Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Rais anasema tuwe wazalendo kwa kusifia vya kwetu,hii ni ngumu sana kwa sababu hivyo vitu anavyotaka tujivunie vingi ni vibovu na vya hovyo ingawa ni vya serikali. Hii haihitaji mganga ili kujua kua shule hospitali pamoja na mashirika mbalimbali ya binafsi ni bora mara dufu kuliko ya serikali. Kwani uzalendo ni kusifia k2 chako hata kama cha hovyo?
Sio kila kitu,
Mfano: Nimewahi kununua kiatu Made in Tanzania HIMO, Kizuri saana, vya nje ya nchi vyote vimeisha lakini kinadumu hadi kesho. Cha ajabu siku mtu mmoja alipokiona akafikiri ni GUCCI akataka nimwambie nimekitoa wapi nilimomwambia ni cha Hapa Bongo akakichukia na kusema Kitaharibika kesho tu hadi kesho kipo saafi kabisa. Hiyo ni COLONIAL MENTALITY.

Pili Vtu vyetu sio lazima viwe vya serikali, Hata wewe unaweza kuanzisha bado ni kitu chetu. Vya nje vipo vibaya na vizuri kama ilivyo vya serikali pia. Ndio maana unaambiwa sasa Muhimbili wanaanza kufanya vile vilivyokuwa vinafanywa INDIA.
 
"We live in a continent where even the health ministers don't have faith with our health departments.."
~Plo Lumbumba
 
Zuga sana huyuu baba nyie hamumjuwi vizuri tu,yaani sio kabisa tume bugi sana watanzani kwa kweli....
 
Wadau habari,
wote tumeshuhudia ubunifu na uchapakazi wa huyu Profesa Semboja tangu akiwa mwenyekiti wa bodi za mashirika kadhaa mfano Tanesco na TCRA. Aidha, katika kutekeleza majukumu yake ametoa mchango wake kama mtaalamu wa uchumi katika kuboresha tija katika taasisi alizopitia.
Nawasilisha.
 
[HASHTAG]#team[/HASHTAG] maprofesa,[HASHTAG]#team[/HASHTAG] lipumba,[HASHTAG]#team[/HASHTAG] waganga njaa,[HASHTAG]#team[/HASHTAG] kujipendekeza
haya majitu hayana faida kwenye jamii,wengi wao wanakaa mkao wa kuvizia ajira kama vijana wenye first degree
 
Mh. rais wa awamu ya tano wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John pombe Magufuli nina maoni ya fuatayo,
kwa kuwa nidhahiri kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa wasomi wengi wanaohitimu limekuwa likiongezeka siku hadi siku huku baadhi ya taasisi na watu mashuhuri tanzania wakitoa takwimu zinazoonyesha kuwa kila mwaka wahitimu zaid ya laki nane wanamaliza vyuo na ni elf 40 pekee ndio hupata ajira walizo somea na katika awamu hii mpaka sasa intake kama tatu hivi ziko mtaani. na kwa mfumo wa elimu ya Tanzania mtu anatumia miaka mingi sana kukaa darasani ukilinganisha na nchi jirani kama kenya na kadhalika na kww mtazamo wangu kutumia miaka mingi kusoma unakuwa unapungu mufa ambao ungetumia kuzalisha kwaida ya nchi. mtu baada ya kusoma miaka mingi na kukosa ajira ,inabidi ajiajiri mwenyewe sasa mpka mambo yake yakae sawa kiuchumi muda wa kuwa kijana mwenye nguvu unakuwa umeisha kias kwamba nguvu ambazo angezitumia mapema kujiajiri amepoteza muda mwingi kusoma na ajira amekosa. natamani mfumo wa elimu ungefupishwa kama kenya.form four anaenda chuo kikuu direct. ili hata akikosa ajira aliyo somea bado anakuwa na nguvu za kuzalisha kwa kipindi kirefu . sorry kama ntakuwa nimekosea jinsi ya kuwasilisha hoja
 
Amefanya nini mbona Tanesco bado mzigo... TCRA nako shida mpaka mkurugenzi akatumbuliwa.... arudi chuo kufundisha...
 
Wadau habari,
wote tumeshuhudia ubunifu na uchapakazi wa huyu Profesa Semboja tangu akiwa mwenyekiti wa bodi za mashirika kadhaa mfano Tanesco na TCRA. Aidha, katika kutekeleza majukumu yake ametoa mchango wake kama mtaalamu wa uchumi katika kuboresha tija katika taasisi alizopitia.
Nawasilisha.
Akiwa TCRA ndiye aliidhinisha kununua mtambo wa TTMS ambao hauwezi kucharge simu za ndani, akatumbuliwa na JPM hivi majuzi, akiwa TANESCO aliboronga Bodi ikavunjwa na Muhongo
 
na yeye ana tabia ya kujenga masji d maofisini kama yule wa ene eth eth efu?

tehtehthetehteheteh huyo hana hizo namjua sana yuko pale Mbezi beach Samaki maisha yake yote ya kusoma alikua Norway anagonga hot chair kama kawa hahahahahah
 
Naomba kunukuliwa kuwa haya ni maono yangu na naamin huu ndo ukweli.

Tangu mkuu huyu kuteuliwa amekua akipambana kwa kila namna kuhakikisha anatimiza malengo yake pia upinzani umekua macho ili kuonesha mapungufu yake.
Na yafuatayo ndo yaliyotekea
1.Mkuu huyu kujaribu kufanya mambo yote ambayo alikua akiona hayako sawa kwa wakat mmoja kitu ambacho kimefanya awe anakosolewa kila siku kwenye nyanja mbalimbali na hilo limefanya aingilie uhuru wa kidemocrasia wa vyama na mtu mmoja mmoja.
2. Upinzani umekua ukimshambulia kwenye mitandao ya kujamii sana ili kupewa haki yao kikatiba, hivyo bas kutumia nguvu nying kumshambulia mkuu huyo na kusahau kueneza sera zao.

Ushauri.
A. Kwa Mkuu huyu kama atasoma au kupewa taarifa.
1.Atumie nguvu zake kufanya majukumu yake kikatiba kwa kutengeneza plan ambazo zitafanya malengo yake mema kwa nchi ya fanikiwe.
2.Aache kulipa visasi asamehe naye atasamehewa kwa mabaya yake.
3.Asijibu mashambukizi yasiyo na msing kwa maneno bali matendo ya kimaendeleo.
4. Afate na kusikiliza ushaur wa wasaidiz wake na aache kuwa mwamuzi wa kila kitu.
5. Afate sera zake na aache kufanya kazi kwa matukio.

B. Kwa upinzani
1. Waache siasa za kumshambulia mtu mmoja mmoja na wahamie siasa za kisera.
2. Kupunguza kulalamika na watafute mbinu mbadala za kueneza sera zao kama kwenye mitandao ya jamii na sehemu nyingne.
3.Kuacha kupoteza nguvu kushindana na Polisi na waitumie nguvu hizo kueneza sera.
4. Kuacha kulisha matamanio yao binafsi bali waweke Taifa mbele hii itasaidia kuwa na nguvu ya kupambana na chama tawala 2020 maana bila hvyo sera ya divide and rule ya Chama tawala itaendelea kutawala.

Kokwa.
Marekebisho na mabiresho yanaruhusiwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom