Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Je anajua kila shilingi mia inayokwenda kwenye mfuko wa bima ya afya shilingi 40 huishia kuliwa na gharama za kiutawala na hivyo kamwe mfuko wa bima hautamletea unafuu mlaji wa hii huduma?
 
Je anaweza kutuorodheshea nchi hata moja duniani ambayo mfuko wa bima unaendesheka? Kila mahali tunaona safu za viwavi jeshi zimepangwa kuutafuna
 
Marekani 70% ya hela ya Obamacare hutafunwa bila hata ya kuwafikia walengwa sasa sisi nchi ambayo hata Ummy Mwalimu naye ni Mheshimiwa Waziri si ndiyo kwisha habari yake?
 
Kama mwenza wa kiongozi wa kitaifa analipwa mafao ya kustaafu serikali ina hoja zipi kila mtumishi wa umma aliyestaafu mwenza wake asilipwe mafao ya kustaafu
 
Kama viongozi wa kitaifa hulipwa mafao ya kustaafu 80% ya mshahara wa sasa wa aliyepo madarakani tungependa kujua kwanini watumishi waliobakia wa umma wasilipwe 80% ya mshahara wa sasa kwenye cheo walichoondokea
 
Kwa lugha nyingine kwanini wastaafu wa kawaida wawekewe kikotoo cha malipo tofauti na viongozi wa kitaifa?
 
Ilimbukwe nchi hii inajaribu kujenga nchi ya ujamaa na kujitegemea na ubaguzi kwenye utumishi wa umma kwa kutunga sheria zenye kujenga matabaka ni kukiuka misingi ya usawa iliyoainishwa kwenye katiba
 
Uteuzi wa Bashite sasa unamkebehi ofisi ya uteuzi na washauri wake
 
Sasa tunaufahamu wa kutosha wa vipawa vya Bashite baada ya takribani ya miaka 5 ya ukuu wa mkoa
 
Tunajua Bashite yawezekana ana vipawa vingi sisi hatujui lakini cha utawala hicho tunajua kaputi
 
Sasa asiye na kipawa cha utawala unalazimisha awe mtawala si ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe
 
Tangia Bashite ateuliwe tunajionea ututusa wake na kutuacha na maswali mengi magumu ya ofisi ya uteuzi
 
Wahenga hutukumbusha mgema ukimsifia tembo hulitia maji
 
Kila mahali anavikwa vilemba vya ukoka lakini utendaji wake ni wa kusuasua
 
Kama Bashite anaonekana ni jembe ndani ya sisiemu basi chama ni mfu
 
Back
Top Bottom