Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kampeni zimeanza!

Mkuu, huyu Mhandisi hata mimi namfahamu. Pia kuna Sauli hapa naye anamfahamu. Hata wewe ungemfahamu, bila shaka kwa kasi na mrengo wa awamu hii inayotegemewa kutokuwa na matabaka, inayojali kazi kwa ustawi wa taifa, ungeungana na Dasha pamoja na mimi kumshauri raisi amteue tu.

Muda wa siasa umekwisha, hakuna sababu ya kupigia kampeni majitu ma bogus yaliyojaa majungu na uzembe uliolifikisha taifa letu hapa.

Lakni kwa huyu jamaa, hata wewe utamkubali tu kwa kazi.

Ninaungana na Dasha. Apewe tu, pamoja na kwamba ccm siwapendi, lakini kwa Mtanzania kama huyu, nikileta upinzani nitakuwa namkosea Mungu na Taifa langu. Anafaa sana.
 
Last edited by a moderator:
Kwa maoni yangu,Dr Bana anakielewa vizuri chama cha mapinduzi na amekua akikisemea vizuri.

Lakini pia kwa usomi alionao atakuwa mbunifu mzuri na atafaa sana kuwa katibu mwenezi na itikadi wa CCM

Naomba kuwasilisha.
 
Mheshimiwa Raisi, nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya. Umewadhihirishia Watanzania kwamba penye nia hakuna linaloshindikana. Umethibitisha kutembea katika maneno yako "HAPA KAZI TU".

Ninaimani na baraza ulilolichagua, na ninaelewa kwa umakini ulioouonyesha kwa Muda mfupi tangu ushike madaraka, bila shaka umezingatia sana ufanisi wa kazi, sifa na malengo ya taifa kwa awamu yako hii.

Kwa kuzingatia hili, ninakushauri WIZARA YA UJENZI NA MIUNDOMBINU AMBAYO WEWE UMEKUWA KINARA WAKE KWA MIAKA MINGI, umteua Engineer Mashiku M. P. aliyeko umwagiliaji.

Huyu mtu ni mchapa kazi wa kiwango cha juu na ambaye anaweza kuwa miongoni mwa Watanzania wachache wanaopashwa kuigwa.

Ni mtulivu na kiongozi makini asiye na makundi, majungu wala makuu. Yeye ni 'HAPA KAZI TU".

Ni mwadilifu na hajawahi kuhusishwa katika kashfa yoyote. Ni mtu asiyekubali hazi iharibike na ni mtu ambaye ni results oriented, mjenga team ya kazi, anasimamia uwajibikaji na results oriented.

Hana mbwembwe wala haonei mtu. Ni kiongozi na Mhandisi mzuri sana.

Bila shaka Mheshimiwa raisi, kwa kumteua Engineer Mashiku M.P, kuwa waziri wa Ujenzi, hutakuja kujuta, watanznia hawatajuta na zaidi sana uteuzi huu utaimarisha kazi na viwango vya ufanisi wa kauli mbiu yako ya "HAPA KAZI TU".

Engineer huyu ni miongoni mwa wahandisi wachache sana wa kuigwa duniani.


Watanzania tulihitaji mabadiliko. Hii ni kutokana na taifa kupoteza dira na taswira ndani na nje ya mipaka yake. Tumeshuhudia teuzi nyingi zikifanyika wa misingi ya undugu na nasaba pasipokujali tija kwa taifa.

Ni jambo la kushangaza kwamba watu kama hawa wanaachwaje kuteuliwa na badala yae wanapewa wizara kina Mulugo. Hii ni inferiority complex na lack of competence ya watawala na woga wa kufanya kazi na wasomi wenye weledi na uadilifu.

Ninaungana na mtoa mada awaangalie watu kama hawa ambao mfumo uliopita haukuhitaji mchango wao ambao taifa linauhitaji.

Huyu mtu kwa sifa hizi sioni sababu kwa nini Mh Magufuli asimpe wizara, badala yake akomae na kina Nnauye wapiga makelele bila lolote la maana.
 
Moja ya sifa kuu ya rais Magufuli, ni hatua alizochukua kubana matumizi. Hatua alizochukua zimewavutia watu ndani na nje ya nchi, hatua kama, kupunguza safari za nje, kuzuia vikao kufanyika hotelini, kupunguza posho, kufuta sherehe za uhuru, kukataa semina elekezi,vikao kuandaliwa kwa bajeti ndogo sana kama alichokaa na wabunge Dodoma na kile cha makatibu wakuu,kupunguza semina za nje ya nchi,kuzuia waheshimiwa kusafiri kwa ndege daraja la kwanza, na hivi punde kuunganisha wizara na kupunguza baraza la mawaziri n.k

Nafikiri sasa ni wakati muafaka kutoa mapendekezo ambayo tunadhani yakitekelezwa yatapunguza matumizi wakati huohuo hayaathiri ufanisi wa kazi. Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ambayo kwa mtazamo wangu yakitekelezwa yatapunguza matumizi na kuongeza ufanisi.

  1. Kutengua na kufuta kabisa, mikoa mipya,wilaya mpya na kata mpya zilizoanzishwa kisiasa. Mfano mkoa mpya wa Songwe
  2. Katika kila wilaya kuna maafisa elimu wawili,shule ya msingi na sekondari,abakie mmoja tu.Maafisa taaluma ndio wawe wawili
  3. Kila wilaya kuna viongozi wakuu watatu,mkuu wa wilaya,mkurugenzi na meya.Wakati umefika wa kumwondoa mmoja kati ya mkurugenzi wa wilaya na mkuu wa wilaya
  4. Uwepo wa wakaguzi wa shule na waratibu elimu kata ni matumizi mabaya ya pesa. Waratibu elimu kata waunde jopo la wakaguzi wa shule,kitengo cha ukaguzi wa shule kifutwe.
  5. Sitting allowance zote zifutwe,wanasemina walipwe night pekee yake
  6. Malipo ya overtime yafutwe

Hayo ni kwa mtazamo wangu, kama kuna jambo unafikiri likifanyika litaisaidia serikali kubana matumizi,basi liweke hapa tulijadili,hata kama lilijadiliwa huko nyuma si vibaya kujikumbusha. Huenda wahusika watapitia hii clip na kuyatafakari mapendekezo yetu
 
Sasa ni mwezi na masiku kadhaa tangu umeingia ikulu na umefanya mambo mengi ambayo yamewakuna wananchi wa Tanzania na hata nje Tanzania.
Kitu ambacho bado kinanipa shida mimi binafsi nadhani hata wananchi wenzangu wataniunga mkono ni kuhusu mgao wa umeme.

Imekuwa ni mazoea ya kampuni kukata umeme bila mpangilio na mara nyingine kutwa mzima kwa kisingizio cha aidha kubadilisha miondo au kukata miti jambo halikubaliki hata kidogo.

Katika hutuba yako ya ufunguzi wa bunhe ulieleza tatizo la kukatika umeme na ukaeleza baadhi mbinu ambazo hutumika ili maji yasijae waendelee kutunyanyasa kwa mgao.

Wakati umefika tuahitaji serikali ya magufuli ya viwanda lakini bila ya umeme haitawezekana.
 
Sasa ni mwezi na masiku kadhaa tangu umeingia ikulu na umefanya mambo mengi ambayo yamewakuna wananchi wa Tanzania na hata nje Tanzania.
Kitu ambacho bado kinanipa shida mimi binafsi nadhani hata wananchi wenzangu wataniunga mkono ni kuhusu mgao wa umeme.

Imekuwa ni mazoea ya kampuni kukata umeme bila mpangilio na mara nyingine kutwa mzima kwa kisingizio cha aidha kubadilisha miondo au kukata miti jambo halikubaliki hata kidogo.

Katika hutuba yako ya ufunguzi wa bunhe ulieleza tatizo la kukatika umeme na ukaeleza baadhi mbinu ambazo hutumika ili maji yasijae waendelee kutunyanyasa kwa mgao.

Wakati umefika tuahitaji serikali ya magufuli ya viwanda lakini bila ya umeme haitawezekana.

TANESCO YAFANYA MAKUBWA KUBORESHA SEKTA YA UMEME NCHINI
1.Kuongeza Uzalishaji Umeme
Kwa kuzingatia ukuaji wa sekta ndogo ya umeme hapa nchini na mahitaji makubwa ya umeme yanayoongezeka kwa kasi, Serikali iliweka mikakati mahsusi kuongeza uzalishaji wa umeme hadi kufikia MW 2,780 Mwaka 2015/16. Katika kipindi cha 2005 ? 2015, Serikali ya Awamu ya Nne ilifanikiwa kuongeza uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme katika Gridi ya Taifa kutoka MW 891 zilizokuwepo mwaka 2005 hadi kufikia MW 1,501.24 mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 68.5. Mpaka kufikia Julai, 2015 uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme katika Grid ya Taifa ulipungua na kufikia MW 1,246.24 kutokana na kukoma kwa baadhi ya mikataba ya wazalishaji binafsi ambao wamekuwa mzigo kwa Shirika kutokana na gharama kubwa. Kuongezeka kwa uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme katika Gridi ya Taifa kwa kipindi cha Awamu ya Nne kutokana na utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme. Juhudi zilizochangia mafanikio hayo ni pamoja na:
(i)Kukamilika kwa Mtambo wa kuzalisha umeme MW 100 ? Ubungo I: Mtambo huo upo katika eneo la TANESCO-Ubungo Dar es Salaam. Mtambo huu una uwezo wa kufua umeme wa MW 100 kwa kutumia gesi asilia na ulifunguliwa rasmi na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Novemba, 2008.
(ii)Kukamilika kwa Ujenzi wa Mtambo wa Kufua Umeme, MW 45 ? Tegeta: Ujenzi wa mtambo huo unaotumia gesi asilia una uwezo wa kufua umeme wa MW 45 ulikamilika na kuanza kufua umeme Mwezi Desemba, 2009.
(iii)Kukamilika kwa Ujenzi wa Mtambo wa Kufua Umeme, MW 105 ? Ubungo II: Mtambo huu unatumia gesi asilia kufua umeme wa MW 105, upo katika eneo la TANESCO ? Ubungo Jijini Dar es Salaam na ulizinduliwa rasmi na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Mh. Prof. Sospeter M. Muhongo Mwezi June, 2012.
(iv)Kukamilika kwa Mtambo wa kuzalisha umeme MW 60 ? Mwanza: Ujenzi wa mtambo huo umekamilika na ulizinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 06 Septemba, 2013. Mtambo huu umesaidia kuboresha upatikanaji wa umeme na kuimarisha gridi ya Taifa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
(v)Kukamilika kwa Mradi wa Umeme wa Somanga Fungu, MW 7.5: Mitambo ya kufua umeme wa MW 7.5 kwa kutumia gesi asilia iliyopo Somanga Fungu mkoani Lindi ilizinduliwa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Agosti, 2010. Mitambo hiyo inafua umeme unaosambazwa katika miji ya Bungu, Kibiti, Kilwa Kivinje, Kilwa Masoko, Kindwitwi, Muhoro, Nangurukuru, Somanga, Tingi, Utete, Nyamwange, maeneo ya Njia Nne na Hospitali ya Mchukwi.
(vi)Mchango wa Wazalishaji Wadogo wa Umeme katika Gridi ya Taifa: Katika kipindi cha 2005 hadi 2015, wazalishaji wadogo wa umeme waliingia mikataba ya kuuziana umeme na TANESCO ambapo umeme wa MW 8 ununuliwa. Wazalishaji hao ni ni TANWAT ? MW 1; TPC ? MW 3; na Mwenga Mini Hydro ? MW 4.
(vii)Kuboresha Huduma ya Umeme Katika Maeneo yaliyopo Nje ya Gridi ya Taifa: Katika kipindi cha 2005 hadi 2015, utekelezaji wa mipango mbalimbali ya ukarabati na ufungaji wa mitambo mipya ya kufua umeme kwa kutumia mafuta katika maeneo ambayo bado hayajaunganishwa katika gridi ya Taifa imefanyika. Ukarabati wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta ulifanyika kwenye vituo vya Mpanda, Kigoma, Masasi, Mafia, Songea, Tunduru, Ngara na Biharamulo. Aidha, Serikali kupitia TANESCO ilinunua mitambo mipya 19 ya kufua umeme kwa kutumia dizeli iliyofungwa katika vituo vya Kasulu (1.25 x 2), Kibondo (1.25 x 2), Kigoma (1.25 x 5), Loliondo (1.25 x 4), Namtumbo (0.32 x 1), Songea (1.9 x 1) na Sumbawanga (1.25 x 4). Mitambo hiyo mipya iligharimu EURO milioni 35.94 sawa na Shilingi bilioni 57.5. Pia kuna wazalishaji binafsi waliowekeza katika maeneo yaliyopo nje ya gridi ambao ni Ngombeni ? MW 1.4 na Andoya Hydro MW 0.5.
(viii)Kukamilika kwa Mradi wa Mawengi wenye Uwezo wa Kuzalisha kW 300 kwa Kutumia Maporomoko Madogo ya Maji: Mradi huo uliopo Wilayani Ludewa ulizinduliwa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Novemba, 2011, ambapo hadi kufikia Mwezi Octoba, 2014 zaidi ya kaya 1,153 zilikuwa zimeunganishiwa umeme.
Kukamilika kwa miradi hiyo kumewezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini na kufanikisha kuondoa mgawo wa umeme hususan kuanzia Mwaka 2012 na hivyo kuboresha ufanisi wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Pamoja na kukamilika kwa miradi hiyo, pia kumekuwepo na mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishazi wa umeme kwenye Gridi ya Taifa na je ya Gridi ya Taifa kama ifuatavyo;
(i)Utekelezaji wa Mradi wa Kinyerezi I ? MW 150 kwa Kutumia Gesi Asilia: Serikali imefanya juhudi kupunguza utegemezi wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta ambayo ni ghali. Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuamua kwa dhati na kwa kutumia fedha za Watanzania kutekeleza mradi wa Kinyerezi - I (MW 150). Mradi huo unaojumuisha ujenzi wa njia za umeme za msongo wa kV 220 (Kinyerezi - Kimara) na kV 132 (Kinyerezi - Gongolamboto) utatumia gesi asilia na utagharimu Dola za Marekani milioni 183.30, sawa na Shilingi bilioni 293.28. Utekelezaji wa Mradi huo ulianza Mwezi Januari, 2013 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwezi Agosti, 2015.
(ii)Mradi wa kupeleka umeme miji ya Mpanda, Ngara na Biharamulo (ORIO): Mradi huu unajumuisha ufungaji wa jenereta mbili (2) zenye uwezo wa MW 1.25 katika kila mji, ukarabati wa njia za umeme zilizoharibika na ujenzi w njia mpya za umeme. Awamu ya kwanza ya mradi (development) ilianza September, 2010; na wamu ya pili ya mradi ambayo ni Utelelezaji, Uendeshaji na Matengenezo (Implementation and Operation & Maintenance Phase) ilianza Septemba, 2012. Hadi sasa mchakato mzima wa tenda kwa ajili ya kuwapata wakandarasi kwa ajili ya utelezaji wa mradi huu umekamilika na kazi ya utekelezaji ilianza mwezi Oktoba, 2013. Pia kumekuwa na mafunzo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na mafunzo ya uongozi wa miradi.
(iii)Mradi wa Kufua Umeme Rusumo na Njia ya Kusafirisha Umeme: Mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa MW 80 kwa kutumia maji. Mpaka sasa uchambuzi yakinifu umekamirika, Ripoti ya mazingira kwa upande wa usambazaji kutoka BENACO mpaka mpakani Rusumo tayari imekamirika na kibari cha kuendeleza mradi kinasubiriwa kutoka NEMC. Mchakato wa kupata njia ardhi kwa ajili ya njia ya usafirishia umeme toka Rusumo mpaka Nyakanazi ya kV 220 tayari umeanza.
(iv)Mradi wa Kufua Umeme Kakono Hydro MW 87: Mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa MW 87 kwa kutumia maji. Mpaka sasa uchambuzi yakinifu umekamilika, Ripoti ya mazingira ya kituo cha kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme toka Kakono hadi Kyaka ipo tayari na imewasilishwa NEMC Mwezi Mei, 2015 kwa ajili ya kupata kibali ya kuendeleza mradi. Gharama ya mradi inakadiriwa kuwa Dola za Kimarekani Milioni 379.4 na unatarajiwa kukamilika 2019.
1Kujenga na Kuimarisha Njia za Usafirishaji na Usambazaji Umeme
Katika kipindi cha kuanzia 2005 ? 2015, juhudi kubwa zimefanyika kuimarisha njia za usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kuwezesha nishati hiyo kuwafikia watumiaji kwa ubora na kwa wakati wote na kuweza kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme nchini. TANESCO imefanya ukarabati na kujenga miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme. Ukarabati huu umefanyika na unaendelea kufanyika katika mikoa mbalimbali inayopata umeme kupitia Gridi ya Taifa. Kazi hii inafanyika kwa fedha za ndani na kwa ufadhili kutoka wahisani mbalimbali wakiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Shirika la Marekani linalotoa??? misaada kwa??? nchi maskini (MCC), Korea Kusini na JICA. Miradi hiyo ni pamoja na ifuatayo;
(i)Kukamilika kwa Mradi wa Kuboresha Kituo cha Taifa cha Kusimamia Mfumo wa Umeme wa Gridi (National Grid Control Cetre): Mradi huu ulianza mwaka 2009 na kukamilika mwaka 2012. Mradi huu ulihusisha ubadilishaji wa mfumo wa zamani SCADA na ufungwaji wa mfumo mpya wa SCADA/EMS. Mradi pia ulihusisha ununuzi, ufungwaji na majaribio ya ?National Grid Control Center (GCC) ? Ubungo, DSM na ufungwaji wa vifaa vingine viambatanavyo na mfumo huo katika nchi nzima. Gharama za Mradi huo ni Euro milioni 3.04 na Dola za Marekani 622,394 sawa na jumla ya Shilingi bilioni 7.4.
(ii)Mradi wa kuboresha mifumo na upatikanaji wa umeme katika Jiji la Dar es Salaam (TEDAP na Finish Project): Mradi wa TEDAP unahusisha ujenzi wa njia??? msongo wa 132kV ya kilomita 7 kutoka Ubungo ? Makumbusho na kituo cha kupoozea umeme cha Makumbusho cha 132/33kV chenye uwezo wa 2 X 45MVA. Mradi huu umekamilika na kuondoa tatizo la umeme mdogo ?Low Voltage? na kukatika katika katika maeneo ya Wilaya ya Kinondoni. Pia ulihusisha ujenzi wa vituo vipya vya kupoozea umeme maeneo ya katikati ya jiji, Kipawa, Mburahati, Mikocheni na Oysterbay, ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme maeneo ya Chang?ombe, Kariakoo, Kurasini, Mbagala, Ubungo na ujenzi wa njia za umeme za kilomita 51.7 za msongo wa kilovolti 132 na kilomita 83 za msongo wa 0.4kV unaotegemewa kukamika ifikapo Mwezi Disemba, 2015.
Mradi wa Finish? umehusisha kujenga njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi ya 132kV kutoka Ilala hadi City Centre Kujenga kituo cha kupoozea umeme cha 132/33/11kV??? chenye uwezo wa 2x45MVA, ujenzi wa njia ya umeme chini ya ardhi kwa ajili ya kuunga kituo cha Kariakoo ? Railway ? Sokoine na kituo cha zamani cha City Centre, kuanzisha kituo cha kuongozea mifumo ya usambazaji umeme katika msongo wa kV 33 na kV 11 (distribution SCADA). Mradi huu ulishaanza na unategemewa kukamilika ifikapo Mwezi Septemba, 2015.
(iii)Ujenzi wa Njia Mpya ya Kupeleka Umeme Zanzibar ya Msongo wa kV 132 na Kupeleka Umeme Pemba kutoka Tanga ya msongo wa kV 33: Mradi wa kupeleka umeme Zanzibar ulizinduliwa rasmi tarehe 10 Aprili 2013 na umeboresha usafirishaji umeme wa uhakika katika visiwa vya Zanzibar. Mradi ulihusisha ujenzi wa waya wa majini (Submarine cable) wa njia ya kilomita 39 ambao ulimalizika mwanzoni mwa mwezi Machi 2013. Pia waya wa juu (Overhead line) wa njia ya kilomita 37 ambao ulimalizika mwishoni mwa mwezi February 2013.??? Pia kukamilika??? mradi wa kupeleka umeme Pemba ambao??? ulizinduliwa rasmi tarehe 9 Mei, 2013 na umeboresha upatikanaji umeme wa uhakika katika kisiwa cha Pemba. Kazi hii??? ilihusisha kutandaza waya wa majini (submarine cable) yenye urefu wa kilomita 90.
(iv)Kuimarisha mfumo wa njia za usafirishaji na usambazaji katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro (TEDAP): Mradi huu ulihusisha ufungwaji wa Transformer mpya katika vituo vya kupoozea umeme vya Boma Mbuzi, Mt. Meru, Kiltex, Njiro B, Sakina, Themi, Trade School na Unga Ltd. Pia ujenzi wa njia za usambazaji wa umeme katika miji ya Arusha kilomita 143 na Kilimanjaro kilomita 25, ukarabati??? wa kituo cha kupoozea umeme cha Kiyungi na ujenzi wa njia ya usafirishaji ya umeme ya kilomita 70 ya msongo wa kilovolti 132 kutoka Kiyungi ? Njiro, Ujenzi wa kituo kipya cha kupoozea umeme cha KIA cha 132/33kV na ujenzi wa njia ya usafirishaji ya msongo wa 66kV Kiyungi (TPC) Moshi hadi Makuyuni Himo. Mradi huu tayari umekamilika.
(v)Mradi wa Makambako - Songea kV 220: Mradi huo unahusisha ujenzi wa njia yenye urefu wa kilomita 250 na? kujenga vituo vya kupoozea umeme 220/132/33kV vya Makambako, Madaba na Songea. Mchakato wa kutafuta wakandarasi wa mradi wa ujenzi wa njia kuu pamoja na vituo vya kupoozea? umeme umekamilika na taarifa ya tathmini imewakilishwa kwenye bodi ya zabuni kwa ajili ya kupata kibali hatimaye ipelekwe SIDA; na kujenga kilomita 900 za njia za usambazaji katika miji ya Makambako, Njombe, Ludewa, Songea, Namtumbo, Mbinga, Mbamba Bay, na vijiji vilivyopo karibu na njia ya kusafirishia umeme. Mchakato??? wa kutafuta wakandarasi wa mradi? wa ujenzi wa njia za kusambaza umeme mijini na vijijini??? umekamilika na? umepata kibali kutoka bodi ya dhabuni. Umepelekwa SIDA kwa ajili ya kupata kibali cha kuingia??? mkataba na mkadarasi aliyeshinda. Wakandarasi wa mradi huu tayari wameanza kazi za awali katika eneo la mradi na kazi inaendelea. Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Sweden kupitia Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida) kwa kiasi cha Swedish Kroner milioni 500, sawa na Shilingi bilioni 112. Kwa upande wa usambazaji, mradi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 5 na mradi kwa ujumla unatarajia kukamilika mwaka 2017.
(vi)Mradi wa Iringa - Shinyanga kV 400 (Backbone): Mradi huu ni wa kuimarisha Gridi ya Taifa ambapo kukamilika kwake kutapunguza upotevu wa umeme na kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya Kanda ya Kaskazini Magharibi. Taratibu za kumpata mtaalamu mshauri wa masuala ya ufundi, sheria na fedha alishapatikana na ameanza kazi; taratibu za manunuzi ya vifaa vya usambazaji umeme (cables na waya) zimekamilika na vifaa vimeanza kuwasili na??? mtaalamu wa usimamizi wa mradi ameanza kazi. Vilevile, Serikali kupitia TANESCO imeanza kulipa fidia katika maeneo ya mradi. Aidha, Mshauri wa mradi, Kampuni ya Fitchner ya Ujerumani anaendelea na kazi ya kusanifu njia ya usafirishaji umeme na vituo vya kupozea umeme. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 650, sawa na Shilingi bilioni 1,040. Mradi unatarajiwa kukamilika Mwaka 2016.
(vii)Mradi wa Dar es Salaam ? Chalinze ? Tanga ? Arusha kV 400: Serikali kupitia TANESCO imedurusu usanifu wa mradi (redesigning) ili uanzie Dar es Salaam kupitia Chalinze hadi Arusha badala ya kuanzia Morogoro. Mwezi Juni, 2012 TANESCO na mkandarasi Kampuni ya TBEA ya China walisaini mkataba wa marekebisho (EPC addendum), kwa lengo la kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka Dar es Salaam. Mradi huu utatekelezwa kwa mkopo? wa takribani Dola za Marekani milioni 770, sawa na Shilingi bilioni 1,232 kutoka Benki ya Exim ya China na unatarajiwa kukamilika mwaka 2017.
(viii)Mradi wa ujenzi wa njia ya umeme ya kV 220 ya Bulyanhulu ? Geita ? Nyakanazi: Mwezi Januari, 2011 Serikali ilisaini mkataba wa mkopo na Taasisi ya fedha ya BADEA ya Misri na OFID ya Saudi Arabia. Lengo ni kutekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya umeme kV 220 kutoka Bulyanhulu hadi Nyakanazi kupitia Geita. Kazi ya kuandaa zabuni za kandarasi za ujenzi ilikamilika mwezi Juni, 2012. Maeneo kwa ajili ya kujenga vituo vya kupoozea umeme tayari yamepatikana na hatua za kuanza kuwalipa wananchi walioathirika na mradi zipo katika hatua za mwisho. Mradi utagharimu Dola za Marekani milioni 53, sawa na Shilingi bilioni 84.8 na unatarajiwa Mwaka, 2017.
(ix)Mradi North ? West Grid kV 400: Serikali imeamua kubadilisha msongo wa njia hiyo ya kusafirisha umeme kutoka kV 220 hadi kV 400 kwa lengo la kuimarisha??? mfumo na upatikanaji wa umeme katika Mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Mbeya, Rukwa na Shinyanga ili kukidhi matarajio ya shughuli mbalimbali za kiuchumi katika maeneo hayo. Maombi ya mkopo yamewasilishwa katika Benki ya Exim ya China kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 259.2 na unatarajiwa kukamilika Mwaka, 2018
(x)Mradi wa electricity ? V: Mradi huu ulitekelezwa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na ulihusisha usambazaji wa umeme katika vijiji, miji midogo na Makao Makuu ya Wilaya katika Mikoa ya Geita (Bukombe), Mwanza (Magu na Kwimba) na Simiyu (Bariadi) na kukarabati vituo vikubwa vya kupozea umeme kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Arusha.??? Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 31, sawa na Shilingi bilioni 49.6. Mradi umehusisha ujenzi wa km 480 wa njia za kilovolti 33, km 251 wa njia za volti ndogo (0.4kV) na ufungaji wa transifoma 109 za kilovolti 33/0.4 na uwezo wa kVA 50 hadi 315 juu ya nguzo; ufungaji wa taa za barabarani na kuunganisha wateja wapatao 8,600 katika mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga na Geita;??? ukarabati wa vituo vya kupozea umeme. Kuongeza Transfoma ya mbili yenye uwezo wa 33/11kV, 15MVA; kubadilisha Switchgear zote za nje za 33kV na 11kV na kuweka za ndani pamoja na kuongeza njia za kusambaza umeme kwa wateja; kuimarisha mfumo wote wa umeme ndani ya kituo; kubadilisha Transifoma ya 33/11kV, 15MVA iliyoungua pamoja na kubadilisha kizima umeme (CB); kuongeza Transifoma 2 za 132/33kV, 50MVA; kurefusha switchgear ya 132kV na njia nyingine ya kupeleka umeme wa 132kV katika kituo cha Kiyungi; Kujenga switchgear mpya ya 33kV yenye njia zaidi ya kusambaza umeme na kuweka mfumo mpya wa kidigitali wa kuendesha kituo na kusimamia uzimaji na uwashaji. Mradi huu unategemea kukamilika ifikapo Mwezi Septemba, 2015.

(xi)Mradi wa Kujenga Njia za kusambaza Umeme:
Mradi huu unahusu ujenzi wa njia za msongo wa kV 33, kV 11 na kV 0.4 kwa ajili ya kusambaza umeme katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe na Tanga. Jumla ya kilomita 1,068 kati ya kilomita 1,335 zimekamilika za njia ya kV 33, kV 11, na kilomita 1,094.4 kati ya kilomita 1,368 zimekamilika kwa njia za kV 0.4. Sehemu ya miradi iliyokamilika kwa Mkoa wa Dodoma ilihusisha jumla ya vijiji 46 katika Kijiji cha Mkoka, Wilayani Kongwa.
(xii)Mradi wa Kujenga Njia ya Pili ya Umeme kutoka Dar es Salaam kwenda Unguja: Mradi huu ulihusika na ujenzi wa njia ya umeme ya kV 132 kutoka Ubungo hadi Ras-Kilomoni na utandazaji wa nyaya za umeme chini ya bahari kutoka Ras-Kilomoni hadi Mtoni ? Unguja.. Gharama za mradi huo ni Dola za Marekani milioni 50, sawa na Shilingi bilioni 80 na tayari umekamilika.
(xiii)Mradi wa Kuunganisha Gridi ya Taifa na Gridi za nchi nyingine: Upembuzi yakinifu wa mradi wa kuunganisha Gridi ya Taifa na gridi za nchi za Zambia na Kenya (ZTK project) ulikamilika kwa upande wa Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Norway. Aidha, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na JICA zimekubali kufadhili utekelezaji wa mradi huo katika kipande cha Singida hadi Namanga. Fedha zinaendelea kutafutwa kwa ajili ya utekelezaji wa sehemu ya mradi kutoka Kabwe hadi Mbeya.??? Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha biashara ya umeme kati ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki na Afrika ya Kusini. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 642. Mradi huu unatarajiwa kukamilika 2018.
 
sasa ni mwezi na masiku kadhaa tangu umeingia ikulu na umefanya mambo mengi ambayo yamewakuna wananchi wa tanzania na hata nje tanzania.
Kitu ambacho bado kinanipa shida mimi binafsi nadhani hata wananchi wenzangu wataniunga mkono ni kuhusu mgao wa umeme.

Imekuwa ni mazoea ya kampuni kukata umeme bila mpangilio na mara nyingine kutwa mzima kwa kisingizio cha aidha kubadilisha miondo au kukata miti jambo halikubaliki hata kidogo.

Katika hutuba yako ya ufunguzi wa bunhe ulieleza tatizo la kukatika umeme na ukaeleza baadhi mbinu ambazo hutumika ili maji yasijae waendelee kutunyanyasa kwa mgao.

Wakati umefika tuahitaji serikali ya magufuli ya viwanda lakini bila ya umeme haitawezekana.

mkuu huku arusha. Umeme unakatwa saa kumi na moja alfajiri, unarudishwa saa 6 usiku. Ni shiida watu wamechoka na hii tanesco wanasingizia kukata miti. Sasa tunajiuliza iyo miti inaanzakukatwa usiku wa manane? Magufuli zinduka tanesco imejaa majambazi na waujumu uchumi.
 
mkuu huku arusha. Umeme unakatwa saa kumi na moja alfajiri, unarudishwa saa 6 usiku. Ni shiida watu wamechoka na hii tanesco wanasingizia kukata miti. Sasa tunajiuliza iyo miti inaanzakukatwa usiku wa manane? Magufuli zinduka tanesco imejaa majambazi na waujumu uchumi.



SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

Maelezo kuhusu Hali ya Umeme kwa baafhi ya Maeneo Mkoa wa Arusha.

Shirika la Umeme linapenda kueleza kile kinachoendelea mkoani Arusha kama ifutavyo; Eneo la Olasiva, Kwa kuanzia tunamalizia, mradi wa Olasiti Meckson school wiki hii. Hivyo wateja wa eneo Hilo watapata umeme mzuri. Pia miradi wa Sanawari Kati na shangalai uko kwenye hatua za mwisho kufikia tarehe 15.12.2015 itakuwa imekamilika. Mradi wa kuboresha, huduma Olasiva uko 40% hivyo mwisho wa mwezi huu, tunaimani kuukamilisha.

Kumalizika kwa miradi hapo juu ambayo tayari imeanza, ulitatupa nafasi kuanza miradi ya Olasiti Kati, Ngaramtoni, na Engosheratoni. Ni matumaini ya mkoa tatizo la umeme mdogo litakuwa historia ndani ya miezi mitatu ijayo. Asante.
 
Jpm amedai kupunguza matumiz ya serikali kama walivyonad ukawa basi punguza halmashauri, mikoa na wilaya kama vipi unganisha kama hizo wizara, mi sioni mantiki ya halmashauri 165 wilaya mia na a mikoa 30

Tujiuliuze kazi ya mkuu wa mkoa ya mkuu wa wilaya na halmashaur tukipata jibu basi ona namna ya kupunguza vitu hivyo.
Punguza matumiz ya seeikali punguza watumishi wasii na tija kwa Taifa,

Zingatia sana
Labda kama huna mtu anayesishi jf kwa ajili yako ndio utapuuza au nitafikiria wewe sio yule bali tumatazamie mwingine
 
Maeneo tajwa hapo juu ni maipu sugu yaliyodumu
katika awamu zote, kama vipi ayatumbue tu tuanze na upya.
 
Wakuu
Nasikitikia wengi wetu hatukumjuwa vizuri kitabia huyu rais wetu.Nakumbuka maneno ya Jakaya pale morogoro kuwa anayekuja mtamuelewa mimi ni mpole.
Huyu jamaa Kama hatapunguza speed anayokwenda nayo kwa sasa ataivuruga hii nchi.Mh rais kama utasoma hii nakuomba chonde chonde kuwa polite angalau kidogo maana hata hao mawaziri uliowateua sidhani kama watakuwa na sauti kwenye baraza lako.Maamuzi yote utakuwa unaamua mwenyewe watabaki " ndio mzee"

Ni hayo tu.
 
Mimi sijamwelewa kwanini kachagua watu ambao wanakashifa......teza za KIFISADI?....mengine atajua yeye.
 
Mh. Rais, hongera kwa kazi.. umeanza vema... nataka nikukumbushe ahadi yako ya SAFARI ZA NJE YA NCHI...!!

Tumefurahi umepiga marufuku mfanyakazi wa Serikali kwenda nje, ila ni kama tu KITU ANAFUATA NJE HAPA TANZANIA HAKIPO... ila sio masomo ya ajabu ajabu, sijui course fupi, seminar, sijui nn ambazo zoooote zinapatikana hapa nchini ila WAFANYAKAZI HASA WAKUU WA MASHIRIKA YA UMMA, IDARA, MAMLAKA WANAENDA NJE ili kupata per diem tu...!!!

1: Tatizo sio mafunzo wala kupata faida fulani kwa Taifa, wafanyakazi HUTAKA PER DIEM... sasa hili la per diem ndio balaa... Wakuu labda wa Mashirika au ma DGs au Ma CEOs unakuta kwa siku mtu analamba hadi $ 4,000 per day... yaani gharama zake zoooote kwa siku za safari za nje... mara per diem, hospitality, transport, phone, medical, emergency, entertainment, hotel.. it goes to $ 4,000 huu ni WIZIIIII.... sasa ulizia kafuata nn, hakuna kitu... ni KUPATA HIYO FEDHA TU...!!! Wakati wafanyakazi wengine wa Serikali hulipwa $ 300 kwa siku na wanaenda mji huo huo, gharama za maisha ni zile zile...

2: PENDEKEZO: Mh. Rais, hakikisha unadhibiti kabisa SAFARI ZA NJE kama ulivyosema... na KAMA YUPO ANAENDA, Per diem isizidi $ 800 per day.. au weka FLAT RATE, $ 800 kwa kila mfanyakazi utakaye mruhusu kwenda nje kimasomo au ktk course fulani... ili iwe rahisi ku track hesabu... i mean watu wanatumia Loopholes hiyo ya vitu vingiiiii kisha wanajazaa madola kibaooo... so weka Flat rate $ 800 per day as TOTAL EXPENDITURES ya siku nzima...!!!

Kazi njema...👉🚶🚶🚶🚶
 
Serikali ndio inatakiwa iuze vitalu vya gesi kwa wawekezaji moja kwa moja sio kuviuza kwa watu wa kati (Madalali) AMBAO hawana uwezo wa kuviendeleza Hivyo kulikosesha taifa mapato wakati madalali hao wakisubiria wanunuzi waje ambao hawaeleweki watakuja lini.

Na kama kuna yeyote aliyenunua kitalu chochote kiwe cha madini au gesi ambaye hajakifanyia lolote serikali imnyang`anye haraka kama ambavyo serikali itawanyang`anya waliouziwa viwanda na mashamba bila kuendeleza.

Magufuli asisahau wamilliki wa vitalu vya madini na gesi wasioviendeleza nao wanyang`anywe wanachelewesha maendeleo ya nchi.

Wizara ya madini ipitie wamiliki wote wa vitalu vya madini aina zote na gesi na wale ambao hawajafanya kazi yoyote kuviendeleza serikali ichukue haraka bila huruma.
 
mkuu huku arusha. Umeme unakatwa saa kumi na moja alfajiri, unarudishwa saa 6 usiku. Ni shiida watu wamechoka na hii tanesco wanasingizia kukata miti. Sasa tunajiuliza iyo miti inaanzakukatwa usiku wa manane? Magufuli zinduka tanesco imejaa majambazi na waujumu uchumi.

Kwa kweli Tanesco inabidi wajipange upya maana haya maelezo yamekuwa yanatolewa kila siku tunaboresha hiki tunaingiza gridi ya lakini hakuna mabadiliko na miaka inaenda
 
Naomba kuuliza wana JF, hivi kwa mfano umeenda mji kama London kwa safari ya kikazi, na ukalala Hoteli ya kawaida kabisa au guest house kama zipo, Je gharama ya chakula, malazi na simu inagharimu kiasi gani kwa siku?
 
2: PENDEKEZO: Per diem isizidi $ 800 per day.. so weka Flat rate $ 800 per day as TOTAL EXPENDITURES ya siku nzima...!!!
sasa hapa umepunguza gharama au umeongeza gharama? hili pendekezo lako ni bure kabisa

piga hesabu rahisi tu kuwa dola 1 = 2,150 so dola 800 x 2150 = 1,720,000/= per day

Hii bado ni pesa nyingi sana hata kama mtu anaenda new york
 
Inategemea unaenda mji gani...miji mingi ya Europe, mfano London, Paris, Geneva maisha ni ghali sana...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom