Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Wabunge wa CCM ni wanafiki kukemea maovu yaliyobainishwa na taarifa ya CAG wakati hawataki kurekebisha katiba na kubadilisha mfumo wa utawala ambao umezaa uwakilishi haramu ambao kazi yao kubwa ni wizi na ubadhirifu wa mali ya umma
 
Watawala wetu hawataki kuirekebisha katiba kwa sababu wanajua hawana sifa za kuiongoza nchi hii
 
Na uwakilishi haramu una uadui na Mwenyezi Mungu na chochote wanachofanya kamwe hawatafanikiwa
 
Mapato yatashuka hata hiyo Trilioni 7.1 wataisikia kwenye bomba
 
Hoja ya wabunge ya kuwatimua baadhi ya mawaziri siyo mwarobaini
 
Timua timua bila ya kurekebishwa katiba na kuchochea uwajibikaji ni ulaghai mtupu
 
Mwaka 2015 na 2020 CCM ilizuia uwajibikaji pale ilipoizua Tume ya uchaguzi kuhesabu kura na matokeo yake kuheshimiwa
 
Ufisadi uliobainishwa na taarifa ya CAG unathibitisha tatizo la nchi hii ni la kimfumo siyo la kiuendaji
 
Ukitindua mfumo kwa kuleta uwajibikaji watendaji wabovu kama hawa wanaopigiwa ukelele wangelikuwa wapigakura wamemalizana nao kwenye masanduku ya kura siyo kwenye mipasho ya wabunge bungeni
 
Tuwe wa kweli na ni ukweli tu ndiyo utatuopoa hapa tulipokwama
 
Tulisema kuendelea kukopa hela kwa ajili ya maendeleo ni ufujaji wa mali ya umma kwa sababu mfumo huu wa wizi wa kura umefifilisha uwajibikaji sasa kuna faida gani ya kukopa kama hela inaenda kuliwa
 
Karibu miundombinu yote iliyotapakaa nchi nzima haina viwango. Hela imeliwa sasa kiongozi anaposema mikopo ina tija wakati fedha za mikopo hiyo zinatafunwa na malengo yake hayatekelezwi ipasavyo itabidi tujiulize huyu mwenzetu anaishi nchi gani?
 
Tufike mahali tukiri utitiri wa taasisi kama TAKUKURU, bodi za mikopo, EWURA, bima ya afya zinapaswa kufutwa maana hazina tija
 
Sana sana tunawapatia watu hususani makada wa CCM ajira na ulaji lakini taasisi hizo haziwezi kutekeleza majukumu kusudiwa
 
Tume zote za kupambana na jinai kama madawa ya kulevya n.k ni wizi na ubadhirifu wa mali ya umma hazina uwezo wa kupambana na uhalifu.

Hivyo, polisi warudishiwe kazi zao
 
Back
Top Bottom