Justice minister
JF-Expert Member
- Sep 1, 2016
- 1,173
- 823
Mkoa wa Dar es salaam na wilaya yake ya Kinondoni hauna RC wala DC, ni bora amteue hata mzee Wassira awe RC na Lembeli au Anne kilango awe DC ili kurejesha heshima ya mkoa huo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu Bibi..
Kuna kipindi hadi tulimuhisi ni yule Mh.Hawa wa Ghaasia kwajinsi alivyokua mropokaji.
AaahahHuyu Bibi..
Kuna kipindi hadi tulimuhisi ni yule Mh.Hawa wa Ghaasia kwajinsi alivyokua mropokaji.
Basi wimbo wa wanyonge ukome mara moja.Kabla ya kilio cha kuadimika kwa madawa katika mahospitali yetu hakijaisha, sasa kimeibuka kilio kingine cha wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kukosa mikopo na hivyo kuendelea kuongeza lawama kwa serikali.
Mh.Raisi,lawama hizi kwa mtazamo wangu si za lazima kabisa bali ni za kujitakia tu kwa nyinyi kushindwa kuwa na vipaumbele na zaidi watu kutaka kuishi maisha ya anasa kwa gharama ya serikali,serikali ambayo teyari ina mzigo mkubwa wa kuhudumia wananchi wake.
Mh.Raisi,mimi nina ushauri mmoja tu kwako juu ya namna bora na ya haraka ya kumaliza tatizo hili bila hata kuathiri bajeti ya serikali wala kuhamisha mafungu na mambo mengine ya aina hiyo.
Mh.Raisi,unachotakiwa ni kufanya maamuzi magumu ya kufuta sitting allowance za wabunge na kuondoa magari ya anasa maarufu kama mashangingi serikalini.
Unachotakiwa ni kupeleka muswaada /mapendekezo Bungeni katika Bunge lijalo la November au January mwakani ya kuwataka wabunge waachane na malipo haya ya sitting allowance ili fedha zitakazookolewa zikahudumie watoto wa masikini pamoja na kuboresha huduma za jamii.
Malipo haya jamani ni ya aibu kwa wanasiasa waliotuomba kura kwa lengo la kutetea masikini na wanyonge wa nchi hii.Hivi nyinyi watu hata nafsi zenu haziwasuti kuendelea kulipwa fedha hizi?Mbona mwalimu au Police traffick hana kitu kinachoitwa standing standing allowance?Nyie huu uhalali wa kujilipa fedha hizi mnaupata wapi?!
Mh.Raisi,nina hakika hakuna atakaepinga hadharani pendekezo hili kwani hata wao nafsi zao zinawasuta kupokea fedha hizi ila tu imekosekana nguvu ya kupendekeza jambo hili lifike mwisho.
Mh.Raisi,eneo lingine ni hili la matumizo ya magari ya anasa maarufu kama mashangingi kwa mawaziri na viongozi wengine waandamizi serikalini.
Magari haya mbali na kuwa yananunuliwa kwa gharama kubwa,lakini hata gharama ya kuyahudumia ni kubwa mno kuanzia mafuta,vipuri,service,n.k.
Hivi kuna ulazima gani wa waziri,naibu waziri,makatibu wakuu,wakurugenzi wa taasisi na mashirika ya umma, wakuu wa mikoa,wilaya,vigogo wa polisi,magereza, na jeshi wote kutumia magari haya?
Hivi Land Cruiser Mkonge New Model haziwatoshi?Anasa za aina hii katika ya umasikini huu kwa faida ya nani?Nani atakaethubutu kupinga hili?Atakaekupinga kwanini usimfukuze?
Mh.Raisi,kaa na watendaji wako kisha mfanye tathimini juu ya kutekeleza uamuzi huu na zaidi muweke timeframe ya kutekeleza mpango huu.
Mh.Raisi,maamuzi ya aina hii ndio tunayoyata.Huu ndio udikteta tunaouhitaji na sio ule wa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na mambo mengineyo yanayafanana na hayo.
Fedha zitakazopatikana zilelekeza kwenye huduma za jamii kama vile kununulia madawati na vifaa tiba, ujenzi wa madarasa na kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu.
Mh.Raisi,hebu jiulize bei ya shangingi moja ingesomesha watoto wangapi wa masikini vyuo vikuu?
Mh.Raisi,kama mliona kuhudumia nyumba za serikali ilikuwa ni gharama mpaka mkaamuza kuziuza, kinawashinda nini kwenye mashangingi haya?
Hivi katika mataifa tajiri na yaliyoendelea,viongozi waandamizi serikal wanatumia magari haya haya ya gharama?
Naamini hata UkAWA waliposema elimu bure mpaka chuo kikuu,vichwani mwao walikuwa na policy za aina hii sera ambazo nyinyi zimewashinda kwa kukosa dhamira na uthubutu tu.
Umasikini na matatizo ya nchii kwa kiasi kikubwa ni ya kujitakia na msingi wake ni ubinafsi wa watu tuliowapa dhamana wao kutaka kuishi kama wako peponi.SEMA HIVI;
Afute wabunge wote wa kuteuliwa ,wabunge wote wa viti maalum,madiwani wa viti maalumu pia wakuu wa wilaya waondolewe ikiwezekana hata bodi mbalimbali mfano parole.
akifanya hayo pesa itapatikana
Hapo unamshauri arejeshe mchakato wa Katiba Mpya kuanzia rasimu ya mzee Warioba, jambo ambalo kwa mfurukutwa wa CCM kama alivyo mtukufu huo ni mwiba mkali! Hana ujasiri huo.SEMA HIVI;
Afute wabunge wote wa kuteuliwa ,wabunge wote wa viti maalum,madiwani wa viti maalumu pia wakuu wa wilaya waondolewe ikiwezekana hata bodi mbalimbali mfano parole.
akifanya hayo pesa itapatikana
-->>NA HAPA NDIPO MAHALA PEKEE WABUNGE WOTE BILA KUJALI UTOFAUTI WA VYA HUKAA PAMOJA NA KUTETEA MASLAHI YAO KWA NGUVU MOJA.
(FEDHA BUANA)