Maoni ya wajumbe 'walio wachache' katika Kamati namba Nne iliyowasilishwa na Mhe. Tundu Lissu!

Maoni ya wajumbe 'walio wachache' katika Kamati namba Nne iliyowasilishwa na Mhe. Tundu Lissu!

dah! kazi kwelikweli,vijana wenzangu tuna Kazi kubwa sana,kwani na sisi pia hatufanyi utafiti wala upekuzi wa kawaida tu,yaan tumeshikiwa akili zetu na wanasiasa,na ndio maana humu tunatukanana bila ya sababu za Msingi,Mimi nimemsikia Tundu Antipas lissu mwanasiasa machachari kabisa,lakini sasa ilikuwa ni jukumu letu vijana kabla ya kulishabikia hili tulichunguze kiundani,na kujiuliza maswali mengi,je kama UN hawatutambui kama jumhuri ya muungano wa tanzania, huwa tunafanya nao Kazi vipi? au nao hawajui wanachokifanya? maana lissu alitaja watu wawili tena kwa majina na si UN kama UN, na pia lissu anasema watu waliozoea uongo vya ukweli hawaviwezi,naye tumuulize alipokuwa kwenye bunge la budget na kusema shirikisho haliwezekani,vipi Leo anapigania shirikisho!

Hivi kipindi kile ulipoacha shule tukiwa darasa la nne, kisa somo la uraia , ulijiendeleza? hivi Zanzibar ni member wa FIFA
 
Leo kikao cha bunge maalum la katiba kimeshindwa kuendelea baada ya kukatika kwa matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni ya Taifa na kulalamikiwa na wajumbe kundi la wachache wanaotaka serikali tatu ambapo taarifa yao ya kamati namba nne ndio ilikuwa ikiwasilishwa.
Mwenyekiti Samwel Sitta alisema lengo la bunge kuingia mkataba na TBC ni kutaka Wananchi waone kila kinachotokea ndani ya bunge ili kuwezesha kupatikana kwa katiba bora ambayo mwisho wa siku Wananchi wataipigia kura ili kutoa maamuzi ndio maana akatoa tangazo la kusitisha kikao.
Alisema ‘kwa sababu yoyote ile hatuwezi kuendelea, natoa maelezo tusikilizane… natoa maelekezo kwa katibu kuangalia muda ilipozimika na Mh. Tundu Lissu alikua anaongea ili Jumatatu tutakapo rejea nimpe Lissu nafasi ya kwanza kuweza kumalizia'
Baada ya Tundu Lissu kuanza kuongea na matangazo ya live kwenye TV (TBC) kukatika, yalianza kutoka malalamiko kwamba yamekatwa makusudi ili kuvunja nguvu ya maoni ya wachache wanaozitaka serikali tatu.

Nje ya ukumbi wa bunge katibu wa baraza la habari Tanzania (MCT) ambaye pia ni mjumbe wa bunge hilo Kajubi Mukajanga akatoa tamko kwa kusema ni jambo la kusikitisha na la aibu, naongea kama Mjumbe na pia Katibu wa baraza la habari… kitendo kilichofanyika leo mpaka hapo tutakapo pata ushahidi kwamba kweli kulikua na tatizo la kimitambo'
‘Ni kitendo cha aibu na kuhujumu tasnia ya habari, haiwezekani mawazo haya yakarushwa…… mawazo haya yasirushwe kwa sababu watu waliopewa majukumu ya kusimamia kituo cha taifa (TBC) wanadhani kwamba hawayapendi mawazo hayo' – Mukajanga.
Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Samwel Sitta leo alikua katika wakati mwingine mgumu hapa bungeni Dodoma baada ya kulazimika kutuliza wajumbe wa bunge hili mara kwa mara wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kamati namba nne kuhusiana na sura ya kwanza na sura ya sita za rasimu ya katiba mpya.

Hisia hizo mara kadhaa zimekuwa zikiibuka miongoni mwa wajumbe pale unapozungumziwa muundo wa muungano huku taarifa ya wajumbe wengi ikiunga mkono muungano wa serikali mbili na wajumbe wachache wakiunga mkono muundo wa shirikisho uliopendekezwa na tume ya mabadiliko ya katiba ya kuwa na serikali tatu.
Licha ya kutuliza hisia hizo pia mwenyekiti wa bunge alilazimika kumtaka mmoja wa wajumbe wachache wa kamati namba nne kusoma maoni ya wachache baada ya msomaji wa maoni ya wengi kukataliwa kusoma maoni hayo.

Namkariri Mh. Sitta akisema >> ‘kama unavyoona mwenyekiti wa kamati namba tatu unachokoza vurugu ndani ya bunge na muda umefikia mwisho kwa hiyo malizia sasa, kwa kuwa wachache mmemkataa mwenyekiti wa kamati namba tatu kusoma nawapeni dakika 15 nyinyi wenyewe msome hayo mambo yenu'
Baada ya ruhusa hiyo ya mwenyekiti, mjumbe Mchungaji PETER MSIGWA akapata nafasi ya kuwasilisha maoni ya wachache na kutoa ufafanuzi kwa dadika 45 badala ya 30 zinazopendekezwa na kanuni za Bunge Maalum la Katiba.

Akiwasilisha maoni ya wajumbe waliowengi wa kamati namba nne licha ya kukatizwa na kelele za baadhi ya wajumbe mwenyekiti wa Kamati hiyo ameeleza kuwa ni vigumu kuwa na shirikisho la serikali tatu kwani litadhoofisha au kuua kabisa muungano.
Sehemu ya alichoongea akiwasilisha ni >> ‘hawa watu wanaosema hati ya muungano ni batili, kwanza ukishasema hati ni batili manake muungano ni batili, manake bunge hili na jamuhuri ya muungano ni batili, wanafanya nini humu????? waondoke!

Chanzo.. Millard ayo website
 
Swala la kwamba Nyerere ni Muongo lipo wazi tumelisema sana Hapa lakini tukaonekana wadini....
Haya Leo Tundu Lisu kasema Nyerere ni Mzushi na muongo PRO CHADEMA mmesikia ?

Umeona eeeh, mimi ndio nnawaambia leo kikowapi?

Tunapodadavua maovu ya Nyerere humu huwa wanatushambulia.
 
Matangazo yalikatika pale Tundu Lissu alipotaka kutoa ushahidi kwamba hati ya Muungano haipo.........................
 
Nikimsoma kwa umakini Lissu nasema Nyerere aliudanganya umma wa Watanganyika. Kumbe hata hati ya Muungano hakuna, sasa kwanini aliung'ang'ania?

Kwa mara ya kwanza nakugongea like na cheki inbox kuna zwwadi yako...nimependa kweli hii post yako..ntaiprint niiweke kwenye archieve
 
Alipomsikia Lissu anataja mpaka ukurasa eti naye akawa ana note! ina maana kasahau au?

hiyo ni zuga, aibu kwa wasom wa nchi hii ambao hawasimamii kwenye msingi ya kweli, maprofesa wote walioko ccm hamna tofauti na darasa la nne
 
Sisi Wazanzibar hatutaki TBC iturushie matangazo ya Bunge maalum,tupeleke ZBC wauturushie,TBC ya bara wanatunyima haki yetu

Nyie mmezoea kuwa wakwezi wa kina Jussa subirini wadude wanaodai serikali tatu washinde!
 
nashauri tbc waanze kulipwa na wana ccm wanaofaidika na chanel hiyo kuliko kulipwa na kodi ya wantanzania ambao hawana faida na tbc,wtz tunaomba star au itv ndo ziwe luninga za taifa .
 
Tanganyika yetu tunaitaka pronto!Propaganda za akina Shivji aliyeshusha heshima yake hazina nafasi.Tnganyika kwanza.
 
Back
Top Bottom