Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
ajibu hili...kazuia mikutano ya kisiasa (hadhara) ...mbona Leprofeser kafanya???...
 
Ushauri wangu kwa raisi ni kwamba, aruhusu bunge lirushwe moja kwa moja, mikutano ya kisiasa ya wazi, busara na hekima vitumike katika maamuzi na siyo ubabe. Neno la Mungu linasema hivi, ''heri wale wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu''. Awe mpatanishi na siyo mchonganishi hasa kwa suala la Zanzibar.
Endelea kumuombea na omba pale ambapo unaona kunamakosa na Mungu ni Mwaminifu atatenda
 
Serikali yake iache kuwagawa watanzania kwa itikadi za kisiasa, hatukuwahi kutengwa kisiasa kama awamu hii, unamruhusu Lipumba anafanya mikutano ya hadhara kwa ulinzi wa jeshi la police wakati kuna zuio la police na halijatenguliwa, wakati huohuo unakataza vyama vingine kufanya mikutano ya hadhara, sisi tunaweza tusiwe na uwezo wa kuihukumu serikali yetu ila tunaamini Mungu anawaona.
 
Anirudishie uhuru wangu wa kuingia bar muda wowote, hasa asubui, kwani muda ninaofanyakazi yeye haujui.
Wenye bar waruhusiwe kufungua na kuuza vinywaji vyenye vileo muda wowote.
Tusipangiwe muda wa kunywa hasa pombe.
 
Wakuu huu uzi ni muhimu sana endapo hatutauwekea mizaha ya hapa na pale.
 
Serikali yake iache kuwagawa watanzania kwa itikadi za kisiasa, hatukuwahi kutengwa kisiasa kama awamu hii, unamruhusu Lipumba anafanya mikutano ya hadhara kwa ulinzi wa jeshi la police wakati kuna zuio la police na halijatenguliwa, wakati huohuo unakataza vyama vingine kufanya mikutano ya hadhara, sisi tunaweza tusiwe na uwezo wa kuihukumu serikali yetu ila tunaamini Mungu anawaona.
Atalifanyia kazi
 
Namshauri awatengue Ummy Mwalimu,Kigwangala,Tizeba,Lwenge,Mwijage,Mpango na Kairuki. Akishindwa kutengua uteuzi wao siyo mbaya hata yeye anaweza kujitengua/kujihudhuru mana ametuletea watu ambao wanafanya kazi kama hawataki/wamelazimishwa,sekta zao zinawaangusha wananchi walio wengi sababu hawaeleweki wanachokisimamia.
 
Dawa zipatikane kwenye hospital za serikali na wanafunzi elimu ya Juu wapewe mkopo wao kwa wakati.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom