Ndugu watanzania wenzangu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, awali ya yote namshukuru sana Mungu mwingi wa rehema na huruma kwetu sisi viumbe wake. Pia niwashukuru sana watanzania kwa heshima kubwa mliyonipatia mimi na Familia yangu, heshima ya kuwa Kiongozi wa hili Taifa ambalo Mungu ametubariki. Nafaham kuongoza Taifa kubwa kama hili sio kwa uwezo wangu binafsi ni kutokana na maombi na Dua zenu.
Pia Niwashukuru sana Viongozi wote waliopita akiwepo Mh Rais mstaafu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. Niwashukuru sana wasaidizi wangu akiwepo Mh Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri mkuu Mh Kasim Majaliwa, Mawaziri wote, Bunge, Mahakama, vyombo vyote vya ulinzi na usalama, pamoja na sekta zote za serikali na binafsi, Balozi mbali mbali zilizopo Nchini. Mmekuwa mdaada wa pekee katika kuijenga Nchi yetu. Ni Imani yangu kuwa Ushirikiano huu utaendelea kwa maslahi ya Taifa letu.
Ndugu Watanzania wenzangu, Tangu Kuingia Madarakani serikali tumejitahidi kufanya mambo mbali mbali kwa maslahi ya Taifa letu. Kama serikali mpaka sasa ndani ya kipindi cha Miaka minne tumefanikiwa mambo yafuatayo :
- Kudumisha umoja na Mshikamano wa Taifa letu. Msingi wa umoja wa Taifa letu ulio asisiwa na watangulizi wetu tumeendelea kuudumisha.
- Serikali tumeendelea kulinda mipaka ya Nchi yetu, pamoja na ushirikiano na Na majirani zetu.
Serikali tumefanikiwa kumalizia miradi mbali mbali iliyo achwa na Serikali ya Mh Kikwete sambamba na hilo tumeanzisha na kutekeleza miradi mbali mbali mikubwa ya Nchi kama ifuatavyo:
- Kuanzisha mradi mkubwa Wa reli Standard Garge.
- Ujenzi wa mradi wa umeme.
- Miradi mbalimbali ya Ujenzi wa barabara.
- Miradi ya hospitali, vituo vya afya, Zahanati. Pamoja na ongezeko la madawa.
- Ufufuaji na Ujenzi wa viwanda mbalimbali Nchini.
- Kuhamisha Ikulu na Serikali nzima kwenda Dodoma.
- Uwezeshi wa wanafunzi kusoma kwa unafuu pamoja na ongezeko la idadi wa wanafunzi wanaopata mikopo ya elimu ya juu.
- Kuboresha maslahi ya wakulima.
- Serikali tumeendelea kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wananchi wa hali ya kipato cha chini.
- Kuendelea Kuboresha maslahi ya wafanyakazi na bado tunaendelelea.
- Kuanzisha Mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi.
- Kudumisha Muungano wetu kwa kuendelea kuishi kwa amani na Upendo.
Sambamba na hayo yote Bado kama Nchi tumekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo :
- Matukio mbalimbali yaliyo wakumba ndugu zetu ya watu kupigwa risasi na kupotea. Jambo hili bado vyombo vyetu vya ulinzi na usalama unaendelea kuishugulikia.
- Tetemeko la ardhi lililo ikumba Nchi yetu na eneo kubwa la Bukoka kuathirika.
- Mvua kubwa kuleta madhara makubwa na madogo.
- Ajali za barabarani kuleta vifo na maumivu kwa watanzania wenzetu.
Pamoja na changamoto hizo na nyingine ndogondogo kama serikali kwa kushirikina na wananchi tunaendelelea kuzitatua na ikiwezekana kwa asilimia kubwa kuzizuia kabisa.
ndugu zangu watanzania wenzangu, Mabadiliko ya kiuchumi huja na changamoto mbalimbali, hivyo kama Nchi niombe Tuvumiliane ili kwenda pazuri zaidi ya hapa tulipo. Pia Hiki ni kipindi muhimu cha kuzidi kushikamana, na kuvumiliana ili tuvuke salama. Tutambue maadui tunao ndani na nje ya Nchi lakini kwa Mshikamano wetu tunaendelelea kuilinda Nchi yetu na watu wetu.
Asanteni kwa kunisikiliza MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU.
Wadau naashumu hii ndio Hotuba ya Rais ya miaka minne. Nilipo kosea mnikosoe. Mnapendekeza aongelee nini kingine?
Karibuni