Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mkoa wa Dar es salaam na wilaya yake ya Kinondoni hauna RC wala DC, ni bora amteue hata mzee Wassira awe RC na Lembeli au Anne kilango awe DC ili kurejesha heshima ya mkoa huo.
 
Hahhahahahhahah
Huyu Bibi..
Kuna kipindi hadi tulimuhisi ni yule Mh.Hawa wa Ghaasia kwajinsi alivyokua mropokaji.

Mkuu sina hakika. Ni nani ila nahakika ni mswahili mwenye elmu madrasa na ile formal education ya hapa na pale (kuunga Inga)
aha
Huyu Bibi..
Kuna kipindi hadi tulimuhisi ni yule Mh.Hawa wa Ghaasia kwajinsi alivyokua mropokaji.
Aaahah

Mku lakini
 
Kabla ya kilio cha kuadimika kwa madawa katika mahospitali yetu hakijaisha, sasa kimeibuka kilio kingine cha wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kukosa mikopo na hivyo kuendelea kuongeza lawama kwa serikali.

Mh.Raisi,lawama hizi kwa mtazamo wangu si za lazima kabisa bali ni za kujitakia tu kwa nyinyi kushindwa kuwa na vipaumbele na zaidi watu kutaka kuishi maisha ya anasa kwa gharama ya serikali,serikali ambayo teyari ina mzigo mkubwa wa kuhudumia wananchi wake.

Mh.Raisi,mimi nina ushauri mmoja tu kwako juu ya namna bora na ya haraka ya kumaliza tatizo hili bila hata kuathiri bajeti ya serikali wala kuhamisha mafungu na mambo mengine ya aina hiyo.

Mh.Raisi,unachotakiwa ni kufanya maamuzi magumu ya kufuta sitting allowance za wabunge na kuondoa magari ya anasa maarufu kama mashangingi serikalini.

Unachotakiwa ni kupeleka muswaada /mapendekezo Bungeni katika Bunge lijalo la November au January mwakani ya kuwataka wabunge waachane na malipo haya ya sitting allowance ili fedha zitakazookolewa zikahudumie watoto wa masikini pamoja na kuboresha huduma za jamii.

Malipo haya jamani ni ya aibu kwa wanasiasa waliotuomba kura kwa lengo la kutetea masikini na wanyonge wa nchi hii.Hivi nyinyi watu hata nafsi zenu haziwasuti kuendelea kulipwa fedha hizi?Mbona mwalimu au Police traffick hana kitu kinachoitwa standing standing allowance?Nyie huu uhalali wa kujilipa fedha hizi mnaupata wapi?!

Mh.Raisi,nina hakika hakuna atakaepinga hadharani pendekezo hili kwani hata wao nafsi zao zinawasuta kupokea fedha hizi ila tu imekosekana nguvu ya kupendekeza jambo hili lifike mwisho.

Mh.Raisi,eneo lingine ni hili la matumizo ya magari ya anasa maarufu kama mashangingi kwa mawaziri na viongozi wengine waandamizi serikalini.

Magari haya mbali na kuwa yananunuliwa kwa gharama kubwa,lakini hata gharama ya kuyahudumia ni kubwa mno kuanzia mafuta,vipuri,service,n.k.

Hivi kuna ulazima gani wa waziri,naibu waziri,makatibu wakuu,wakurugenzi wa taasisi na mashirika ya umma, wakuu wa mikoa,wilaya,vigogo wa polisi,magereza, na jeshi wote kutumia magari haya?

Hivi Land Cruiser Mkonge New Model haziwatoshi?Anasa za aina hii katika ya umasikini huu kwa faida ya nani?Nani atakaethubutu kupinga hili?Atakaekupinga kwanini usimfukuze?

Mh.Raisi,kaa na watendaji wako kisha mfanye tathimini juu ya kutekeleza uamuzi huu na zaidi muweke timeframe ya kutekeleza mpango huu.

Mh.Raisi,maamuzi ya aina hii ndio tunayoyata.Huu ndio udikteta tunaouhitaji na sio ule wa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na mambo mengineyo yanayafanana na hayo.

Fedha zitakazopatikana zilelekeza kwenye huduma za jamii kama vile kununulia madawa na vifaa tiba,ujenzi wa madarasa,kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu,n.k.

Mh.Raisi,hebu jiulize bei ya shangingi moja ingesomesha watoto wangapi wa masikini vyuo vikuu?

Mh.Raisi,kama mliona kuhudumia nyumba za serikali ilikuwa ni gharama mpaka mkaamuza kuziuza, kinawashinda nini kwenye mashangingi haya?

Hivi katika mataifa tajiri na yaliyoendelea,viongozi waandamizi serikalini wanatumia magari haya haya ya gharama?

Naamini hata UkAWA waliposema elimu bure mpaka chuo kikuu,vichwani mwao walikuwa na policy za aina hii sera ambazo nyinyi zimewashinda kwa kukosa dhamira na uthubutu tu.
 
SEMA HIVI;
Afute wabunge wote wa kuteuliwa ,wabunge wote wa viti maalum,madiwani wa viti maalumu pia wakuu wa wilaya waondolewe ikiwezekana hata bodi mbalimbali mfano parole.
akifanya hayo pesa itapatikana
 
NAUNGA MKONO HOJA SITTING ALLOWANCE IS NON-SENSE.../
•WANA MIFUKO YA MAJIMBO KUSAIDIA MAJIMBONI.
•WANA MISHAHARA INAYOFIKIA MIL 10+
-->>UBUNGE NDIO KAZI YAO INAYOWAPA MISHAHARA.,KAMA MWL,AU MTUMISHI YEYOTE YULE WA UMMA.
**HIVI KUNA TEACHING ALLOWANCES?,FOR TEACHERS?
 
Kabla ya kilio cha kuadimika kwa madawa katika mahospitali yetu hakijaisha, sasa kimeibuka kilio kingine cha wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kukosa mikopo na hivyo kuendelea kuongeza lawama kwa serikali.

Mh.Raisi,lawama hizi kwa mtazamo wangu si za lazima kabisa bali ni za kujitakia tu kwa nyinyi kushindwa kuwa na vipaumbele na zaidi watu kutaka kuishi maisha ya anasa kwa gharama ya serikali,serikali ambayo teyari ina mzigo mkubwa wa kuhudumia wananchi wake.

Mh.Raisi,mimi nina ushauri mmoja tu kwako juu ya namna bora na ya haraka ya kumaliza tatizo hili bila hata kuathiri bajeti ya serikali wala kuhamisha mafungu na mambo mengine ya aina hiyo.

Mh.Raisi,unachotakiwa ni kufanya maamuzi magumu ya kufuta sitting allowance za wabunge na kuondoa magari ya anasa maarufu kama mashangingi serikalini.

Unachotakiwa ni kupeleka muswaada /mapendekezo Bungeni katika Bunge lijalo la November au January mwakani ya kuwataka wabunge waachane na malipo haya ya sitting allowance ili fedha zitakazookolewa zikahudumie watoto wa masikini pamoja na kuboresha huduma za jamii.

Malipo haya jamani ni ya aibu kwa wanasiasa waliotuomba kura kwa lengo la kutetea masikini na wanyonge wa nchi hii.Hivi nyinyi watu hata nafsi zenu haziwasuti kuendelea kulipwa fedha hizi?Mbona mwalimu au Police traffick hana kitu kinachoitwa standing standing allowance?Nyie huu uhalali wa kujilipa fedha hizi mnaupata wapi?!

Mh.Raisi,nina hakika hakuna atakaepinga hadharani pendekezo hili kwani hata wao nafsi zao zinawasuta kupokea fedha hizi ila tu imekosekana nguvu ya kupendekeza jambo hili lifike mwisho.

Mh.Raisi,eneo lingine ni hili la matumizo ya magari ya anasa maarufu kama mashangingi kwa mawaziri na viongozi wengine waandamizi serikalini.

Magari haya mbali na kuwa yananunuliwa kwa gharama kubwa,lakini hata gharama ya kuyahudumia ni kubwa mno kuanzia mafuta,vipuri,service,n.k.

Hivi kuna ulazima gani wa waziri,naibu waziri,makatibu wakuu,wakurugenzi wa taasisi na mashirika ya umma, wakuu wa mikoa,wilaya,vigogo wa polisi,magereza, na jeshi wote kutumia magari haya?

Hivi Land Cruiser Mkonge New Model haziwatoshi?Anasa za aina hii katika ya umasikini huu kwa faida ya nani?Nani atakaethubutu kupinga hili?Atakaekupinga kwanini usimfukuze?

Mh.Raisi,kaa na watendaji wako kisha mfanye tathimini juu ya kutekeleza uamuzi huu na zaidi muweke timeframe ya kutekeleza mpango huu.

Mh.Raisi,maamuzi ya aina hii ndio tunayoyata.Huu ndio udikteta tunaouhitaji na sio ule wa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na mambo mengineyo yanayafanana na hayo.

Fedha zitakazopatikana zilelekeza kwenye huduma za jamii kama vile kununulia madawati na vifaa tiba, ujenzi wa madarasa na kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu.

Mh.Raisi,hebu jiulize bei ya shangingi moja ingesomesha watoto wangapi wa masikini vyuo vikuu?

Mh.Raisi,kama mliona kuhudumia nyumba za serikali ilikuwa ni gharama mpaka mkaamuza kuziuza, kinawashinda nini kwenye mashangingi haya?

Hivi katika mataifa tajiri na yaliyoendelea,viongozi waandamizi serikal wanatumia magari haya haya ya gharama?

Naamini hata UkAWA waliposema elimu bure mpaka chuo kikuu,vichwani mwao walikuwa na policy za aina hii sera ambazo nyinyi zimewashinda kwa kukosa dhamira na uthubutu tu.
Basi wimbo wa wanyonge ukome mara moja.
 
SEMA HIVI;
Afute wabunge wote wa kuteuliwa ,wabunge wote wa viti maalum,madiwani wa viti maalumu pia wakuu wa wilaya waondolewe ikiwezekana hata bodi mbalimbali mfano parole.
akifanya hayo pesa itapatikana
Umasikini na matatizo ya nchii kwa kiasi kikubwa ni ya kujitakia na msingi wake ni ubinafsi wa watu tuliowapa dhamana wao kutaka kuishi kama wako peponi.

Mavyeo mengine wala hayana umuhimu wowote zaidi ya kuongeza tu gharama kwa serikali.
 
SEMA HIVI;
Afute wabunge wote wa kuteuliwa ,wabunge wote wa viti maalum,madiwani wa viti maalumu pia wakuu wa wilaya waondolewe ikiwezekana hata bodi mbalimbali mfano parole.
akifanya hayo pesa itapatikana
Hapo unamshauri arejeshe mchakato wa Katiba Mpya kuanzia rasimu ya mzee Warioba, jambo ambalo kwa mfurukutwa wa CCM kama alivyo mtukufu huo ni mwiba mkali! Hana ujasiri huo.
 
-->>NA HAPA NDIPO MAHALA PEKEE WABUNGE WOTE BILA KUJALI UTOFAUTI WA VYA HUKAA PAMOJA NA KUTETEA MASLAHI YAO KWA NGUVU MOJA.
(FEDHA BUANA)

Hivi kweli unampa sitting allowance mtu mwenye umri wa miaka 40,50,60 tena aliesoma bure,aliekwisha jijenga na mwenye mamiradi chungu nzima alafu unamuacha mtoto wa muuza nyanya, maandazi,samaki,n..k analilia mkopo?!

Politicians sio watu kabisa!
 
