mikoa beach plots zinanyumba za udongo .
 
Engineer Mashiku P. M.

Yuko wizara ya kilimo ni mkimya sana, lakini mchapa kazi kuliko kawaida, hana makuu ni mweledi na mwadilifu hujawahi ambiwa.

Kama anahitaji watu wa kufanya nao kazi kwa kauli mbiu ya "hapa kazi tu", naam huyo ndiye saizi yake na hatajuta na wala Watanzania hawatajuta. Jamaa ni balaa wa kazi na utawala.

mkuu unamuongelea DD irrigation.? kama ndiye hakika hujakosea

na anaishi maisha ya kawaida sana hana makuu na jamii inayomzunguka inamkubali


nakumbuka alivokuwa mbeya watumishi wengi pale ofisini walitaka Kufanya naye kazi kabla hajaletwa wizarani, kuanzia madereva hadi watumishi wengine
 
mkuu unamuongelea DD irrigation.? kama ndiye hakika hujakosea

na anaishi maisha ya kawaida sana hana makuu na jamii inayomzunguka inamkubali


nakumbuka alivokuwa mbeya watumishi wengi pale ofisini walitaka Kufanya naye kazi kabla hajaletwa wizarani, kuanzia madereva hadi watumishi wengine


Haswaaaaaaaaaaaa, ni yule yule jamaa. Mchapakazi halafu ni kiongozi mzuri sana anayethamini watu na uwajibikaji wa kiwango. Hana kashfa wala makandokando.

Kwlei mimi nawachukia ccm lakini huyo jamaa, wakimsogeza, Magufuli atakuwa kapata jembe la kazi. Nilikuwa naye kwenye ziara moja na kila mtu alimkubali. Wageni wakasema, "Tanzania kuna watu wenye kila sifa ya kuleta maendeleo".
 
Umeme huku arusha.unakatwa tangu. Asubui mpaka saa 6 usiku ndiyo unarudishwa. Wanasema wanakata miti, sasa tunajiuliza iyo miti inakatwa mpaka usiku wa manane? Mh rais naomba ulimulike ilishirika la umeme kuna hujuma zinafanywa na mameneja fukuza kazi wote.
 
Watu watafanyaje kazitu. Wakati umeme hakuna? Maendeleo yatakujaje wakati umeme ni wa kuunga unga? Tanzania itakuwaje nchi ya viwanda wakati umeme hakuna mh miwa mtukufu rais? Safisha ili shirika kuanzia mkurugenzi mpaka mameneja wote. Ulisuke upya.
 
NI RAHISI KUWA RAIS WA TANZANIA KULIKO
KUWA BABA WA FAMILIA..
Ukiwa rais wa tanzania ni rahisi kuunganisha
wizara mbili harafu ukateua mawaziri wawili na
naibu waziri wao harafu ukawaambia watanzania
kuwa nmevunja wizara moja ili kubana matumizi
na bado watanzania wakashangilia kuwa ww ni
jembe..
Ukiwa baba wa familia yenye watoto wawili
huwezi kununua kaputula moja harafu ukampa
mmoja ukasema nmebana matumizi harafu
ukatarajia yule aliekoswa atashangilia, hiyo haipo
itakubidi uinunue na nyingne ili wote wafurahi...
Ukiwa rais wa Tanzania unaweza ukawaambia
watu kuwa unatumbua majipu harafu ktk wizara
hiyo yenye matatizo unawafukuza watu wa chini
harafu katibu wake ukasema utampangia kazi
nyingne na bado wananchi wakashangilia ww ni
jembe..
Ukiwa rais wa tanzania unaweza kumfuta kazi
mkurugenzi wa TRA kwa kushindwa kukusanya
mapato pamoja na mambo mbali mbali lakini
mawaziri wa fedha waliokuwa wanahusika kipindi
hicho ukawapangia tena wizara zingine za kilimo
na bado wananchi wakashangilia wewe ni
mtumbua majipu..
Ukiwa rais wa tanzania unaweza ukaenda
bandarini ukagundua kontena zaidi ya 2500
hazikulipiwa ushuru harafu ukavunja bodi yote
bandari harafu mawaziri waliokuwepo enzi hizo
tena wakitumia bilioni 1.9 kwa kikao cha siku
moja ukawapa tena uwaziri wa sheria na katiba
na wengne ukawafanya kuwa manaibu speaker na
bado watanzania wakashangilia kuwa unatumbua
majipu kisawasawa..
Ukiwa rais wa Tanzania unaweza ukaenda TRL
ukawafukuza watumishi wengne kwamba
wametafuna bilioni 16 lakini aliekuwa waziri wao
alienunua mabehewa fake tena kinyume cha
utaratibu ukamzawadia uwaziri na bado wana wa
nchi wakasema wewe ni rais wa dunia tena
watakuita hakunaga wao..
Ukiwa rais wa Tanzania mtu anaweza kusimama
bungeni kwa nguvu kubwa huku amebeba
makaratasi lukuki ya uongo akitetea wizi wa IPTL
ktk akauti ya ESCROW kwamba hapakuwa na
fedha za umma wala hakuna wizi wowote pamoja
na kwamba CAG na TRA wamesema kuna fedha
za umma na mtetezi huyo akajiuzuru na wengne
wakafutwa kazi harafu wewe mtumbua majipu
bado ukaja ukampa tena uwaziri tena ktk wizara
hiyo hiyo .. pamoja na kwamba alifanya uzembe
mkubwa na uongo tena ndani ya bunge tukufu na
bado watanzania wakakubeba juu juu kwamba
wewe ni jembe nk.
Huo usanii unaweza kuufanya kwa watanzania tu
tena ukiwa rais na watu wake wakakushangilia.
lakini ktk familia kama wewe ni baba huwezi
kufanya usanii kama hakuna chakula ndani
utakinunua tu ili familia ile, na kama mkeo hana
mavazi utayanunua ili avae tena hapo ni bora
wewe uwe na suruali moja lakini mkeo apendeze
tu ... na kama watoto wanahitaji elimu na wewe
baba yao upo huwezi kufanya usanii wa
kuwaeleka kuleana kwamba wazazi wao ni
marehemu. utawapeleka shule tu na ada utalipa
mwenyewe na kama utafanya usanii wa hivyo
siku wakiwa wakubwa na wakajuwa watakukataa.
Kwa hiyo jamani mm naona kuwa baba wa
familia ni kazi ngumu zaidi kuliko kuwa rais wa
Tanzania ....
Hata rais wa kwanza wa Kenya aliwahi kusema
mm naongoza watu waliolala ila ipo siku
wakiamka wataniuliza maswali . lakini jirani
yangu anaongoza wafu ambao hawawezi kuamka
na kuhoji chochote..
Naomba kuwasirisha ........
 
Mheshimiwa Raisi, nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya. Umewadhihirishia Watanzania kwamba penye nia hakuna linaloshindikana. Umethibitisha kutembea katika maneno yako "HAPA KAZI TU".

Ninaimani na baraza ulilolichagua, na ninaelewa kwa umakini ulioouonyesha kwa Muda mfupi tangu ushike madaraka, bila shaka umezingatia sana ufanisi wa kazi, sifa na malengo ya taifa kwa awamu yako hii.

Kwa kuzingatia hili, ninakushauri WIZARA YA UJENZI NA MIUNDOMBINU AMBAYO WEWE UMEKUWA KINARA WAKE KWA MIAKA MINGI, umteua Engineer Mashiku M. P. aliyeko umwagiliaji.

Huyu mtu ni mchapa kazi wa kiwango cha juu na ambaye anaweza kuwa miongoni mwa Watanzania wachache wanaopashwa kuigwa.

Ni mtulivu na kiongozi makini asiye na makundi, majungu wala makuu. Yeye ni 'HAPA KAZI TU".

Ni mwadilifu na hajawahi kuhusishwa katika kashfa yoyote. Ni mtu asiyekubali hazi iharibike na ni mtu ambaye ni results oriented, mjenga team ya kazi, anasimamia uwajibikaji na results oriented.

Hana mbwembwe wala haonei mtu. Ni kiongozi na Mhandisi mzuri sana.

Bila shaka Mheshimiwa raisi, kwa kumteua Engineer Mashiku M.P, kuwa waziri wa Ujenzi, hutakuja kujuta, watanznia hawatajuta na zaidi sana uteuzi huu utaimarisha kazi na viwango vya ufanisi wa kauli mbiu yako ya "HAPA KAZI TU".

Engineer huyu ni miongoni mwa wahandisi wachache sana wa kuigwa duniani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom