Maoni ya mwananchi: Bima ya Afya kwa wote haitekelezeki, hata ikija ni ya wachache

Maoni ya mwananchi: Bima ya Afya kwa wote haitekelezeki, hata ikija ni ya wachache

Ni simple knowledge kwamba bima ni michango ya hiyari ambayo wanachama wataweza kusaidiana kupata huduma za afya urahisi.

Lakini swala linakuja ni michango,washirika na namna namna serikali itaweza kulifanikisha hilo jambo hapo bado kuna upigaji jambo ambalo CCM wameshindwa kabisa kudhibiti.

Bima adui yake mkubwa ni upigaji na rushwa. Na rafiki mkubwa wa bima ni uwekezaji mzuri wa pesa katika miradi au vyanzo vya uhakika vya mapato ambavyo vitawezesha mfuko kuzalisha pesa zaidi na kuwa na ziada. Sio kutegemea michango ile ile.

Sasa unakuwa na serikali inayochota tena michango hiyo hiyo ikalipe walimu, ikanunulie viongozi magari ya mabilioni hiyo bima mtatoboa?
"Serekale" iweke Kodi ya bima ya afya ya kiasi cha 200USD kwa Kila gari linaloingizwa nchini.

...."Watu mnasema hamna hela wakati namba E zimejazana barabarani"?
 
Makundi maalumu ndio akina nani tena hao ?
Aliyeleta maada, kidogo hajaweka ufafanuzi mzuri, ndo maana watu mnahoji Maswali mengi kupita kiasi.

Bima Afya kwa wote, imegawanyika sehemu 3.

1. Watu wanaojiweza watachangia/kufungua kadi kwa Tsh 150000.
2. Makundi maalumu ( walemavu, wasiojiweza, wazee kuzia miaka 60/65, na mama mjamzito)
3. Wanafunzi na wanachuo - hii itabaki vile vile kama mwanzo 50400

Namna ya kuwapata makundi maalumu :-
1. Walemavu, hili lipo wazi tayari wanajulikana

2. Watu wasiojiweza, hii watapatikana kupitia TASAF, maana watu wote waliosajiriwa na TASAF basi moja kwa moja itajulikana wapo kwenye makundi maalumu.

3. Wazee na watoto chini ya miaka mitano hii inajulikana toka mwanzo kuwa tiba zao ni bure.

Kwa hiyo basi kwa maelezo hayo, tutaaza na majaribio kwa makundi malumu kama nilivyo taja hapo juu, baada ya hapo wananchi wa kawaida watafuata, kutoka kwenye shillingi 30000 hadi 150000/-

Namna ya ulipaji wa fedha kwa makundi maalumu,
1. Serikali italipa hela zote kwenye mfuko wa NHIF, hivyo hakutakuwa na madeni inayodaiwa. 🤝🤝.
 
Back
Top Bottom