Hizi posho za wabunge ni aina ya ufisadi wa kitaasisi. Huu ni wizi wa kuaminiwa. Wabunge kwa ujumla wao wanakosa kitu kinachoitwa "social conscience"; yaani kukosa hisia juu matatizo na dhiki za wananchi. Lakini kwa upande mwingine, ulipaji wa hizi posho ni mkakati wa watawala wa kuwaondoa wabunge kwenye tabaka la wananchi wa kawaida na kuwaweka kwenye tabaka la juu la watawala ili kupunguza nguvu na hisia ya uwakilishi wao kwa wananchi. Huku kuhama tabaka moja la kijamii kwenda lingine kunaitwa "social mobility". Mtu akiwa tabaka la juu hawezi kamwe kuwakilisha maslahi ya tabaka la chini. Kinachotokea ni wananchi kukosa uwakilishi wa kweli bungeni, kwa upande mmoja, na wabunge kuungana na watawala katika kupora na kujinufaisha binafsi na rasilimali za nchi, kwa upande mwingine.
 
Salary Slip hapa hata wafunge kula mwaka mzima kusevu fedha, watumishi walipwe nusu mishahara nk nk hakuna mabadiliko yeyote yatakayo tokea. Kwa nini? Kwa sababu wameshashindwa kuongoza nchi. Mangapi wamesimamisha mpaka sasa na hakuna tofauti zaidi ya shida kuongezeka? Kodi wanasema hazikwepwi hivyo makusanyo makubwa tofauti iko wapi?
Kuendesha serikali ni utaalamu kama haupo hata tusaidiwe na dunia nzima hatuta songa mbele zaidi ya kurudi nyuma.
Ni kama mtu mmoja aliambiwa acha pombe ndio utaweza kupata maendeleo, akamuuliza huyo anayemuambia hivyo kuwa mbona wewe na wenzako ambao tunafanya kazi ya aina moja na kipato kinalingana hamnywi pombe lakini mie nimejenga na nyie mmepanga?
Kwa hiyo ilipaswa JPM kwa manufaa ya nchi amuulize yule mgombea aliyesema atatoa elimu bure hadi Chuo kikuu angetumia maarifa gani kama yeye hata kukopesha tuu anashindwa? Nchi hii ni yetu hivyo anaruhusiwa kutumia mawazo yeyote ya kujenga taifa kutoka kokote bila aibu. Unless hakuwa na nia njema na taifa wakati anatafuta kazi hiyo aliyonayo
 
Kwa jinsi wanavyopenda raha sidhani km watalifanyia kazi
Labda uwambie wapunguze mishahara ya walimu hapo watakuelewa.
Km Fao la kujitoa wamelitoa lkn wao baada ya miaka 5 tu wanapata mafao yao
Sidhani lbda
 
Hivi mkuu unadhani kuwa Magufuli kakosa hizo fedha za kupeleka huko? Hicho siyo kipaumbele chake na kwanza anaona kupeleka huko ni kupoteza fedha zake bure.

Wewe hujiulizi kuwa alichangisha fedha za majanga na hajazipeleka japo zilotolewa na watu itakuwa hizo nyingine??

Kikwete mbona alinunua mashangingi na aliweza kupeleka walau tufedha tudogo huko? Naona bado hujamfahamu JPM wewe!

Yeye anajitahidi kufanikisha wizara yake ya ujenzi ndo maana hata fedha za matukio anazuia na kupeleka ujenzi.
 
Kwa haraka haraka ni wazo zuri. Hata hivyo, ukienda kwa undani wake hutachelewa kubaini kuwa wazo hili si endelevu. Mikopo itawrza kupatikana kwa semester au mwaka mmoja lakini itakuwaje mwakani na miaka mifano ijayo? Tutarudi kwenye tatizo la msingi ambao wakosoaji wanaita kuendesha mambo kwa mizuka, kwa matukio, kwa kukurupuka, kwa mtindo wa zimamoto n.k.

Mkuu, tunachohitaji ni mipango endelevu na utekelezaji makini zaidi baaasi. Other things will fix themselves.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom