Wabunge wa CCM ni wanafiki kukemea maovu yaliyobainishwa na taarifa ya CAG wakati hawataki kurekebisha katiba na kubadilisha mfumo wa utawala ambao umezaa uwakilishi haramu ambao kazi yao kubwa ni wizi na ubadhirifu wa mali ya umma
Ukitindua mfumo kwa kuleta uwajibikaji watendaji wabovu kama hawa wanaopigiwa ukelele wangelikuwa wapigakura wamemalizana nao kwenye masanduku ya kura siyo kwenye mipasho ya wabunge bungeni
Tulisema kuendelea kukopa hela kwa ajili ya maendeleo ni ufujaji wa mali ya umma kwa sababu mfumo huu wa wizi wa kura umefifilisha uwajibikaji sasa kuna faida gani ya kukopa kama hela inaenda kuliwa
Karibu miundombinu yote iliyotapakaa nchi nzima haina viwango. Hela imeliwa sasa kiongozi anaposema mikopo ina tija wakati fedha za mikopo hiyo zinatafunwa na malengo yake hayatekelezwi ipasavyo itabidi tujiulize huyu mwenzetu anaishi nchi gani?