Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
hatimaye na wewe umetambua kwamba boss wenu kuna muda huwa anateleza.
Wakati watu wanachagua makabila kuna Siasa kubwa ya utani ambao unatufanya akili ya mwanadamu iwe inatikili kuwa KABILA moja ni Bora kuliko lingine... SASA turudi kwenye uhalisia wa mambo:

Siasa ya KABILA la wahaya linaponzwa Sana na kukubaliana na yote HAYA bwana hivyo kusifika Kwa Sifa (Mie tajiri Ila wewe Ndiyo unahela)

Ili tufanye KAZI Kwa bidii ni muda wa kuchunguza Sifa za makabila mengine ili namjua iwe na MAANA mathalani:

Wapate Sifa ukiitoa Kwa sumaye ni kuwa na maviwanja mengi yasiyo endelezwa hivyo lable ya NOPLAN ni MTAJI makubwa kwenye kabila hili labda Kwa sababu hatujui PARE panahitaji nini

Wachaga!? Hawana Dharau kweli! Sijui maana Chadema ndiyo mfano wa Aina ya Siasa inayotakiwa nchini tunatakiwa tier na RAIS WA maisha MAANA NYERERE alisema ni CHADEMA pekee insyoweza kuchachafya Hadi saizi mwenyewe ni tule tule na kama ni Chama cha mfano basi tuteuwe rais WA MAISHA Katiba siyo ishu ili CHaga zetu zifanye KAZI.. wake watu wa kisa langu liende Kwa mwingine..

Wahehe:!?

Wagogo!?

Wajinga!?

Wanyakyusa!?

Matatizo waliweka posts Tunatafuta KABILA linalotekeleza elimu Tanzania ili lituondolee hatha ya Kufanya KAZI zisizo na maana kama kutokuwa na Akira ni fursa, kuwa na MAISHA ya kombolela fursa, maisha ya NOPLAN fursa n.k

Tukishindwa figure za kuelewa zinahusu


 
Ndugu watanzania wenzangu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, awali ya yote namshukuru sana Mungu mwingi wa rehema na huruma kwetu sisi viumbe wake. Pia niwashukuru sana watanzania kwa heshima kubwa mliyonipatia mimi na Familia yangu, heshima ya kuwa Kiongozi wa hili Taifa ambalo Mungu ametubariki. Nafaham kuongoza Taifa kubwa kama hili sio kwa uwezo wangu binafsi ni kutokana na maombi na Dua zenu.

Pia Niwashukuru sana Viongozi wote waliopita akiwepo Mh Rais mstaafu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. Niwashukuru sana wasaidizi wangu akiwepo Mh Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri mkuu Mh Kasim Majaliwa, Mawaziri wote, Bunge, Mahakama, vyombo vyote vya ulinzi na usalama, pamoja na sekta zote za serikali na binafsi, Balozi mbali mbali zilizopo Nchini. Mmekuwa mdaada wa pekee katika kuijenga Nchi yetu. Ni Imani yangu kuwa Ushirikiano huu utaendelea kwa maslahi ya Taifa letu.

Ndugu Watanzania wenzangu, Tangu Kuingia Madarakani serikali tumejitahidi kufanya mambo mbali mbali kwa maslahi ya Taifa letu. Kama serikali mpaka sasa ndani ya kipindi cha Miaka minne tumefanikiwa mambo yafuatayo :

  • Kudumisha umoja na Mshikamano wa Taifa letu. Msingi wa umoja wa Taifa letu ulio asisiwa na watangulizi wetu tumeendelea kuudumisha.
  • Serikali tumeendelea kulinda mipaka ya Nchi yetu, pamoja na ushirikiano na Na majirani zetu.

Serikali tumefanikiwa kumalizia miradi mbali mbali iliyo achwa na Serikali ya Mh Kikwete sambamba na hilo tumeanzisha na kutekeleza miradi mbali mbali mikubwa ya Nchi kama ifuatavyo:

  • Kuanzisha mradi mkubwa Wa reli Standard Garge.
  • Ujenzi wa mradi wa umeme.
  • Miradi mbalimbali ya Ujenzi wa barabara.
  • Miradi ya hospitali, vituo vya afya, Zahanati. Pamoja na ongezeko la madawa.
  • Ufufuaji na Ujenzi wa viwanda mbalimbali Nchini.
  • Kuhamisha Ikulu na Serikali nzima kwenda Dodoma.
  • Uwezeshi wa wanafunzi kusoma kwa unafuu pamoja na ongezeko la idadi wa wanafunzi wanaopata mikopo ya elimu ya juu.
  • Kuboresha maslahi ya wakulima.
  • Serikali tumeendelea kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wananchi wa hali ya kipato cha chini.
  • Kuendelea Kuboresha maslahi ya wafanyakazi na bado tunaendelelea.
  • Kuanzisha Mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi.
  • Kudumisha Muungano wetu kwa kuendelea kuishi kwa amani na Upendo.

