Mpendwa Mh. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Mwuungano wa Tanzania kwanza kabisa Rais wetu napenda kukupongeza kwa jitihada kubwa unazozifanya, kama Rais wetu wa awamu ya pili Mh. Ali Hassan Mwinyi kwenye hiyo clip niliyo itanguliza hapo juu ameeleza, za kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi na nchi yako Tanzania. Nakueleza haya Rais wetu ili utambue kuwa pindi mafanikio ya jitahada zako yatakapo onekana ulimwenguni, utakuwa umetuletea sisi na nchi yetu Tanzania sifa kubwa sana ya kutambulika ulimwenguni kwote na wewe jina lako kuto sahaulika milele.
Mh. Rais wewe ni mfano bora sana wa kuigwa ulimwenguni, kwani katika hii karne ya 21 sijawahi sikia binadam ambaye ana moyo wa ushujaa kama wewe ambaye kwa mapenzi na huruma kwa binadam wenzake na upendo kwa nchi yake kuwa tayari kuyaweka maisha yake kwenye risk kubwa kwa kupambana na makampuni au mataifa yanayo jiita giants katika vita vya uchumi wa kuokoa na kulinda rasilimali zetu kama wewe.
Mh. Rais napenda pia utambue kuwa kwa haya machache uliyo yafanya mpaka sasa umewafanya watanzania kuamini pia kuwa tumempata kiongozi ambaye mda mrefu tulikuwa tuna mlilia baada ya Baba wa Taifa Mwalim Nyerere na Waziri wetu Mkuu Mh. Edward Moringe Sokoine.
Pamoja na juhudi zako zote hizo za kizalendo unazozifanya kwetu Mh. Rais hata hivyo mimi binafsi huwa nasikitika na kusononeka sana moyoni na kupata maumivu makubwa sana sana, nikiona au kusikia watu unao waamini na kukupa matumaini yao makubwa kuwa wata-perform vizuri katika utendaji na utekelezaji wa mambo unayowataka wayafanye, inapokuja watu hao hatimaye wanakuangusha.
Kwa hali hii Mh. Rais, pamoja na kuwa upeo wangu wa kujua mambo mengi kuhusu utendaji wa kazi wa serikali na diplomasia ni mdogo ukilinganisha na wako, tukizingatia experience uliyoipata kama member wa cabinet zaidi ya miaka ishirini na sasa Rais wa nchi, hata hivyo kama mtanzania aliyezaliwa, kukua na kusoma mpaka kidoto cha sita Tanzania na baadae kupata elimu ya masomo ya juu, utaalam na uzoefu wa kazi Ulaya ambako baada ya kumaliza masomo yangu nilipata bahati ya kuishi na kufanya kazi kwa mda mrefu, ningependa kupata nafasi katika nafsi yako ya kunisikiliza machache ninayo taka kuyaeleza hapa chini.
Mh. Rais nasikitika kukueleza kuwa sisi watanzania tulio wengi, walio soma na wasio soma, kusema ule ukweli hatuna uwezo wa kutenda na kupanga mambo kama wewe unavyo taka au ungependelea tufanye. Mtanzania aliyezaliwa Tanzania na kusoma mpaka vyuo vikuu Tanzania na hata kama ameenda nje kusoma tu na kurudi, naapa kwa mungu ni wachache sana watakao weza perform vizuri mambo mengi kulingana na matakwa yako.
Utawateua na kuwaapisha wengi kushika madaraka makubwa na kuwapanganua kwa jinsi unavyotaka kuwapeleka huku au kule na kumpachika huyu hapa au pale, ukweli ni kwamba wengi wetu tutakukatisha tamaa tu, sio kwa sababu sisi hatuna akili, hapana, akili tunazo tena kubwa sana, ila sisi tunakosa fantasy ya maisha.
Nitaomba radhi kama nitakuwa nina wakwaza baadhi ya watu. Sijaja hapa kumlaumu mtu bali nimekuja kwa ajili ya kutoa mchango wangu wa kujaribu kupata ufumbuzi wa matatizo unayo kabiliana nayo katika kuwatafuta watu ambao watakusaidia vizuri katika utendaji wa kazi ili kufanikisha malengo unayotaka yatimike ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Kusema ule ukweli Mh. Rais tatizo letu limeanza na Azimio la Arusha mwaka 1967. Azimio la Arusha lilizaa ujamaa na ujamaa ulizaa wananchi ambao walikuwa tegemezi na hivyo kufanya mambo mengi yaende "sisi waswahili wa siku za nyuma twasema" mpesempese. Hiyo hali ya utegemezi ndiyo imetufanya sisi wengi wetu tudumae kiakili na kutokuwa na reasoning ability. Kwa bahati nzuri katika sakata hili hatuko peke yetu, nchi nyingi ambazo ziliamua kuchukua mfumo wa kijamaa, ki-comunism na ki-socialism duniani wanachi wao wana matatizo haya haya kama yetu. Najua wengi wataanza kupinga na kuja juu na kusema au kuuliza mbona wachina wameendelea?
Watanzania tusiyachukulie mambo kijuujuu tu. Siri ya maendeleo ya wachina sisi sote tunajua, sio wachina wenyewe kwa nguvu zao peke yao ndiyo zimeleta maendeleo kweye nchi yao, bali ni ndugu zao au wachina wenzao walio kuwepo kwenye provinces ambazo zilikuwa zimeendelea kiuchumi kama Taiwani, Hong Kong na Makao na pia nchi za nje kama Amerika, Japan na nchi za Ulaya kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo hayo. Kingine ni uamuzi ambao serikali ya china ilichukua ya kuifungua nchi yao kiuchumi, hiyo pia ilichochea maendeleo ya nchi yao. Ikumbukwe pia kuwa Hong Kong ilikuwa chini ya utawala wa uingereza, Taiwani waamerika na Makao wareno. Matatifa hayo tawala mfumo wao wa kiuchumi na maisha ni wakibepari (capitalism).
Baada ya kusema hayo Mh. Rais nisingependa kuondoa matumaini na malengo yako ya kuifikisha nchi yetu kwenye uchumi wa kati itakapofikia mwaka 2025, la hasha, ila ningependa kidogo tuangalie hali halisi ya uwezo wa watanzania wenyewe kielimu na mazingira yao na afya. Elimu yetu bado ni ndogo sana na mazingira yetu ya maisha bado ni dhaifu sana kuweza kubeba mzigo mkubwa wa ku-revolutionize nchi kuwa ya viwanda bila assistance na nguvu kutoka kwa watu wenye discipline ya kazi kama ya wanadiaspora. Sitaki kumkatisha mtu tamaa, lakini ukweli ni kwamba watanzania wa Bongo peke yetu hatutaweza ifikisha nchi yetu kwenye uchumi wa kati mpaka mwaka 2025. Hiyo nakataa kata kata!
Serikali yako na utajiri wake wote inaweza wajengea watanzania infrastucture nzima ya maisha, lakini nakuhakikishia Mh. Rais bila mabadiliko ya "mind set" yetu kipindi wewe utakapo ondoka tu, tutarudi tena kule kule tuliko toka, kwani unayo yafanya sasa Baba wa Taifa pia aliya fanya kwa uwezo wake. Naomba pia izingatiwe kuwa mabadiliko ya mind set ni process ya mabadiliko ya utamaduni wetu wa maisha na hii haiwezi ikaja mara moja. Inahitaji mda.
Ili tuweze fikia malengo hayo tunayo yataka kwa haraka ni lazima “radical methodes” zitumike kwenye kuleta mabadiliko ya mind set yetu kupitia nguvu za ndugu, watoto na wajukuu wa ndugu zetu watanzania wazalendo ambao wako kwenye nchi zilizo endelea kiuchumi bila kujali uraia wao na uwezo wao wa kiuchumi, cha umuhimu ni uzalendo, commitment na utayari wao wa kushirikiana na watanzania katika kuleta maendeleo ya uhakika kwa manufaa ya wote wanao itakia mema na kuipenda nchi yetu kwa dhati na upande mwingine ni uihari na dhamira ya serikali kuwawezesha wazalendo hao. Kwa vile nchi yetu haina mabepari wengi, ni jukumu la serikali kutoa incentives (Rehani) kwa wazalendo wetu kuwa na uwezo wa kuchukua mikopo huko wanakotoka kwa ajili ya kuwekeza nchini katika sekta mbali mbali za kiuchumi, sayansi, teknoloji na research na arts na culture.
Katika mkakati huu kazi kubwa ya serikali iwe kuleta impulse ya malengo yake kwa wanadiaspora ili mbinu zao mbalimbali za maisha walizo jifunza huko waliko zaliwa na kukulia wazitumie kwenye utekelezaji na mahitimisho ya maendeleo yetu. Hivi vizazi vya watanzania wenzetu vitatuletea discipline na spirit ya utendaji kazi kiufanisi wakishirikiana na watanzania halisi ambao hawaja pata nafasi ya kuona au kuishi katika manzingira hayo mengine.
Nathubutu kuchukua nafasi hii kutoa mchango wangu huu kwa sababu mimi pia ni mmoja wapo wa watanzania walio bahatika kushuhudia kuvunjika kwa ukuta wa Berlin na kuona maendeleo ya mwuungano wa nchi hizo mbili. Kama ambavyo nimesema hapo awali kuwa baada ya kumaliza masomo yangu niliendelea kuishi na kufanya kazi kwenye nchi hizo mbili zikiwa zimeungana na hivyo kupata nafasi ya ku-observe faida na hasara za mwuungano huo na kujifunza mambo mengi juu ya tofauti zao. Kitu kingine ambacho nilikishuhudia kipindi hicho nilicho ishi huko ni mapinduzi ya uchumi na teknolojia wa nchi ya kituruki hasa chini ya utawala wa Rais wao wa sasa Erdogan.
Wenzetu wachina na waturuki ni mataifa ambayo watoto na wajukuu wa watu wao waliozaliwa nje, iwe nchi yeyote ile ya Ulaya, Amerika au kwenye provinces kama Makao, Hong Kong na Taiwani, wanabaki kuwa ni wao na kwa hali hii inakuwa rahisi kwao kushirikishwa kwenye serikali za nchi wazazi wao wanatoka kwa moyo mweupe na kwa uzalendo mkubwa.
Nitoe tu mfano; watoto wengi wakituruki ambao wamezaliwa Ujerumani hata wale walioletwa na wazazi wao wakiwa wadogo na baadhi yao mimi nilibahatika kuwa nao masomoni, wengi wao walikuwa very patriotic na nchi ambayo wazazi wao wametoka na hatimaye baada ya kumaliza masomo yao wengi walienda kuijenga nchi ya wazazi wao kiuchumi na kuleta maendeleo ambayo sisi tunayaona leo nyumbani ya mradi wa SGR. Waturuki kwa uelewa wangu sio nchi ambayo wanatengeneza Treni, cha kujiuliza ni kuwa hiyo teknolojia ya kutengeneza treni wameipata wapi?
Ujerumani ime-play major role katika ku-transfer teknolojia hiyo uturuki na vizazi vya waturuki walio kwenda Ujerumani kutafuta maisha ndiyo waliohusika kwa asilimia kubwa zaidi. Of cause msimamo wa serikali ya Erdogan kushirikiana na wanadiaspora hao ndiyo ufumbuzi mkubwa sana katika kuhitimisha mafanikio waliyo yapata na sasa ni baadhi ya global player katika kuuza teknolojia yao.Hivi ndivyo maisha yanavyo function.
Ieleweke hapa kuwa Ujerumani baada ya vita kuu ya pili ya dunia iliwaleta waturuki wengi sana kweda kufanya kazi kwenye viwanda na makampuni yao. Vizazi vyao na baadhi ya watu hawa walibahatika kupata utaalam na wadhifa kwenye makampuni na viwanda vya wajerumani na hatimaye nchi yao ilipo funguka kiuchumi waliweza shirikiana na serikali yao au ya wazazi wao kuleta maendeleo yanayo onekana sasa nchini uturuki. Nacho taka kuonyesha hapa ni kuwa ieleweke generation hii ya vijana kutoka nje ndiyo iliyo wapelekea ndugu zao nyumbani ustaarabu na mwenendo wa kufanya kazi kwa ufanisi kama vile wazungu wa kwenye nchi ambazo walizaliwa na kupata utaalam.
