Habari za leo ndugu wana JF, leo naomba tujadili juu ya hili suala la mishahara ya watumishi wa Serikali kutofautiana kwa kiwango kikubwa.
Mimi nashindwa kuelewa ni kwa nini, hasa Wizara ya Elimu kuna tofauti kubwa kati ya wafanyakazi walio walimu na wasio walimu kwenye mishahara na hata kwenye maslahi mengine kama vile kupandishwa vyeo kwa wakati semina n.k
Ndugu zangu imekuwa ni jambo la kawaida katika hii wizara kuona mwalimu akipandishwa cheo, kuwa na mshahara mkubwa ukilinganisha na mfanyakazi mwingine asiye mwalimu hata kama wana level moja ya elimu, kupata semina wezeshi na kupewa kipaumbele kwenye mambo mengi kuliko mfanyakazi asiye kuwa mwalimu.
Mambo haya ndugu zangu yanawakatisha tamaa sana wafanyakazi wasio walimu hasa kwenye vyuo vya ualimu, unaweza ukakuta mwalimu anakuwa na mtiririko mzuri wa kupanda madaraja na vyeo kuliko asiye mwalimu na hata ukiangalia utofauti wa mishahara kati ya mwalimu na asiye mwalimu ni mkubwa sana, sasa huwa najiuliza ni kwanini hali hii iko hivi? ni kwanini huyu mwalimu athaminiwe kuliko mtumishi asiye mwalimu wakati wote ni waajiriwa wa Serikali moja, wizara moja na waziri mmoja, naibu waziri mmoja, katibu mkuu mmoja.
Ndugu zangu nayasema haya sio kwa kuwaonea wivu walimu hapana, nasema ili wahusika najua wanajua haya ila wameamua kukaa kimya kwa kuwa wao hawaumizwi na hali hii, haiwezekani mtu unakaa zaidi ya miaka nane pasipo kupandishwa daraja na unapofika wizarani maafisa utumishi wanatoa majibu yasiyoridhisha, halafu mwalimu aliyeajiriwa juzijuzi tu anapandishwa vyeo haraka anakuacha wewe ukiwa kwenye cheo na daraja hilohilo, hali hii haivumiliki inaumiza wafanyakazi tena inashusha morali ya ufanyaji wa kazi.
Naomba Rais, Waziri Mkuu, Katibu mkuu kiongozi, Waziri wa Elimu, Naibu waziri wa Elimu, Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu waliangalie hili kwa ukaribu ili wafanyakazi wote wawe na haki sawa na iyo haki itowele kwa wakati unaostahili haiwezekani kuwe na tofauti kubwa ya mshahara kati ya mwalimu na asiye mwalimu, tofauti kubwa ya kupandishwa vyeo kati ya mwalimu na asiye mwalimu, wote sisi ni watumishi wa umma tunapaswa kupewa stahiki zetu kwa usawa sio kama hali ilivyo sasa.
Ndugu Waziri nakuomba sana Rais wetu amekuamini kuwa utamsaidia kazi na ndio maana amekuteuwa kuwa waziri wa wizara hii ya elimu ivyo basi tunakuomba shughulikia swala hili mapema iwezekanavyo.
Asante nawasilisha.