Sambamba na hayo yote Bado kama Nchi tumekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo :
  • Matukio mbalimbali yaliyo wakumba ndugu zetu ya watu kupigwa risasi na kupotea. Jambo hili bado vyombo vyetu vya ulinzi na usalama unaendelea kuishugulikia.
  • Tetemeko la ardhi lililo ikumba Nchi yetu na eneo kubwa la Bukoka kuathirika.
  • Mvua kubwa kuleta madhara makubwa na madogo.
  • Ajali za barabarani kuleta vifo na maumivu kwa watanzania wenzetu.

Pamoja na changamoto hizo na nyingine ndogondogo kama serikali kwa kushirikina na wananchi tunaendelelea kuzitatua na ikiwezekana kwa asilimia kubwa kuzizuia kabisa.

ndugu zangu watanzania wenzangu, Mabadiliko ya kiuchumi huja na changamoto mbalimbali, hivyo kama Nchi niombe Tuvumiliane ili kwenda pazuri zaidi ya hapa tulipo. Pia Hiki ni kipindi muhimu cha kuzidi kushikamana, na kuvumiliana ili tuvuke salama. Tutambue maadui tunao ndani na nje ya Nchi lakini kwa Mshikamano wetu tunaendelelea kuilinda Nchi yetu na watu wetu.

Asanteni kwa kunisikiliza MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU.

Wadau naashumu hii ndio Hotuba ya Rais ya miaka minne. Nilipo kosea mnikosoe. Mnapendekeza aongelee nini kingine?

Karibuni
 
Ni kweli Rais anafanya vizuri katika uwajibikaji wake lakini katika hotuba zake namshauri apunguze ukali wa maneno na kuwatukana waliomchagua.

Leo katoa kauli yenye utata kwa kisukuma baada ya kujibu "Mkatolwe" kwa kisukuma maana yake mkaolewe je ni sahihi kumwambia mwanaume mwenzako akaolewe? Tena mbele za watu?

Swali alikuwa ameshajibu vizuri ila akaongeza vikorombwezo yaani anaona ni sawa kuwaunganisha wanaume na wanawake kwamba wakaolewe?

Mimi sina tatizo na Rais Magufuli ila ajiulize kwanini wakati yule jamaa anauliza swali watu walikuwa wakimshangilia na yeye baada ya kujibu watu wakaa kimya? Kuna tatizo tena kubwa!
 
Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya huduma muhimu haiwezi kutafuta fedha kwa ajili ya kukulisha wewe na mke wako.
JPM -Leo Tabora
 
Usipate tabu mkuu!!..
images.jpeg.jpeg
 
Kwa niaba ya Wasukuma naomba msamaha.

Wasukuma ni watu tunaojivunia kuishi vizuri na watu, kauli njema, ukarimu, kuishi kwa kuchukuliana, kuizuia hasira, kufurahi na watu na kuheshimu maadili ya jamii.

Magufuli Si mara moja wala mbili. Amedharau maadili ya Kisukuma. Nawaomba msimchukulie kama mfano wa tabia za Wasukuma.

Tuna watu wengi wa Kisukuma waliotumikia taifa kwa utiifu na unyenyekevu.

Kina Paul Bomani, Chifu David Makwaia, Jaji Francis Nyalali, kutaja wachache tu.

Hawakuwahi kuwavunjia heshima Watanzania hivi.

O ntemi wise ate na masala gete!
 
usipo muelewa huyu mzee utapata tabu sana
huyu mzee ni mtu wa utani sana
Tushatoka "Hapa kazi tu" tunaingia "utani sana" ?

Utani kwa mkuu wa nchi ni suala delicate sana, halitakiwi liwe na habari za "usipomuelewe huyu mzee".

Rais anatakiwa awe clear, anaeleweka kirahisi.

Ukitaka watu wanze ku solve calcululus na kuagua habari kwa kusoma majani ya chai ili wamuelewe rais, huyo rais hafai urais na hajui mawasiliano ya kirais.

Mbona Nyerere alijua utani, alichekesha watu sana, aliwatania rafiki zake kina Kahama kwenye hotuba, lakini hajawahi kusema maneno yasiyo na staha kama haya?

Nyerere alihutubia akapiga utani na vijembe, watu wanacheka nusu dakika nzima.

Bila kutoa maneno yasiyo staha.
 
..ukiulizwa swali lazima amdhalilishe muuliza swali au amlishe maneno na kupotosha hoja ya muuliza swali.

..na ukitofautiana naye kimtizamo au msimamo lazima atatoa kauli za matusi, kwa mfano aliwahi kumtuhumu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuwa ana mawazo ya kishetani.
 
Naunga mkono hoja, japo most of the time huwa kama anatania lakini kiukweli utani mwingine ...
Hii hoja na mimi niliwahi kuuliza huko nyuma
P
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom