Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Tungetumia fursa hiyo kuuza mazao kwenye nnchi zenye migogoro ya kisiasa kama Sudani, Somalia nk. Tungewapelekea michicha ya kutosha ili wapate nguvu ya kupigana haswaa
 
Tungetumia fursa hiyo kuuza mazao kwenye nnchi zenye migogoro ya kisiasa kama Sudani, Somalia nk. Tungewapelekea michicha ya kutosha ili wapate nguvu ya kupigana haswaa
Serikali hii ya sasa kipaumbele chake sio kilimo maana sio juhudi zozote za kuinua kilimo. Huwezi kuzungumzia viwanda wakati kilimo kiko hoi?! Kilimo kwanza hutoa chakula cha kulisha nguvukazi ya viwandani na kwingineko lakini pia hutoa malighafi kwa ajili ya viwanda.kilimo pia huongeza pato la taifa kwa kuuza ziada ya chakula nje na kupata fedha za kigeni! Kilimo pia ni chanzo kikubwa cha ajira. Nchi Ina maji mengi ardhi kubwa yenye rutuba na nguvukazi ya kutosha. Serikali ijenge miundo mbinu ya umwagiliaji na Ku mechanize kilimo ili kiwe cha tija na cha kisasa! Tuachane na kilimo cha kutegemea mnvua na jembe la mkono.
Tumezungukwa na nchi nyingi zenye mahitaji makubwa ya chakula kutokana na political instability au hali mbaya ya hewa tutumie fursa hii ya soko la chakula
Nchi ijitosheleze kwa chakula kwanza Ndio ufikirie bombardier SGR viwanda nk
 
Kila chama kilikuwa na ilani yake, sasa kusema ampe ubunge then cheo anachostahili Serikalini una maana gani? Je akiwa serikalini atakuwa anatekeleza ilani ipi kati ya ile ya ACT ya kwake na hii yenu ya CCM?
kwani hivi wabunge wa cdm na cuf wanatekeleza ilani gani......wajuvi mnijuze kidogo
 
Mh Rais mimi ni raia wa taifa hili nilizaliwa hapa na nitakufa katika ardhi yangu pendwa Tanzania.

Kiukweli nasema either wanijua au haunijui, mimi nina kilio cha siku nyingi sana kumuhusu huyu Makonda na nilishawahi kuandika thread kukuambia uwe makini na kijana Makonda maana matendo yake yameficha anguko kubwa la serikali yako.

Unaweza kuniuliza kwanini nasema haya ila nakuomba ujue kama wewe ndio kiongozi wetu basi yakupasa kutupenda sote na usikubali ngoma ya mtu mmoja.

Mh Rais ninazo sababu mia moja kumpinga Makonda na kukutahadharisha naye ama ukubali ama usikubali.

Wewe ni Rais wa Jamuhuri ya Tanzania na Makonda ni Mkuu wa Mkoa. Taarifa ya mkoa inapita kwenye vyombo kadhaa ili kukufikia, lakini hapo hapo Makonda sio mtu wa karibu na wewe katika swala la reporting line.

Kusimamia maneno au maelezo ya kijana mmoja bila kufuata taratibu za kiti chako ni kuleta madhara makubwa kwa chama na taifa. Kwa sababu Makonda sio Waziri ni Mkuu wa Mkoa, je inakuwaje yeye anasimama sehemu ya waziri? Je majina aliyoyatoa yalipita kwa nani mpaka akataja watu?

Mh Rais hapa unacheza hata na usalama wako na sikushauri uendelee na hii hali. Mh Rais hili ni taifa huru na watu wake wapo huru, tunataka kujua majina alipata wapi na kwanini idara za usalama zilizokuzunguka zisiseme kama sheria inavyosema?

Mh Rais hili sio taifa la kila mtu akiwa na taarifa hata bila kuthibitishwa anaita vyombo vya habari na kuanza kutaja watu. Hili ni taifa lililo na sheria na katiba na wote tunaongozwa na sheria. Sio mambo ya kuzushiana.

Mh Makonda amevunja sheria na kama hulioni kwakweli wengi wetu tutaanza kuona wewe sio Rais wa wote ila una makundi tena makundi yasiyotenda haki. Makonda ni lazima afuate sheria na pia ni lazima umuondoe kwenye kiti kuondoa machozi ya wengi au usubiri kuuona ukweli wakati muda ukiwa umepita.

Nimeandika haya kwa uchungu sana maana naona sasa tunatoka kwenye mstari.

TISS mshaurini Rais, Maafisa wa ngazi za juu mshaurini Rais.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom