Makundi maalumu ndio akina nani tena hao ?
Aliyeleta maada, kidogo hajaweka ufafanuzi mzuri, ndo maana watu mnahoji Maswali mengi kupita kiasi.
Bima Afya kwa wote, imegawanyika sehemu 3.
1. Watu wanaojiweza watachangia/kufungua kadi kwa Tsh 150000.
2. Makundi maalumu ( walemavu, wasiojiweza, wazee kuzia miaka 60/65, na mama mjamzito)
3. Wanafunzi na wanachuo - hii itabaki vile vile kama mwanzo 50400
Namna ya kuwapata makundi maalumu :-
1. Walemavu, hili lipo wazi tayari wanajulikana
2. Watu wasiojiweza, hii watapatikana kupitia TASAF, maana watu wote waliosajiriwa na TASAF basi moja kwa moja itajulikana wapo kwenye makundi maalumu.
3. Wazee na watoto chini ya miaka mitano hii inajulikana toka mwanzo kuwa tiba zao ni bure.
Kwa hiyo basi kwa maelezo hayo, tutaaza na majaribio kwa makundi malumu kama nilivyo taja hapo juu, baada ya hapo wananchi wa kawaida watafuata, kutoka kwenye shillingi 30000 hadi 150000/-
Namna ya ulipaji wa fedha kwa makundi maalumu,
1. Serikali italipa hela zote kwenye mfuko wa NHIF, hivyo hakutakuwa na madeni inayodaiwa. π€π€.