Sisi watanzania wengi Mh. Rais, pamoja na kuwa tunaweza tukawa tumesoma sana na ma-PHD mengi mengi, lakini ukweli ni kwamba tunakosa maarifa ya kutransform yale tulio yasoma ambayo yako kwenye ubongo wetu kuyapeleka kwenye practical. Hatutaki kuumiza vichwa vyetu kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu. Tunatafuta mkato. Na kwa vile wengi wetu vitu vingi hatujawahi viona bado, hatuna reference ya kutosha ambayo itatuwezesha sisi kufanya vitu kwa kujiamini. Na ndiyo maana umejionea mwenyewe jinsi gani wasomi wetu wametuangusha katika swala la rasilimali zetu. Badala ya wao kutumia rasilimali zetu kuleta maendeleo ya nchi yetu wao wana wanufaisha mabepari. Inatia haibu kuwa na wasomi wa aina hiyo. Ni mara kumi kuwa wote mbumbumbu kuliko kuwa na wasoni ambao hawana manufaa kwa jamii. Ni waaribifu wa rasilimali zetu na egocentric!
Labda nikupe siri moja Mh. Rais, sisi watanzania hatuko innovative. Wengi wetu tuna tamaani kuishi kama ma-stars wa Amerika bila kujua njia walizo tumia ma-stars hao kufika hapo walipo. Na ndiyo maana tukipata nafasi ya kushika madaraka na hasa ya fedha, basi hapo kila mbinu zitafanyika hata kuuana sisi wenyewe kwa wenyewe ili dream zetu hizo zikamilike. Maisha ya watanzania wanyonge hapo hayahesabiki tena kwa watu wenye msimamo huo. Na ndiyo maana Tanzania inasifa mbaya sana Ulaya kuhusiana na watanzania wenzetu ambao ni Albinos. Ukiangalia kwa undani zaidi utaona wahusika wakubwa kwenye ushirikina huo ni hao hao wasomi wetu kwasababu ya kutojiamini.
Magufuli wewe sio binadam wa kawaida, wewe kwa matendo yako utakuwa mtakatifu tu Rais wangu, kweli nakuambia! Amini hilo!
Unajua Mh. Rais nimeguswa sana na pongezi ambazo Rais Ally Hassan Mwinyi amekupa kwenye hiyo clip. Ilinipa strong feeling ya ile story kwenye biblia ya Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake Misri kuwa yeye ni ndugu yao waliye mwuuza kwa mfanya biashara mmisri alipo kuwa mdogo na wote wakawa wamemzunguka na kumwinamia kama alivyo kuwa ametabiri kwenye ndoto yake ya utotoni. Hapo nafikiri walitambua power ya mungu wa baba yao Yakob ambayo Yosefu alikuwa nayo. Na hiyo ndiyo power uliyo nayo Mh. Rais ya kujiamini. Na ndiyo maana nakusihi Mh. Rais weka imani yako kubwa kwenye vizazi vya wanadiaspora. Discipline yao ya utendaji kazi waliyo nayo kutoka nchi walizo zaliwa na kupata experience ya maisha zitatusaidia sana sisi katika mikakati hii tunayo ifanya ya kulikwamua Taifa letu kiuchumi. Ieleweke kuwa wengi wao wana uzoefu mzuri wa maisha ya kuchapa kazi kwa ufanisi na mambo ya rushwa na uzembe wa kiafrika kama wetu sisi wengi wao hawana, kwani wana mwamko mwingine wa maisha ya kikazi na malengo yao ni thabiti.
Nasema hivi kwa sababu natambua mawazo waliyo nayo juu ya tabu na masononeko ya maisha ambayo wazazi wao wameyapitia ugenini na ambayo mimi naamini yamekuwa conserved kwenye genes zao na wish waliyo nayo kubwa ni kutaka kurekebisha makosa ya maisha yaliyo sababisha wazazi wao yawatokee. Hii generation mara nyingi inakuwa very, very, motivated. Ni generation ambayo imewaletea waturuki na wachina mafanikio.
Angalia mwenyewe Mh. Rais, juzi wewe mwenyewe umewapitia wavuvi Ferry na kuwasikiliza kero zao. Cha kujiuliza ni kwamba kwa nini wewe ufanye hiyo kazi watendaji wako wanafanya nini? Huo ni uthibitisho kuwa sisi peke yetu hatuwezi weka mambo sawa kwa sababu hatuna Reference. Hao wavivu wako huko Ferry miaka na miaka, lakini mpaka sasa hakuna hata mmoja amewaza kuwajengea ofisi kwa nini?
Tushirikiane na wanadiaspora. Mengine yote yatakuja yenyewe!
Asanteni sana!