Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kenya inaongoza kwa ufisadi...ila maendeleo yako juu yetu... Tatizo la serikali yetu ni wanasiasa kuingilia mambo ya kitaalamu... Na juzi nilimsikia kenyatta akijipongeza kwa hili...
Taaluma na njaa!!!ngumu kuelewa,ni mwanasheria gani atahudhuria mahakamani bila kushiba,ni mwalimu gani atafundisha huku anapiga miayo?ni muuguzi gani atafanya kazi na njaa?ataomba rushwa tu au atabana nguvu zake ili aweze kutembea wakati wa kurudi nyumbani.
Mishahara ya wakenya ndiyo hii ya kibongo?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Hilo haliwezekani, hata wakiacha kujilipa hata shilingi na kufanya kazi ya kujitolea hizo fedha bado hazitatosha kulipa kila Mtanzania vizuri, maadamu hkn uzalishaji hakuwezi kuwa na fedha ya maisha mazuri!
Kama haliwezekani tusubiri Yesu arudi,tusiote maendeleo basi,siyo tunapigiana makelele tu.Yaani mimi nimlinde faru Fausta anayetumia mamilioni halafu nilipwe laki mbili !!wakati hata chakula chake tu nakitamani!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kama haliwezekani tusubiri Yesu arudi,tusiote maendeleo basi,siyo tunapigiana makelele tu.Yaani mimi nimlinde faru Fausta anayetumia mamilioni halafu nilipwe laki mbili !!wakati hata chakula chake tu nakitamani!

Post sent using JamiiForums mobile app


Wewe unaweza kuacha huwo ni uamuzi wako lkn tupo Watz wengi tulio tayari kujitolea kwa ajili ya nchi yetu!
 
Wewe unaweza kuacha huwo ni uamuzi wako lkn tupo Watz wengi tulio tayari kujitolea kwa ajili ya nchi yetu!
Na baada ya kujitolea kwenu mbona hatuendelei?
Mie nimetoa ushauri tu kwa serikali kama wewe ndo serikali sawa,subiri tutaendelea kesho.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Na baada ya kujitolea kwenu mbona hatuendelei?
Mie nimetoa ushauri tu kwa serikali kama wewe ndo serikali sawa,subiri tutaendelea kesho.

Post sent using JamiiForums mobile app


Sasa kama wewe umeshajitoa, kwa nini ni shida yako tena kama tunaendelea au hatuendelei?
 
Jaribu kutoa mawazo kingi kipatikane tugawane na sio kulazimisha tugawane sawa hiki kidogo....

TANZANIA WANAOZALISHA NI ASILIMIA NDOGO SAANA, WALAJI NI WENGI na MATOKEO YAKE NI HASARA, NI WAKATI WA SERIKALI KUONGEZA IDADI YA WAZALISHAJI WAFIKIE ZAIDI YA MIL 20 TOFAUTI NA NASASA AMBAPO WAZALISHAJI NI CHINI YA MIL10. NI JUKUMU LA SERIKALI KUBUNI MBINU ZA KUONGEZA UZALISHAJI KWENYE KILIMO,VIWANDA NA TAASISI NYINGINEZO ILI WATANZANIA WENGI WATUMIKE KUZALISHA..
 
Tuache hizi longolongo za uzalendo sasa,zimepitwa na wakati.Mara wapiga dili sijui mafisadi na wala rushwa mambo ya kizamani hayo. Mhenga mkuu aliyezifanya mbingu na nchi alishasema ni halali kwa mlawi kula vya madhabahuni.
Unategemea nini kuniweka juu ya hazina yako wakati nina kiu na njaa balaa!naanzaje mimi kutunza hiyo hazina bila kuitiatia mkono?
Njaa siyo mchezo,Mfalme Daudi alikula mikate ya wonyesho akijua si halali kwake, Hivi vijichenji mnavyo walipa watumishi wenu havikidhi njaa zao mjue.Lipeni mishahara ya maana muone watu wanavyopiga kazi.Kazi na njaa ni kama mbingu na ardhi bana.
Hebu jaribuni hilo mjionee maajabu.

Post sent using JamiiForums mobile app
maendeleo yatakuja Tz pale tu nduli CCM itakapo kufa
 
Hakuna kitu kigumu kama uko kazini alafu nyumbani umeacha mambo hayajakaa sawa, kuanzia cha asubuhi mpaka jioni hakieleweki. Huwezi kufanya kazi kwa ufanisi, lazima utatafuta means nyengine ya kujiongeza kabla mwisho wa mwezi.
 
Hii nchi itaendelea baada ya watu kuifanya siasa ndio uti wa mgongo wa nchi hii.
 
