Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
mbna kama unachuki binafsi kwani kuna ubaya?
Chuki binafsi unaijuaje? Mimi siwezi kuwa na chuki binafsi na Magufuli, kwa sababu ni mtu aliyeifanyia familia yangu mchakato wa kuishi vizuri Tanzania, anajuana na familia yangu tangu akiwa Waziri.

Sasa chuki binafsi itoke wapi?

Naongelea ukweli, kwamba Magufuli hana kifua cha kujizuia kutotoa kauli zisizo na staha.

Unabisha?
 
Magufuli kashawahi kumbaashia Mama Salma Kikwete, kwenye hotuba.

Hapo wanaomtetea watasema alitania!

..alishamdhalilisha na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, yule Prof mwanamama.

..baadaye akamdhalilisha Mh.Dr.Janet Mbene alipotembelea jimboni kwake. Eti anamsifia ana sura nzuri. Kauli ambazo hazivumiliki ktk mazingira ya kikazi.
 
Wakati ana jibu huwa inategemea katumia mlevi gani muda huo,kama ni cha Arusha ndo anafyatuka kama alivyofyatuka
 
..alishamdhalilisha na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, yule Prof mwanamama.

..baadaye akamdhalilisha Mh.Dr.Janet Mbene alipotembelea jimboni kwake. Eti anamsifia ana sura nzuri. Kauli ambazo hazivumiliki ktk mazingira ya kikazi.
Jamaa ni bonge la mshamba fulani hivi.

Magufuli is a country bumpkin.
 
Leo pia alimwambia muuliza swali,kuwa anafanana na Chenge, na akaongeza kuwa labda Change alipita Igunga,!
huu ni utani ,sawa ila NI utani delicate Sana,unatakiwa uwe kwa watu waliozoeana ,kwa level yake hapana.
Hivi watoto walio sikiliza huo utani ...wanapata Nini!
 
Hajaanza leo kutukana , Akihutubia kwenye jimbo la Chato wakati ule akiwa waziri wa ujenzi , aliwaambia wazee waliomuomba kuwekwa lami barabara kuu ya eneo hilo kwamba , WAKUSANYE KINYESI CHAO WASILIBE BARABARA HIYO ILI IWE LAMI , na kwamba yeye si waziri wa eneo moja , hapo alikuwawala hajawa na ndoto ya kuwa Rais , sasa kishakuwa rais mtakoma .
 
Habarini wana jamvi.

Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu mwema kwa kuitunza amani ya nchi yetu pamoja na watu wake kuwa watulivu kwa kipindi chote cha uchaguzi, ambao umeleta matokeo chanya kwa upande mmoja zaidi kuliko mwingine.

Pili nimpongeze Rais wetu kwa kuendelea kubalance mambo, yaani leo anakukera kesho unampenda tena.

Kwa analotukera tutazungumza na analotufurahisha tutalipongeza pia.

Katika ziara zake nyingi amekuwa na utaratibu mzuri sana wa kusikiliza watu wake yaani wananchi (wenye nchi), kwa utaratibu huu nampongeza sana maana haujawahi kuwepo kitambo sana.

Ila sasa, Mheshimiwa Rais unakosea hapa tu, unapenda sana kuwa na majibu yako tayari kichwani ambayo mengine ni ya kukera hasa kwa watu waliokata tamaa mtaani.

Mtoto wako sijui kama unaweza kumjibu kama unavyojibu watoto wa masikini huku mtaani. Kumbuka ushawahi kusema mwenyewe kuwa inawezekana nyumbani wewe ni mpole ukali unauonyesha huku kwetu tu.

Sasa basi angalia kwamba wewe ni kiongozi wa nchi na kumbuka wanaokuopenda sana ni wale walio kwenye system zaidi kuliko ambao hawapo kwenye system.

Sasa ambao hawapo kwenye system wanapotoa kero zao usiwajibu ovyo ovyo bali watie moyo. Unaposema wakalime, wakafanye kazi hivi hizo kazi zipo wapi?

Hayo mashamba yapo wapi? Umeenda Tabora waulize mvua zimeanza kunyesha lini? Ardhi ya nchi nzima ina rutuba? Pesa za kulima wanazo? Au bado una mawazo ya kilimo cha kizamani shika jembe ukalime?

Hao wananchi unaotaka wafanye kazi kumbuka wanatoka vyuoni, umewakopesha na pesa.

Kumbuka ulisitisha ajira ukaenda kununua ndege na kujenga mabarabara ya kutosha, mara madaraja, tumbua tumbua, vyeti feki n.k sasa ivi wamejaa mtaani unawaambia wakalime wakati tatizo lilianza unapolijua mwenyewe.

Cha kusisitiza hapa ni kutafuta njia nzuri za kuwapatia vijana hawa ajira maana hata kilimo kina wasomi sio kilimo cha kizamani.

Hawa hawa vijana ndio nguvu ya taifa. Baba akikosa hela atakuwa jambazi, mama akikosa huduma atakuwa malaya, watoto wakikosa matunzo watakuwa omba omba na chokoraa mtaani. Kazi kwako.
 
Wabheja nkoi..
Lakini yeye ni mzilankanda sijui ndio kabila gani hili amelitaja leo.
 
Wabheja nkoi..
Lakini yeye ni mzilankanda sijui ndio kabila gani hili amelitaja leo.
Hivi naona ni vikabila vidogo vidogo vinavyokaa pembezoni mwa Wasukuma, watu wake wakiulizwa kabila gani, wengi hujitambulisha kama Wasukuma.

Nilishawahi kusema Magufuli si Msukuma.

Wasukuma ni watu wa kuwapa watu good time, si roho ya korosho kama huyu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom