Jambo Moja ambalo lipo clear ambalo Mie kwa upande wangu linaniudhi Ni vitu kupanda Bei na kutoongeza mishahara.Hili linaniudhi kwelikweli.
Ila wanasiasa hili la mishahara haliwahusu wao kilio Chao Ni demokrasia ili wapate fursa ya ajira (Ubunge & Udiwani)
Kiuchumi, kwa kawaida ("ceteris paribus" wanavyosema wenyewe wachumi), kuna mambo mawili yanayokinzana ambayo hayawezi kuambatana, mpaka kuwe na uchumi usio wa kawaida.
1. Kunaweza kuwepo na nafasi za kazi nyingi, ajira ikawepo bwerere, mishahara ikapanda kwa kanuni za kiuchumi za demand and supply (wafanyakazi wachache ajira zimewazidi, waajiri inawabidi waongeze mishahara kuvutia wafanyakazi). Hili ni jambo zuri kwa waajiriwa. Lakini, ubaya wake linapelekea bei za vitu kupanda. Wafanyabiashara wanaona watu wana hela, ajira zipo, wanapandisha bei. Watu watanunua tu bidhaa, kwa sababu hela wanazo. Hapo tunaona habari ya ajira kupanda kusababisha bei za bidhaa kupanda. You win some, you lose some.
Unaweza kulalamika bei za bidhaa zinapanda, lakini usilalamike sana, kwa sababu bei zimepanda kutokana na neema ya ajira kuongezeka.
Uchumi unauma na kupuliza. Wanasema uchumi unakupa mitihani na njia za kuikabili. Kama mtihani ni kwamba bei za vitu zinapanda, njia ya kuukabili mtihani ni kutumia uwepo wa ajira nyingi. Katika soko la ajira nyingi ukiona bei za vitu zinapanda sana unaweza hata kuacha kazi moja ukapata nyingine yenye mshahara unaoendana na kupanda kwa bei ya vitu.
2. Upande wa pili wa uchumi classical, under ceteris paribus (kikawaida, wanasayansi wanasema "Standard Temperature and Pressure" ) unasema kwamba:-
Kukiwa na ukosefu mkubwa wa ajira, kazi zikawa adimu, ujumla wa bei za vitu kupanda (inflation) utapungua. Kwa sababu, uwezo wa watu kununua vitu (purchasing power) utapungua, waajiri hawatapandisha sana mishahara. Wafanyabiashara wakipandisha bei, vitu vitadoda kununuliwa.
Hapa tunaona uchumi unauma na kupuliza tena. Kama uchumi umeuma kwa kukosekana kwa ajira, basi unapuliza kwa kufanya mfumuko wa bei kiujumla (inflation) upungue au kutokuwepo kabisa.
Kama nakusoma vizuri na kama nausoma uchumi wa Tanzania vizuri, uchumi wa Tanzania si wa kawaida. Haupo katika mafungu yote mawili hayo juu ya chumi za kawaida.
Kwa sababu, ni uchumi ambao una tabia mbili ambazo kikawaida hazitakiwi kufuatana pamoja, lakini kwa Tanzabia zinafuatana pamoja.
Uchumi wa Tanzania unaonekana kuwa na ajira ndogo, ambazo kikawaida zinatakiwa kudhibiti mfumuko wa bei, lakini Tanzania tunaona tuna ajira ndogo, halafu hapo hapo kuna mfumuko wa bei pia.
Hili linawezekanaje?
Hili linawezekana kama nchi ina intake kubwa katika soko la ajira kuliko soko la ajira linavyoweza kumudu kuichukua intake hiyo. Halafu hapo hapo infirmal sector haijawa imara kuchukua waliobaki.
Katika mfumo kama huo, ambao characteristicts zake ni population growth ya 2.5 - 3%, ambayo kwa sasa tushaipita (2017 figures zinaonesha population growth ya Tanzania ni 3.1%), ni vigumu kudhibiti ukosefu wa ajira, kwa sababu kika mwaka watu wengi sana wanaingia kwenye soko la ajira, lakini hawapati sehemu zinazoweza kuwachukua nankuwapa ajira.
Na hapo hapo, ni vigumu sana kudhibiti mfumuko wa bei, kwa sababu, kuna watu wengi tu wana ajira na biashara zao, na wana oesa nzuri tu za kuweza kutengeneza demand nzuri tu katika soko.
Hapo utaona kuna tatizo la mipango ya matumizi ya mitaji na uzalishaji. Kwa sabau, kati ya wale wale waliokosa ajira, kungekuwa na mioango mizuri ya kutumia mitaji kuzalisha, hao hao wangeajiriwa na kutumika kutengeneza bidhaa na huduma ambazo wangeuziana hao hao wenyewe.
Wengine wangeajiriwa vuwanda vya nguo, wakatengeneza nguo, wakawauzia wenzao. Wengine wangeajiriwa mashamba makubwa ya kilimo, wakakima, wakalisha wenzao. Wengine wangeajiriwa mahospitalini, wakatibu na kuhudumia wengine.
Wengine wangekuwa wanasheria, wakatisaidia kwenye mambo ya haki.
Tatizo letu tumekuwa na jamii iliyo na exclusivity.
Walimu wa Chuo Kikuu wanatamba kwamba Chuo Kikuu cha Dar hakijapata First Class shahada ya sheria kwa miaka thelathini, kama vike hilo ni jambo zuri.
Rais anaita watu vilaza, bila kujali ukweli kwamba mfumo wa elimu na maisha wa Tanzania unafanya hata mambo ya kawaida yawe magumu. Kitu kama ajira, ambacho kwa kweli ni haki ya msingi ya utu (human right) na kila mtu, mpaka watu wenye matatizo ya mtundio wa ubongo wanaofungiwa ndani, anatakiwa awe na ajira inayoendana na uwezo wake, vinginevyo tutakuwa tunajipunja wenyewe wote kama jamii.
Tukiweza kuondoa hizi habari za kizamani za kujutapa Chuo Kikuu hakijatoa First Calass degree ya sheria miaka thelathini au arobaini, tukijua kwamba tunaweza kujenga viwanda vyetu, tukatengeneza nguo zetu, tukauza nguo, anayenunua nguo anamlipa anayetengeneza nguo, anayetengeneza nguo anamlipa mkulima anayelima chakula, anayelima chakula anamlioa tabibu anayemtibu, na wote hawa ni wale wale wahitimu ambao bila kujioanga wangekisa ajira, tutaweza kufanya mengi.
What we have here is a failure if imaginatiin, leadership and organization.
Tuna tatizo la population growth pia, lakini hata hilo ukiliangalia sana halijafumuka kiasi cha kutuzidi (linaelekea huko).
Wangekuwepo viongizi wa maana wangejua kufanya excess population kuwa market ya bidhaa zetu, kwa kuipa ajira na pirchasing power.
Tatizo tuna a double whammy. Everywhere you look.
A weak currency to promote exports, but no exports.
High unemployment, but a quirky high inflation too.
Bad leadership, but a surprisingly complacent (and even jubilant) populace.
We are cut from a different cloth.