Naona umeshawasoma wakina Philip Mpango na Magufuli, maana wao huchukua mawazo ya wana JF na kuyafanyia kazi, hivyo unadhani hili wazo watalifanyia kazi, thubutu!! Magu hasomeki hata mshahara mwaka huu nyongeza endeleeni kuota, kwanza ni uhakiki wa DRS la saba, then unakuja uhakiki wa vyeti vya taaluma, tunaanza na Certificate ikiisha, inakuja vyeti vya Diploma, then Bachelor na Masters then ndo nyongeza sasa hiyo ni 2019, tujiandae kwa uchaguzi wa kumrudisha Magu tena, hahaha

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Naona umeshawasoma wakina Philip Mpango na Magufuli, maana wao huchukua mawazo ya wana JF na kuyafanyia kazi, hivyo unadhani hili wazo watalifanyia kazi, thubutu!! Magu hasomeki hata mshahara mwaka huu nyongeza endeleeni kuota, kwanza ni uhakiki wa DRS la saba, then unakuja uhakiki wa vyeti vya taaluma, tunaanza na Certificate ikiisha, inakuja vyeti vya Diploma, then Bachelor na Masters then ndo nyongeza sasa hiyo ni 2019, tujiandae kwa uchaguzi wa kumrudisha Magu tena, hahaha

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
Lakini mkuu,wanapohakiki si ndo kazi yenyewe?na si wameshiba?tuhakikiane tukiwa tumeshiba wote basi.Fikiria ile energy mwalimu anayotumia kukuimbisha a,b,c,d,halafu hata maji hana si uzwazwa huo! watoto watafaulu kweli?Wabadilike tu hata kama wanapunguza ajira ni sawa lakini hao wanaobakia washibe.ili watumike kweli.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kwa heshima na taadhima naomba nitoe ushauri wa kiroho kwa Mhe. Rais John Joseph Pombe Magufuli(JJPM). Nimepata msukumo huu wakti nilipokuwa nikimwombea Rais wetu kama ambavyo amekuwa akiomba siku zote Watz tumwombee.

Mimi kama mtumishi wa Mungu nimepata msukumo huu ambao naamini umetoka kwa Yehovah Mungu Baba aliye yote na juu ya mambo yote. Sina hakika kama Mhe Rais atakuwa tayari kuupokea ushauri huu wa kiroho! Hata hivo ana hiari ya kuukubali au kuutupilia mbali na hapo itakuwa ni yeye na Mungu!!

Tangu Mhe. JJPM aingie madarakani kuna mengi mazuri na mabaya ambayo amewafanyia Watanzania. JJPM anajua yeye si malaika hivo kama binadamu ana mapungufu yake. Ushauri wangu wa kiroho unajikita kwenye mabaya ambayo amewafanyia Watanzania kwa kipindi hiki cha takribani mwaka na miezi 8. Nianze na kumkumbusha Rais JJPM jambo la msingi sana kutoka kwenye Biblia kuhusu andiko juu ya Kaini na Habili(Abel) waliokuwa watoto wa Adamu na Eva. Kwamba Kaini alimwua ndugu yake Habili kwasababu ya chuki tu!! Mungu alipomtafuta Kaini kumwuliza yuko wapi ndugu yake Habili, Kaini kwa jeuri na Kibri akamjibu Muumba wake kuwa hajui kwa vile yeye siyo mchungaji wa ndugu yake Habili! Lakini Mungu akiwa anajua kilichotokea alimwambia Kaini, MBONA DAMU YA NDUGU YAKO INANILILIA TOKA ARDHINI? Kilichotokea hapo ilikuwa ni adhabu au hukumu ya Kaini kulaaniwa na kufurushwa toka bustani ya Edeni na akatiwa alama usoni ili mtu akimwona asimwue(Mwanzo 4: 8-14).

Nakumbuka baada ya Uhuru tulikuwa na slogan au msemo unaosema, ''Watanganyika wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja''.Kitendo cha Rais JJPM kuanza mbinu za kudhibiti na kuwabagua wapinzani kwa kuwatesa,kuwanyanyasa na hata wengine kuwapoteza katika mazingira ya kutatanisha ni jambo ambalo linaumiza hisia za Watanzania wengi wapenda amani, utulivu na mshikamano. Nitoe mfano mubashara kuhusu kupotea kwa ndugu Ben Saanane ambaye mpaka leo haijulikani yuko hai au ni marhemu! imekuwa ni kitendawili ambacho hakuna aliyeweza kukitegua kuhusu wapi aliko Ben Saanane!!

Kwa Serikali inayojinasibu kuwa ina utawala bora na sikivu kwa Wananchi wake hili ni doa ambalo haliwezi kufutika kirahisi! Nchi kama Israel huwa haingalii ni raia wangapi wako hatarini au kutushiwa maisha huwa inachukua hatua za mara moja kuokoa maisha ya raia wake hata akiwa ni mmoja tu!! Tangu Ben apotee, si Rais wala Serikali yake wameweka bayana ya wapi aliko huyu ndugu yetu! Jambo moja nina hakika kuhusu Ben Saanane, kwamba kuna watu wamehusika na kupotea kwa ndugu yetu Ben Saanane na wanajua kila kitu kilichotokea siku ile alipopotea. Mungu anajua na pengine angelishuka leo kama kule Edeni na kuwauliza hawa watu waliohusika wangelisema kama Kaini, kwamba wao siyo wachungaji wa Ben Saanane. Mungu anawaambia MBONA DAMU YA NDUGU YENU INAWALILIA? Kinachofuata hapo ni hukumu kama ilivokuwa kwa Kaini!!

Namshauri Rais JJPM abadilike katika namna ya kuendesha nchi hii. Rais asijione kwamba yeye yuko juu ya Katiba na Sheria na Watanzania wote. Kwamba anachofanya yeye ni sahihi na maaadamu Katiba inamlinda kwamba hatashtakiwa kwa lolote alilofanya akiwa Rais ajue kuwa kuna MUNGU ALIYE JUU YA YOTE akiwemo Magufuli mwenyewe, CCM na Serikali yake!! Rais JJPM lazima ajue kuwa hata Wapinzani ni Watanzania, ni ndugu zetu na maadamu Katiba inaruhusu vyama vingi lazima aheshimu uhuru wao wa kujieleza na awachukulie wapinzani kama sehemu ya Serikali yake maana kuna 40% waliochagua kusimama na Upinzani!!

Namshauri Rais aachane na Lugha za kuwatisha Watanzania hasa wapinzani kwa kuwaambia ati waache kuropokaropoka!! Rais amesikika akimwambia Spika Job Ndugai kuwadhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni kwa kuwatimua, na wakitimuliwa huko Bungeni yeye Rais atawadhibiti huku nje ya Bunge!! Tumeona yaliyotokea kwa Halima Mdee na Esther Bulaya kwa kufungiwa mwaka 1 kutokanyaga Bungeni na baada ya kuwa nje tayari Halima Mdee alikamatwa na kuwekwa mahabusu 48 hrs kwa Amri ya DC na tayari ana kesi ya kujibu Mahakamani!! Tumeona aliyekuwa PM wakti wa Kikwete Waziri Mkuu Lowassa akisumbuliwa kuhojiwa na Polisi kisa kutoa maoni yake kuhsu Masheikh waliko mahabusu zaidi ya miaka 4 leo!!wa CCM

Namshauri Rais aache kuwatumia Ma-DC na Ma-RC kunyanyasa wapinzani kwa kuwakamata na kuwaweka korokoroni kwa masaa 24 au 48 kwasababu ambazo hazina mashiko! Na hili limehsmiri sana kwenye maeneo ambayo yanaongozwa na Wapinzani!!Tumeona kilichotokea kule Hai baada ya DC wake kuharibu shamba la Mbunge wa Hai, Mwenyekiti wa CHADEMA(T) na Kiongozi wa KU-Bungeni Mhe. Freeman Mbowe kwamba sheria imechukua mkondo na DC huyu anatakiwa kulipa gharama za uharibifu 549m/- Tshs! Je, nani atalipa hiyo fedha? Je, ni DC, Serikali au Rais aliyemteua???

Kwa sasa Taifa liko kwenye taharuki. Manung'uniko yamekuwa mengi kuliko shangwe na furaha ya Utawala huu. Kuna nderemo na furaha kidogo sana kutoka kwenye mfumo wa Utawala wa CCM ambao kwa namna moja au nyingine ndiyo wananufaika na mfumo huu!! Wana wa Israeli baada ya manyanyaso na mateso makali toka kwa Utawala wa Farao wa Misri, walimlilia Mungu na akasikia mang'uniko na vilio vyao. Mungu alishuka na kuanza mpango mahsusi wa kuwaondosha Wana Israeli toka Misri kwa mkono wenye nguvu kuwapeleka nchi ya ahadi Kanani!! Juzi tumesikia Bungeni baadhi ya Wabunge wa Upinzani wakiliambia Bunge kuwa kama Serikali inaona Upinzani hautakiwi nchi hii, basi wabadilishe Katiba ili Upinzani ufutwe kabisa ili watu wajue moja kwamba hakuna Upinzani Tanzania kuliko kuendelea katika manyanyaso na mateso!!!. Naomba kuwasilisha.
 
Hii nchi sasa hivi kila mtu mwanasiasa hatuna muda maalum wa kudeal na siasa na muda wa kufanya maendeleo hatujifunzi kutoka nchi zilizoendelea wakimaliza uchaguzi....
Watu walioenda shule kuiacha siasa kwa wasioenda shule ndio imekuwa tatizo,wenye elimu watakwambia mimi na siasa tofauti ndio maana mabashite wanatuongoza kwasababu wao wameingia kwenye siasa na kuwa viongozi.na mtu yoyote hawezi kujitenga na siasa kwasababu siasa ndio inatupangia maisha iwe unataka au hutaki siasa itaathiri maisha yako kwa namna moja au nyingine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom