Habarini wana jamvi.
Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu mwema kwa kuitunza amani ya nchi yetu pamoja na watu wake kuwa watulivu kwa kipindi chote cha uchaguzi, ambao umeleta matokeo chanya kwa upande mmoja zaidi kuliko mwingine.
Pili nimpongeze Rais wetu kwa kuendelea kubalance mambo, yaani leo anakukera kesho unampenda tena.
Kwa analotukera tutazungumza na analotufurahisha tutalipongeza pia.
Katika ziara zake nyingi amekuwa na utaratibu mzuri sana wa kusikiliza watu wake yaani wananchi (wenye nchi), kwa utaratibu huu nampongeza sana maana haujawahi kuwepo kitambo sana.
Ila sasa, Mheshimiwa Rais unakosea hapa tu, unapenda sana kuwa na majibu yako tayari kichwani ambayo mengine ni ya kukera hasa kwa watu waliokata tamaa mtaani.
Mtoto wako sijui kama unaweza kumjibu kama unavyojibu watoto wa masikini huku mtaani. Kumbuka ushawahi kusema mwenyewe kuwa inawezekana nyumbani wewe ni mpole ukali unauonyesha huku kwetu tu.
Sasa basi angalia kwamba wewe ni kiongozi wa nchi na kumbuka wanaokuopenda sana ni wale walio kwenye system zaidi kuliko ambao hawapo kwenye system.
Sasa ambao hawapo kwenye system wanapotoa kero zao usiwajibu ovyo ovyo bali watie moyo. Unaposema wakalime, wakafanye kazi hivi hizo kazi zipo wapi?
Hayo mashamba yapo wapi? Umeenda Tabora waulize mvua zimeanza kunyesha lini? Ardhi ya nchi nzima ina rutuba? Pesa za kulima wanazo? Au bado una mawazo ya kilimo cha kizamani shika jembe ukalime?
Hao wananchi unaotaka wafanye kazi kumbuka wanatoka vyuoni, umewakopesha na pesa.
Kumbuka ulisitisha ajira ukaenda kununua ndege na kujenga mabarabara ya kutosha, mara madaraja, tumbua tumbua, vyeti feki n.k sasa ivi wamejaa mtaani unawaambia wakalime wakati tatizo lilianza unapolijua mwenyewe.
Cha kusisitiza hapa ni kutafuta njia nzuri za kuwapatia vijana hawa ajira maana hata kilimo kina wasomi sio kilimo cha kizamani.
Hawa hawa vijana ndio nguvu ya taifa. Baba akikosa hela atakuwa jambazi, mama akikosa huduma atakuwa malaya, watoto wakikosa matunzo watakuwa omba omba na chokoraa mtaani. Kazi kwako.